Lamisa Danish
JF-Expert Member
- Nov 17, 2019
- 284
- 627
Kwako Mama yetu Mh Rais,
Mm nikiwa kama Shabiki yako namba moja,mkereketwa wako Kindaki Ndaki na mpiga debe wako niliejitolea kukusemea,kukutetea na kukuunga mkono Juhudi zako zote za kuliletea maendeleo taifa letu,Nina haya machache kwako nikiomba uyatupie jicho.
Kwanza
Wafanyakazi wa Nchi hii wanajituma sana ktk kufanya kazi ili kujikimu wao na familia zao,wakati huohuo wakisaidia kulijenga taifa kupitia kodi zao wanazokatwa kabla hata ya kuchukua mishahara yao.
Wamekuwa pia wakilipa kodi kila wakinunua bidhaa mbalimbali madukani,masokoni, kwenye vyombo vya usafiri nk.
Ikiwa yote hayo hayatoshi bado na sasa hivi Wafanyakazi wamekuwa wakilipa TOZO kwenye miamala yao wanayoifanya wanapohamisha fedha kwenda kwa ndugu zao na jamaa zao mbalimbali waliopo vijijini.
Wamekuwa wakifanya haya yote kwa moyo mmoja,bila kujali vipato wanavyopata ktk mishahara hiyo midogo isiyokidhi mahitaji,ila wameendelea kuwa watiifu wakitii mamlaka bila shuruti ukizingatia serekali ya awamu ya tano haikufanya nyongeza yeyote ktk awamu yake.
Pamoja na yote hayo ya kiwango kidogo cha mishahara ukilinganisha na mifumuko ya bei ya bidhaa mbalimbali nchini,TOZO,ulipaji wa kodi kwa wakati nk nk bado kuna suala LA mifuko ya Jamii kama vile NSSF,PSPF nk nk huko pia fedha zinakwenda kutoka kwenye mshahara wa huyu mfanyakazi.
HOJA YANGU ni kwamba nashauri hii mifuko ianzishe Mikopo kwa wafanyakazi ili hii mikopo iwasaidie kufanya mambo yao kama UJENZI wa Nyumba,Kufungua biashara ili kupunguza ukali wa maisha nk nk.
Kwa mfano,Mfanyakazi akiwa amechangia Million 30 aruhusiwe kukopa robo or nusu ya fedha zake ili aweze kufanya mambo yake ingali akiwa na nguvu sababu mnakuja kumpa MTU hela zake uzeeni ameshachoka na hana anachoweza kukifanya sababu nguvu zimeshamuishia na hela zenyewe nyingi.
Huyu MTU hawezi tena kufanya biashara,wala lolote na hapo ndipo wengine huitwa baby na kujikuta pesa zake zinatapanywa ilihali ujanani aliishi kwa tabu.
Faida ya kufanya hivi ni kwamba Hawa wafanyakazi wakishapewa hii mikopo wataizungusha na kuongeza mzunguko wa fedha kuisadia serikali katika suala LA uhaba wa ajira uliopo sasa.
Jambo LA Pili Mh Rais,ni kwa Hawa Wazee waliostaafu or walioacha kazi kwa namna moja ama nyingine wasicheleweshewe kupewa fedha zao,unakuta MTU amefanya kazi ana kadi ya Uanachama siku anataka apewe pesa yake anatakiwa alete barua ya Muajiri kuthibitisha Uajiriwa wake.
Sasa unajiuliza hizo fedha zilizopo kama michango zilikuwa zikilipwa na nani?na imekuwaje wakizipokea kama hawajui huyu MTU ameajiriwa ama Laa?
So Mh Rais Mama yetu kipenzi tunakuomba utupie Jicho hii mifuko ya Jamii Urasimu ni Mwingi pasipo sababu zozote za msingi.
Ni hayo tu Wasalaam