Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 120
- 132
RAIS MWINYI : FALSAFA ZA BABA WA TAIFA ZINATEKELEZWA KWA VITENDO.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa kaulimbiu ya Mbio za Mwenge mwaka huu imeonesha umuhimu kwa Taifa linalohitaji maendeleo, sambamba na kuwa na mazingira endelevu yatakayochangia maendeleo ya nchi.
Amefafanua kuwa ni jambo jema kuona miaka 25 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, falsafa zake zinaendelea kuishi na kutekelezwa kwa vitendo, huku akiwahimiza Watanzania kuziendeleza.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Rais Dk. Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia malengo ya viongozi waasisi wa Muungano, ambayo yanaendelea kuwaunganisha Watanzania.
Halikadhalika, Dk. Mwinyi amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha na kuunga mkono Muungano kwa mshikamano wa Watanzania.
Rais Dk. Mwinyi amewasisitiza wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Rais Dk. Mwinyi ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wananchi kwa maandalizi mazuri ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa Taifa, na Wiki ya Vijana kitaifa.
📅 14 Oktoba 2024
📍CCM Kirumba, Mwanza