Pre GE2025 Rais Mwinyi: Tuendelee kuiombea nchi Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Member
Sep 4, 2024
85
132
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema jamii ina Wàjibu wa Kujifunza Umuhimu wa Amani kupitia Mambo yanayojiri katika Nchi zilizokosa Amani Ulimwenguni.

IMG_3257.jpeg
Akizungumza katika Dua Maalum ya Kuiombea Nchi pamoja na Viongozi Wakuu, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliofanyika Chaani Tangini, Alhaj Dkt.Mwinyi amesema Amani ni jambo la kwanza kwa Taifa lolote linalohitaji Maendeleo na Maisha Bora ya Watu wake.

Amefahamisha kuwa Watu wanaohitaji Maendeleo na Kuwepo kwa Haki wanapaswa kufahamu kuwa Amani ya Nchi ndio jambo la kwanza linalohitaji kupewa kipaumbele.

IMG_3258.jpeg
Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameendelea kuwahimiza Wanasiasa, Waandishi wa Habari na Viongozi wa Dini kutumia nafasi zao kuhubiri Umuhimu wa Amani.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amewasisitiza Wananchi kuendelea Kuiombea Nchi Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba na kuwashukuru walioandaa Dua hiyo aliyoielezea kuwa ni zawadi kubwa kwa Mwanaadamu.

Baada ya Dua hiyo Rais Dkt. Mwinyi alisalisha Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Adhuhuri Kiwanjani hapo.
 
Back
Top Bottom