Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,058
- 2,623
Rais Samia,
Pole na kazi ngumu ya kujenga taifa (ujasiriadola) katika mazingira mapya yenye changamoto lukuki.
Kazi ya kujenga nchi inahusu kuuliza na kujibu maswali yapatayo kumi hivi, mojawapo likiwa:
"Katika safari yetu ya kusukuma gurudumu la maendeleo kuelekea kwenye kilele cha mlima wa maisha bora nani atatekeleza majukumu gani na kwa nini?"
Leo naomba nikupe salama moja tu. Ni kuhusu umuhimu wa kuweka wazi hati za majukumu ya mawaziri na watumushi baki wa umma.
Jambo hili linajibu sehemu ya "kwa nini" katika swali hapo juu.
Umeshawateua mawaziri na manaibu wao, kwa pamoja wakiwa ni 50 tangu 08 Januari 2022.
Kuna maprofesa 3, madokta 8, elimu baki 39; wanawake 13, wanaume 37; wabunge wa majimbo 41, wabunge wa viti maalum 4, na wabunge wa kiteuliwa 5; na kuna Wazinzibari 2, Wabara 48.
Vyombo vya habari vinafanya tathmini kwa mtindo wa kuaminisha umma kuwa kuna mikoa umeibagua.
Mfano, gazeti la Mwananchi la juzi Jumamosi limetaja mikoa ya Morogoro, Rukwa na Geita.
Pia mitandao ya kijamii inaasema kuwa Mkoa wa Pwani umepata mawazi na manaibu 5 wakati mikoa baki ina wawili wawili, mmoja mmoja au zero zero. Kwamba umependelewa.
Picha inajengwa kwamba katika uteuzi wako umefanya ubaguzi na upendeleo dhidi ya baadhi ya makundi ya watu au dhidi ya mikoa fulani.
Dawa ya kutibu mawazo haya ya kubahatisha ni kuweka bayana hati ya majukumu ya wateule wako.
Hati hiyo itabainisha sifa za mtu anayepaswa kuteuliwa, majukumu yake, mipaka ya majukumu yake, na mambo kama haya.
Kwa vile sasa serikali mtandao inasonga mbele vizuri, nashauri hati za majukumu tuwekewe kwenye tovuti za serikali kama vile tovuti ya ikulu, tovuti za wizara, tovuti ya Bunge na kadhalika.
Baada ya hapo sisi wapambe wako huku Simbawanga na kwingineki tutakuwa tunakudatisha (kukuhabarisha) kuhusu kasi ya wateule wako na lini wanapotoka nje ya reli.
Tutatekeleza jukumu letu kwenye mlinganyo wa uwajibikaji na uhasibikaji (responsibility and accountability equation).
Nakutakia kila jema.
Mama Amon,
Simbawanga mjini.