Rais Samia Suluhu Hassan tusaidie kutengua kitendawili cha wasiojulikana

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,368
23,525
Toka awamu ya tano iingie madarakani matukio ya kutekwa, kushambuliwa na kuuawa yalikuwa yakidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana.

Hadi hii leo ninapotoa ombi langu hili kwako, watekelezaji wa vitendo hivyo vya kutisha hawajaweza kubainika ni akina nani zaidi ya wasiojulikana.

Katika hiyo miaka mitano utekaji, mateso na mauaji tumewapoteza wananchi lukuki na mara zote vyombo vyetu vya usalama vilidai ni wasiojulikana.

Nakuomba uunde tume huru kufanya uchunguzi ili uweze kutegua kitendawili cha hicho kikundi hatari cha watu wasiojulikana ili waweze kujulikana.
 
Task force na genge la bashite ndio wasiojulikana.

Task Force kuwazingua wafanyabiashara - rejea issue ya kuvamiwa zakaria - kuwapora mali zao.
Genge la bashite - Kuwashughulikia waliokuwa wanakosoa utawala wa jiwe au kumkosoa JIWE.
 
N
Toka awamu ya tano iingie madarakani matukio ya kutekwa, kushambuliwa na kuuawa yalikuwa yakidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana.

Hadi hii leo ninapotoa ombi langu hili kwako, watekelezaji wa vitendo hivyo vya kutisha hawajaweza kubainika ni akina nani zaidi ya wasiojulikana.

Katika hiyo miaka mitano utekaji, mateso na mauaji tumewapoteza wananchi lukuki na mara zote vyombo vyetu vya usalama vilidai ni wasiojulikana.

Nakuomba uunde tume huru kufanya uchunguzi ili uweze kutegua kitendawili cha hicho kikundi hatari cha watu wasiojulikana ili waweze kujulikana.
Naunga mkono hoja yako mkuu.
 
Kule yule aliyeteuliwa na kuengeliwa haikupita masaa 24 kabla ya kuapishwa.
 
Vyote huyo mama anaweza kufanya, lakini sio kufuatilia hilo genge maana linafahamika wazi kuwa lilikuwa kundi la jiwe. Na akiweza kufanya hilo atajizolea uungwaji mkono wa ajabu ndani ya nchi hii. Lakini kwa mazingira yalivyo akina Mwigulu, Kabudi, Mpango nk hawawezi kukubali maana wanajua mengi ya kundi hilo, na hata kuwa na baraka zao kwenye hilo kundi chafu.
 
Nchi ipo kwenye vita ya kiuchumi halafu wanakuja watu wanasaliti,nyinyi wanajeshi mnajua mnapokuwa vitani kwenye mapambano af anatokea mmoja wenu anageuka nyuma,nadhan Cha kumfanya mnakijua,hiyo ilikuwa wakati anatoa hotuba yake pale alipokuwa anapokea report ya kamati ya uchunguz wa wizi wa madini ikulu,few hours later tunaskia tundu lisu anashambuliwa na risas bungeni na watu wasiojulikana,

Indeed it was very dark period,dear lord Asante KWA kusikiliza vilio vyetu
 
Uzuri sie watz ni waoga na wapole sana, hatuna makuu hata wakishikwa mkono wakawekwa hadharani wala hakitatokea chochote hasa hasa tu tutakuwa tumepata ubuyu mpya.

Watekaji watesaji wa Dr ulimboka waliwekwa hadharani hadi simu zao, hata hawa wa sasa sio kwamba hawajulikani kiiivo, wachache wanajulikana wanadunda tu mtaani.

Nadhani tunahitaji ubuyu tu na si kingine au nasema uongo ndugu zangu?
 
Toka awamu ya tano iingie madarakani matukio ya kutekwa, kushambuliwa na kuuawa yalikuwa yakidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana.

Hadi hii leo ninapotoa ombi langu hili kwako, watekelezaji wa vitendo hivyo vya kutisha hawajaweza kubainika ni akina nani zaidi ya wasiojulikana.

Katika hiyo miaka mitano utekaji, mateso na mauaji tumewapoteza wananchi lukuki na mara zote vyombo vyetu vya usalama vilidai ni wasiojulikana.

Nakuomba uunde tume huru kufanya uchunguzi ili uweze kutegua kitendawili cha hicho kikundi hatari cha watu wasiojulikana ili waweze kujulikana.
Kwani wewe unajulikana? Acha kwanza wewe kujulikana kisha na hao wasiojulikana wenzako wajulikane, kwanini watizama kibanzi kwenye jicho la jirani yako wakati jicho lako linabolt.
 
Back
Top Bottom