kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,838
- 7,722
Rais Samia kwenye hotuba yake kupokea gawio za mashirika ya umma na yale yenye hisa za serikali kuna mambo amesema yanatia mashaka. Kwanza kufuatana na msajili wa mashirika hazina ni asilimia ndogo tu ya mashirika yametoa gawio kwa hivyo hapo bado hali ni mbaya vigogo wengi bado wanakula mashirika kama vile wao ndio wamiliki. Isitoshe CAG kwenye ukaguzi wake alionyesha ubadhirifu mkubwa kwenye mashirika kwa hivyo hili onyesho la kupokea gawio bado ni onyesho tu kupata pointi za bure kisiasa.
Jambo lingine ni pale rais akitamba juu ya kukopa. Ametamba kwamba ataendelea kukopa eti riba ni ndogo sifuri pointi kadhaa tu, na muda wa kulipa ni mrefu. Niulize hivi lini mabepari wa benki wakawa na urafiki na masikini. Mama awe mchunguzi na kufanya kazi na watu wenye weledi na uzalendo maana kuna wasiwasi anakopa mikopo kausha damu huku vigogo wanaoingiza nchi madeni wakifahamu na kufaidi binafsi. Wenye kukopesha mikopo kausha damu watakwambia riba ni asilimia kwa mfano 5 huku wakikuficha taarifa nyingi.
Wanakuja kukwambia umeshakopa riba ni asilimia 5 kwa mwezi sio kwa mwaka. Unakuta kumbe kuna mtandao kuanzia benki yako kuzuia mafao yako kwa mfano ya ya kustaafu. Unajikuta umefanya ujinga maana hata ukienda mahakamani mtandao wao uko unadhulumiwa mafao yako yote ya kustaafu au unaporwa mali kama nyumba na mali yako. Unajikuta umekopa shilingi milioni 20 mwisho wa siku unadaiwa milioni 400. Kwa nchi vizazi vinajikuta mapato yanaishi kulipa madeni ambayo pia hawaoni cha maana kinachoweza kuitwa maendeleo.
Lingine serikali imejiachia juhudi za kujitegemea kila kitu waziri ni kukopa. Utasikia majisifu TRA wamevunja rekodi ya makusanyo na mama kusifiwa kwa kutapanya fedha mikoan eti za maendeleo. Huko mikoani kazi ya vigogo imekua sio kukamilisha miradi kwa muda na ubora ila ni kubuni namna ya kula hela za umma na ikishindikana mwisho wa mwaka hela zinabaki hazitumiki zinatafutiwa namna ya kupigwa. Mkuu wa mkoa Makonda Arusha ameona hilo baada ya kugundua hela nyinyi hazijatumiwa wakati wananchi wana kiu kubwa ya maendeleo.