Rais Magufuli yuko tayari,amejipanga na kupangika

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Kesho,tarehe 2 Machi,2016 Rais John Pombe Joseph Magufuli,atahutubia wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC na wageni wengine waalikwa. Ni pale ukumbi wa AICC Arusha kutakapofanyika mkutano wa wakuu wa EAC.

Wanachama wa EAC ni Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi. Kama Mwenyekiti wa EAC,Rais Magufuli yuko tayari kuhutubu. Amejipanga na kupangika. Anatarajia kuitikisa Jumuiya kwa hotuba yake. Kwa lugha mwanana na yenye hoja na misimamo ya kitaifa na kikanda.

Ni kesho. Ni kutokea Arusha. Amejipanga...mwaka huu wataisoma!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ni nana hao wataisoma namba?hao wanachama wa huo umoja au wageni waalikwa kwenye huo mkutano?
 
Kwa kuhutubia watu waisome namba? Huu upuuzi wenu utaisha lini? Unless uwe na agenda ya "lugha" kwenye bango lako ili wale jamaa wachangie.
 
Safi sana tutakuwa standby kusubiria hotuba yake kwa hamu sana ili kujua msimamo wake kuhusu nkurunziza wa burundi, itarushwa live?, saa ngapi?, vituo gani vya radio na tv?
 
Wasalimie wachaga wenzago huko uchagani.
 
Lugha gani itatumika maana wengine sie kimombo hatuju,i asije akatumia lugha ambayo watanzania wengi hatuifahamu.
 
Ata hutubia kwa lugha gani? Mina najua lugha ya kujifunzia bongo siyo kibongo najiuliza sa itakuwaje sasa
 
Mwambieni mambo ya Hapakazituu sio ya EAC asije akatumia kwenye hotuba yake, hizo ni slogan za bongo tuu.
Sijui kwa nini, ila moyoni Nina hofu kubwa ninaposikia Rais wangu anataka kuzungumza na wenzake wa nje.
 
Hiyo lugha mwanana ndo lugha ipi iyo mkuu
 
Mwambieni mambo ya Hapakazituu sio ya EAC asije akatumia kwenye hotuba yake, hizo ni slogan za bongo tuu.
Sijui kwa nini, ila moyoni Nina hofu kubwa ninaposikia Rais wangu anataka kuzungumza na wenzake wa nje.
Maana wewe ni Ju.ha ndio maana
 

WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Published on Jun 11, 2013

Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
1. Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.

2. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.

3. Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.
 
Wakuisoma namba ni sisi na watz wenzetu. Huko EAC ataisoma namba nani tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…