Wanajamvi habari zenu.
Robert Mgabe (92) Rais wa Zimbabwe, ametangaza nia ya kugombea tena kiti cha urais nchini humo. Mkewe (50+) amenukuliwa akisema mumewe ataiongoza Zimbabwe hadi atapokufa.
Mke huyo ameongeza kuwa yupo tayari kumsukuma mumewe kwenye kitoroli kokote aendako ilimradi tu aendelee kuwa Rais.
Mke huyo akasisitiza pia kuwa hata Mugabe akiwa maiti, wananchi wanapaswa kumpigia kura ili wamwenzi.
Source: Redio DW idhaa ya Kiswahili leo saa 7 mchana.
Najua raia wa Zimbabwe wataamua kumchagua Rais anayewafaa. Lakini habari hii imeniachia maswali mengi. Yafuatayo ni baadhi tu.
- Kwa nini viongozi wanakuwa ving'ang'anizi namna hii?
- Kwa nini wananchi wampigie kura maiti wakati kuna watu hai tena wenye nguvu na maono ya uongozi?
- Ikitokea maiti akatangazwa mshindi ataongozaje?
- Nchi zingine hasa zile zinayoongozwa na akina Bi.Kirembwe zikiamua kuiga mawazo hayo sijui itakuwaje?
Ngoja tusibiri wakati ukifika mambo yatakuwaje.