Rais Samia awa kivutio mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
26,225
19,119
Ndugu zangu Watanzania,
Rais Samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita ameendelea kuonyesha namna Dunia inavyotambua mchango wake chanya katika maendeleo ya bara la Afrika. Dunia imetambua ya kuwa Rais Samia ndio Nembo ya Afrika.

Katika mkutano wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia ya nchi unaoendelea kule Dubai umemfanya Rais samia akose muda wa kupumzika au kufanya mambo yake binafsi. Hii ni kutokana na misururu ya viongozi mbalimbali kutoka kila pembe ya Dunia kutaka kuonana naye na kufanya naye mazungumzo walau hata kwa dakika chache tu,kila mtu anataka kusalimiana naye na kupata neno kutoka kwake na picha ya pamoja.

Amekuwa ni kivutio na kiongozi aliye upendezesha mkutano huo na kuuteka,uwasilishaji wake wa hoja hapo jana wakati akifungua mpango wa matumizi ya nishati safi pamoja na kuwaonyesha documentary inayoelezea athari ya matumizi ya kuni kwa mwanamke au mtoto wa kike barani Afrika imewakuna wengi na kugusa mioyo ya wahudhuriaji wengi ambao wameendelea kukoshwa na uwezo mkubwa wa kiakili na maono wa Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan.

Katika muendelezo wa kupigana vikumbo kwa viongozi mbalimbali ili kupata nafasi ya kuonana na Rais samia jana makamu wa Rais wa Marekani alifanikiwa na kupata bahati ya kuonana na kusalimiana na Rais samia na kuchota busara kutoka kwake.ikumbukwe ya kuwa Rais Samia Ndiye Rais mwanamke pekee kutoka bara la Afrika na aliyeonyesha uwezo mkubwa sana wa kiuongozi uliyogusa maisha ya mamilioni ya watu na kuwaletea maendeleo makubwa ndani ya muda mfupi sana.

kabla ya hapo katibu mkuu wa UN Antonio Guterres naye alipata bahati ya kuonana na Rais samia na kufanya naye mazungumzo ya muda mfupi kutokana na Rais samia kubanwa kiratiba na hivyo kutoa dakika chache za kufanya maongezi pale mtu anapomuomba kufanya hivyo.

Tuendelee kufuatilia mkutano huo ambao kiukweli Rais wetu ndiye nyota wa mkutano huo na ambaye Anategemewa sana kimawazo katika mkutano huo kutokana na uzoefu wake mkubwa alio nao. Ndio maana kila kiongozi anahamu na kiu ya kutaka kupata picha ya kumbukumbu arejeapo kwake kwa kupiga na Rais samia. Ndio maana hata vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vimekuwa karibu sana kuchukua matukio anayoyafanya Rais samia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
MKuu anagombewa wanajua shamba halina mlinzi!
 
Weka picha ya video hapa.
 
we jamaa sijawahi kuona umeongea point kama mtu mzima mwenye akili, ivi huwa unajielewa?
 

Siku hixi JF ina ruhusu ‘takataka’ kama hizi kukaa humu bila kufutwa?
Kweli JF imepoteza dira aisee
 
Jitahidi braza huku Halmashauri hamna kitu, komaa upate uteuzi uwe hata DED wetu..!!!

#YNWA
 
Wewe chawa inaonekana hata dunia hujui ilivyo. Busara gani wanazona kwake. Ukabila, Udini, wizi, uchu wa madaraka, nchi iliyozungukwa na mito na mziwa lakini iko gizani ukosefu wa umeme na maji,.....
 
Wewe chawa inaonekana hata dunia hujui ilivyo. Busara gani wanazona kwake. Ukabila, Udini, wizi, uchu wa madaraka, nchi iliyozungukwa na mito na mziwa lakini iko gizani ukosefu wa umeme na maji,.....
Wapi huko kusiko na maji na umeme? Nani umesikia KAFA kwa kiu ya maji? Mamvua yote haya yanayoendelea kunyesha unaanzia wapi kusema kuwa mji hayapo? Au unataka serikali ije ikuchotee maji hapo ulipo? Hujaona namna serikali ya Rais samia ilivyowekeza mabilioni ya pesa kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama? Mwakani pia bwawa la mwalimu Nyerere linaanza kutupatia megawati 2115 kwa hiyo habari za kukatika kwa umeme itabakia katika vitabu vya historia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…