Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,111
- 26,002
MODS naomba msiuunganishe mada hii na nyingine.
Mimi mmoja wa waathirika moja kwa moja wa kusuasua kwa TANROADS, na amana yangu inaelekea kuuzwa na benki kutokana na TANROADS kushindwa kutulipa.
Hali ya kusuasua na kuelekea kufa kwa TANROADS ni hali ambao haijawahi kutokea toka Taasisi hii ianzishwe mwaka 2000.
Kuanzishwa kwa TANROADS kulitokana na sera nzuri za serikali wakati huo kuwawezesha wazawa kushiriki moja kwa moja katika ujenzi wa hasa barabara.
Miaka ya 70, na 80 uujenzi wa barabara ukifikiriwa mara zote watu walikuwa wanawafikiria kina MOWLEM(walijenga Pugu Rd, sasa Nyerere rd), Stirling Astaldi(Italians), Fredericci (Italians),SOGEA (French), COGEFA SPA(Italians).
Makampuni mengi ya ujenzi wa barabara yalikuwa ya ki-Italiani.
Mpaka ukawepo msemo kati ya watu kuwa ulitaka barabara ijengeke mpe mtaliani.
Lakini kwa umakini Serikali iliona jinsi fedha zake zikienda nje kwa kasi ya ajabu maana fedha zote za ujenzi hata barabara ndogo zilikuwa zinaenda nje.
Rais Mkapa(Mungu amrehemu) ndiye aliyekuwa na ujasiri wa kuziweka sera za ujenzi kwa kutumia fedha zetu wenyewe kwa kuanzia namna ya kukusanya fedha na jinsi ya kuzitumia kiamilifu ili kujenga barabara nchini
Mkapa alizanisha utaratibu wa kukusanya fedha kwa kutumia ROAD FUND ambayo ilikusanya fedha kupitia mauzo ya mafuta.
Mkapa vile vile alianzisha TANROADS, taasisi ambayo ingekuwa ya kitaalam kubuni, kusimamia zabuni na kusimamia kitaalam miradi ya ujenzi na kuwasimamia makandarasi.
Yes, makandarasi.
Na hapo ndipo ninaingia.
Makandarasi wazawa walijiandikisha kwa wingi kuingia zabuni za ujenzi wa miundombini na hata matengenezo ya miundombinu iliyoharibika.
Makandarasi wengi wameichukulia TANROADS kama ndiyo sekta rasmi ya serikali kufanya nayo kazi, na kwa miaka zaidi ya 20.
Fedha hizo wanazopata makandarasi wazawa, ni lazima zingeenda kwa waItaliani.
Lakini sasa wazawa wamejijenga na familia zao na kuwekeza nchini mambo mengi ambayo yameongeza mzunguko wa fedha za ujenzi nchini.
Tukumbuke kuwa sekta ya ujenzi inachangia GDP over 13.5%(2015) ya uchumi wa nchi.
Hivyo basi hii Awamu ya 6 kwa sasa imefanya vibaya katika sekta hii ya ujenzi katika kuwashirikisha wazawa.
Kwa sasa hivi makandarasi wengi nyumba zao ziko sokoni, wengine zimeuzwa tayari. Kufanya kazi na serikali(TANROADS0 kumekuwa kuchungu mno hasa mwaka huu.
Hali hii hatujaiona zaidi ya liaka 30.
Hatumung'unyi maneno na hili si suala la kichama wala kisiasa pamoja na kwamba wengine sisi ni makada wa chama.
Toka rais Mkapa aanzishe TANROADS, akaj Kikwete,Magufuli mambo yalikuwa shwari, Serikali ilitekeleza majukumu yake kisawasawa kupitia Taasisis hii.
Kufa kwa TANROADS Mama Samia na Awamu ya 6, hamtakosa lawama.