Rais Samia azindua shule mpya Bumbwini Zanzibar na kuipa jina la Makamu wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Balozi Seif

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,193
3,248
Siku ya leo Rais Samia amezindua shule mpya ya Sekondari huko Bumbwini Zanzibar na wakati anazindua shule hiyo Samia ameomba shule hiyo iitwe Balozi Seif kwa ajili ya kumuheshimisha makamu wa Urais wa pili kutoka Zanzibar Balozi Seif.

Rais Samia amesema:

"Nilipoingia niliona kipande cha mbele cha hii shule kitupu hakina jina. Nikasema mbona hawa hawajaweka jina wasije wakanishtukiza kule wakasema wanaiita Samia hii ntawakatalia pale pale. Nikasema nimepata wazo.

"Jamani makamu wa pili mstaafu amefanya kazi kubwa ndani ya nchi
Na sijapita pahali nikaona kitu kimeitwa balozi Seif. Niwaombe ndugu zangu shule hii tuiite balozi Seif"


 
Usikute ni kodi za Watanganyika hizo ndiyo zinaenda kuwajengea hao urojo miundombinu ya kila aina. Yaani Mwalimu alifanya kosa kubwa sana kutuunganisha na hawa kupe.
 
Nyerere alituuza hapa ila waliomfuata wanatunyanyasa sana wadanganyika.
Mla urojo halipi kodi ila anasamehewa deni la nishati, kikotoo hakimhusu, kikotoo cha tra kwa waagiza magari hakimkabi koo kama wadanganyika, miradi mikubwa inatembea siyo kama Isaka-Mwanza SGR, deni la taifa ni 0 siyo kama tilion 92.
 
Tunaomba majengo mengine yanayofuata moja liitwe Abdul na lingine liitwe mzee Ameir bila kumsahau shemeji yetu Wanu.
 
Back
Top Bottom