Wakuu,
Rais mteule Donald Trump amepewa msamaha wa moja kwa moja katika kesi ya kughushi nyaraka za biashara kuficha malipo kwa Msanii Stormy Daniels, hatua inayomaanisha hatakabiliwa na kifungo, faini, au masharti yoyote baada ya hukumu iliyotolewa na Jaji Juan Merchan jana
Hapo awali Trump alikuwa ameshtakiwa kwa makosa 34 ya kughushi nyaraka, akidaiwa kuficha malipo ya dola 130,000 kwa Stormy Daniels ili kuficha madai ya uhusiano wao wa kimapenzi ambapo ikisemekana kuwa kesi hii ilihusiana na jitihada za kulinda kampeni yake ya uchaguzi wa mwaka 2016 ambapo yeye mwenyewe Trump akisisitiza kuwa malipo hayo yalikuwa kwa nia ya kulinda Familia yake.
Aidha Jaji Merchan alisema msamaha huu umelenga kuepusha kuathiri majukumu ya urais wa Trump huku akibainisha kuwa hukumu hiyo haiwezi kuondolewa kwenye rekodi yake ingawaje Trump amepanga kukata rufaa akisisitiza kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa.
========================================================
A judge has sentenced US President-elect Donald Trump to an "unconditional discharge," bringing to an end the first criminal trial of a former US president.
The sentence in the hush-money payment case means the incoming president has been spared any penalty, including jail time or a fine, but he will still take office as the first US president with a felony conviction.
"Never before has this court been presented with such a unique and remarkable set of circumstances," Justice Juan Merchan said shortly before announcing the sentence, calling it a "truly extraordinary case".
Appearing via video call from Florida and flanked by his attorney and two prominent American flags, Trump declared he was "totally innocent".
Source: BBC News