radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,438
- 32,249
Afrika iliishindia Ufaransa kombe la Dunia, na Ulaya inafaa kusitisha ubaguzi dhidi ya wahamiaji kulingana na rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
Akizungumza katika mji mkuu wa Caracas, chombo cha habari cha kitaifa kilimnukuu akisema.
''Timu ya Ufaransa ilishinda ijapokuwa ilikuwa kama ya Afrika . Ukweli ni kwamba Afrika ilishinda-wahamiaji wa Afrika waliowasili nchini Ufaransa, natumai Ulaya itapokea ujumbe huo''.
''Ulaya haifai kuwabagua Waafrika, hakuna ubaguzi dhidi ya wahamiaji. Ufaransa iliishinda Croatia 4-2''.
Mwaka 2016, mwaka mmoja baada ya shambulio baya la kigaidi, mchezaji wa zamani wa Ufaransa Louis Saha alisema kuwa Ufaransa ingali nyuma ya mataifa mengine katika kukabiliana na ugaidi.
Ni mara ya pili Ufaransa imejishindia taji la kombe la dunia. Kabla ya kujishindia taji la 1998 kiongozi wa mrengo wa kulia Jean-Marie Le Pen alikuwa amewakosoa baadhi ya wachezaji wake akiwemo Zinedine Zidane ambaye ana mizizi ya Algeria.
Alikuwa amesema kuwa wengi wao walikuwa wageni ambao walikuwa hawaimbi wimbo wa taifa kabla ya mechi.
Kwa upande wangu:
Hivi kwa mfano france isingechukua ubingwa hizi kelele zingekuwepo?
Bado naona ngozi nyeupe hii kitu imewauma sana naona wao ndo wanafanya ubaguzi na kauli zake za kitoto.