Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,432
118,840
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwaletea hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni wito wa ustaarabu kwa Rais Samia, rais Samia Suluhu, sio malaika, ni binadamu kama binaadamu wengine wote na anaweza kukosea kama binaadamu wengine wote, kwa kufanya makosa ya kibinaadamu, hivyo nashauri, tusimfanyie nongwa, tusikalie kumlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa madogo madogo kabisa ya kawaida ya kibinaadamu, kwasababu binadamu wote huwa tunakosea, na hakuna mkamilifu.

Ila pale ambapo rais Samia amefanya makosa ambayo sio ya kwake, yale makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake au vyombo vyake, yakiwemo vyombo vya uteuzi vyenye jukumu la kufanya vetting, kwa baadhi ya watu wa hovyo hovyo kukwaa uteuzi, sio sawa, sio haki kumlaumu na kumshutumu mteuzi tuu yaani Rais Samia, nashauri kwanza, tumuonyeshe Mama Samia kuwa amechomekewa mabomu, kisha tumuonyeshe hayo makosa na makorokocho ya baadhi ya wateule wake walivyo wa hovyo, kisha tu project the consequences za kuwa na viongozi mabomu, kisha tumvumilie kwa tumpe muda wa kutosha kuwa atarekebisha mwenyewe yale makosa madogo madogo with time.

Tukiona ameambiwa makosa yake au makosa ya wateule wake, tukimkosoa kwa a constructive criticism tukamuonyesha the right thing to do, na kuonyesha madudu ya wateule wake, na yeye akiwaona bado wanamfaa, tuheshimu maamuzi yake, tusimpangie kwa jinsi ile ile ambayo hatukumpangia mtangulizi wake, lakini kwa sababu tutakuwa tumeainisha the consequences, hizo consequences zikija kutokea, tunakuwa hatuna jinsi, bali kumtundika msalabani!.

Declaration of Interest
Humu jf, kumezuka mtindo, ukisifia tuu jambo lolote zuri la viongozi wetu, unanyooshewa vidole kuwa unausaka uteuzi wa u-DC, na ukikosoa lolote, unanyooshewa kidole cha hizo ni hasira za kuukosa uteuzi!.

Naomba ku decrare interest, mimi Pascal Mayalla nikisifia, sisifii ili kuutafuta uteuzi, wowote wa nafasi yoyote, wanaosifia kwa ajili ya kutafuta uteuzi, kazi yao itakuwa ni kusifia tuu mwanzo mwisho na kamwe hutawasikia wakikosoa lolote!.

Mimi husifu tuu pale penye kustahili sifa na hukosoa kwenye makosa, ila ukosoaji wangu ni constructive cricitisim, nikikosoa naonyesha kosa, hapo hapo sio tuu nashauri nini cha kufanya, kurekebisha makosa, pia hutoa couscous statement ya the consequences if ushauri hautafuata, nini kitatokea!, hivyo ushauri ukipuuzwa likatokea la kutokea, unakuwa hauna jinsi, ni kumtundika msalabani kwa spana za kutosha!.

Mimi kwa shughuli zangu za PPR, nachangia fedha za kiasi cha kutosha kuwalipa mishahara ya mwaka mzima RC, DC na Mkurugenzi!, sasa mtu kama huyu, autafute u DC wa nini?!. Japo kwa sasa, nakiri kupigika sana lakini kwa mtu kama mimi, kitu ninachokihitaji kwa Mama, ni kuendelea tuu kuboresha mazingira ya biashara, PPR irudishe zile tenda zake, tumsaidie Mama, kumlipia mishahara ya ma RC, ma DC na Wakurugenzi wake!.

Japo mkubwa ni jalala, na ukiwa kiongozi ni lazima uwe na ngozi ngumu, lakini tusimsakame saana Mamaa kwa makosa ambayo sio makosa yake bali ni anakuwa ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!.

Pili, Rais Samia sio malaika ni binadamu tuu, kama binaadamu wengine wote, hivyo na yeye kama binadamu, anaweza kukosea kama, binadamu wengine wowote, hivyo anapokosea anahitaji kusaidiwa kwa kukosolewa kwa lugha ya kistaarabu, staha na heshima kwa kumuonyeshea kosa, ushauri wa kurekebisha, namna bora zaidi ya kulifanya hilo jambo, na the consequences of mapuuza endapo atapuuzia!.

Pia tujenge tabia ya uvumilivu wa kuyavumilia makosa madogo madogo ya kibinaadamu, to err is a human nature!.

Nakiri kupandisha bandiko kufuatia kelele nyingi za shutuma, lawama, kumsakama Mama Samia kwenye uteuzi wa baadhi ya watu. Mfano ni bandiko hili

What the hell is wrong with you Samia?

Shameful! Repulsive! Disgusting!

And shame on you Samia! Are you proud of appointees like this?

Are you that morally bankrupt? You don’t care? Don’t give a damn?

=====

Hakuna watu wanaomsaidia Rais @SuluhuSamia kufanya vetting ya ma DC kabla ya kuingizwa kwenye PDF?

Soma Gigy Money amponda Alberto Msando kuhusu video iliyovuja akimpima oil
View attachment 1827155
Mkuu Nyani Ngabu, kwanza naunga mkono hoja ya vetting, Mama amepelekewa makorokocho, na yeye bila kujua ni makorokocho, akateua tu.

Kuna baadhi ya makorokocho hayo, sababu ya uteuzi wao ni mchango wao kwa CCM, Msando amefanya kazi mzuri iliyotukuka kwenye ile kamati ya mali za CCM.

Hayo makorokocho na Gigy ni personal private matter akiwa under influence of alcohol. Kuvuja kwa hizo video ni kuingilia privacy zake, kama tutapekenyeua privacy za kila mtu kwa kutumia a hidden camera, hakuna msafi, na hakuna atakayebaki !.

Mwisho, with due respect, umetumia lugha kali mno na very harsh kwa mtu gentle kama Mama Samia.

Maneno kama
"What the hell is wrong with you Samia?"
"Shameful! Repulsive! Disgusting!"
"shame on you Samia! Are you proud of appointees like this?"
"Are you that morally bankrupt? You don’t care? Don’t give a damn?"
are unclalled for kwa mtu mwenye sifa kama za Mama Samia, wote tunajua vetting hafanyi yeye, yeye analetewa tuu majina, hivyo maneno makali haya, hayamstahili, mtu mwema, mpole, mstaarabu, mwelewa, mnyenyekevu kama Mama Samia.

Na kwa kuongezea, tofauti kubwa ya mwanaume na mwanamke sio physiological on sex tuu ya being male and female, bali ni psychological, men thinks, women feels, ukimtukana mwanaume kwa maneno makali hata matusi, mwanaume can take it na isiwe a big deal, kwasababu ana ngozi ngumu, lakini kwa mwanamke, it's not, wanawake wana ngozi laini, hivyo naomba usiyalize yale macho, laini, legevu, ukayarowesha kwa machozi, utatuumiza wengi!. Please lets spare this lovely lady kwenye baadhi ya mambo.

Just look at her Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!

Nasisitiza tusimtoe machozi mtu mwenye macho haya... Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?

Hitimisho
Kama ambavyo hatukumpangia Magufuli, nashauri pia tusimpangie Samia, tuepuke matukano, lugha za machukizo, ukali kebehi, kubagaza, tuendelee kumkosoa kwa lugha ya heshima, staha, kistaarabu kwa nia ya kujenga, huku tukikosoa constructively kwa nia ya kujenga huku tukishauri, the right thing to do.

Paskali
 
Makosa mengine unaona kabisa kuna tatizo sehemu na hyo sehemu isiporekebishwa itatuletea matatizo huko mbele ya safari ... sehemu yanyewe ni katika teuzi zake mpk unajiuliza hv kuna vetting kweli au kuna madalali wa hz teuzi ? Unafanya teuzi less than 24hrs unatengua teuzi yako, kuna watu wengine mpk unajiuliza hv huyu kweli?

Hakuna jambo la hatari kusafiri porini usiku huku taa za gari zote ni mbovu kwa maana haziwaki au zinawaka na kuzima akumbuke wateuzi wake ndio taa zake akifikiria 2025 ambayo hakuna alieiona, akashindwa kufikiria maisha ya kila siku ya watu milion 60 binafsi naona kabisa tuendapo Mwanga wake ni mdogo sana kulinganisha na tulipotoka.
 
Mibavicha ndio haina akili kabisa!

Mwanzo ilikuwa inamsifia sana! Alipofanya uteuzi wa kuwateua kina Nassari na Lijuakli ndio ikawa kama mbogo!

Nawaulizeni nyie mabavicha, hivi mlifikiri mama atafanya kwa matakwa yenu na si ccm?
 
"Tusimalumu kwa makosa ya kukoseshwa"

Lakini mbona hayo makosa ya kukoseshwa yamekuwa mengi sana kwake kwa muda mfupi aliokaa madarakani tofauti na watangulizi wake, hapa naona bado kuna tatizo la msingi mahala, tusimkwepeshe majukumu, atakoseshwa mpaka lini?

Kuanzia kwa yule mkurugenzi wa TPDC aliemuondoa muda mfupi baada ya uteuzi, yakafuata mengine hapo kati, mpaka kwa haya ya uteuzi wa wakuu wa wilaya, hii kitu inaonesha kuna udhaifu mahali unaojirudia na utamuharibia asipokuwa makini.

Hapa naona ni either hana last say kwenye teuzi anazofanya, au amekuwa mpole sana wa kupitishiwa majina na kuyakubali kwa ile huruma ya "mama kwa wanae", au ameshindwa kuendana na nguvu ya ushawishi/ushindani wa makundi yaliyoko ndani ya chama chake kwa kutaka kuridhisha kila kundi.

Mama Samia anatakiwa awe makini zaidi na hao wasaidizi wake, asiogope, awe na msimamo hata kama hautawafurahisha wengi chamani, japo naunga mkono hoja kwenye lugha inayotumiwa kumkosoa, isiwe kali sana, kwani nae ni binadamu ana udhaifu wake kama tulivyo wengine.
 
daima huwa nasema kuna watu hawana nia njema na nchi hii.

mama akifanya linalowafurahisha wao ni kelele kikubwa mwendazake amekosolewa.

wao furaha yao ni kuteseka kwa kundi linaloishi ndotoni mwao la sukumagang,ambalo kiuhalisia halipo na wala halipati tabu kama wanavyofikiri.
 
Inashangaza Sana waliokuwa wanamsifia Magufuli hata alipokuwa anateua watu Wana kesi huko USA za human rights abuses ..
Na kufoji vyeti ndo hao wanataka kumpangia Samia nani wa kumteua ...

Magufuli alisema asipangiwe na kila mtu akaufyata..
Samia kila mtu anataka kumpangia..
 
Pasco Mayalla sasa ni Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM. :)


Nimekuelewa sana hapa kwenye ^makosa ya kukoseshwa^ Kumbe kweli Bi Mkubwa amekalia kiti cha JPM, lakini kalamu aliyoshika ni ya Mstaafu wa Msoga. Hii ni hatari kwa afya ya taifa letu.
 
Kwakweli hawamtendei haki Mama, anajitahidi sana kazi anayoifanya sasa sio ya kubeza nafikiri sote tunaona jinsi kesi zinavyopanguliwa na mambo mengine kama hayo.

Tumpe muda na tumsaidie kwa kufanya kazi zetu kwa weledi.
 
Mkuu mi sikubaliani na wewe,Uraisi ni taasisi,sio mtu mmoja,

Haya mambo ya kuamka na kufsnya teuzi kama vile anateua shoga zake wakwenda nae ngomani yanakera,

Unateuaje viongozi waovyo,ambao clip zao wakifsnya mambo ya hovyo mtaani zipo kibao,hao intelligensia wanafanya Kazi gani!?Kwanini hateui watu kama Antony Mtaka,unaenda kutuletea Almasi Nyangasa! kwa kipi kikubwa alichofanya?

Kipindi Bety Mkwasa anateuliwa kuwa DC,nchi ilimuona kwa juhudi zake za kutoa Elimu ya ukimwi,sasa Hawa Kina Nick wa pili, Mwaipaya, wamefanya nini?

Kwanini anateua watu wa hovyo kabisa, si bora hata Ukampa Diamond unaibu waziri. Nchi inawatu milioni 50+,unateua mijitu ambayo Haina accomplishment yoyote duniani, zaidi ya Swaga za ujana, wapo vijana wadogo Wana PHD, masters zao kwenye vyuo, wapo vijana wanapiga biashara kama Vunja bei, kwanini uwapi hao vyeo kwenye wilaya za kimkakati Ili walete Mawazo mapya,Hawa kina Mwaipaya, sasa hv wanawaza jinsi ya kuongeza kiwanja,kumaliza nyumba ya kupanga, hakuna kitu hapo
 
Back
Top Bottom