Rais Magufuli: Utawala wangu sitaki kulimbikizia watu vyeo. Mbunge hawezi kuwa RC au DC

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kuwa katika utawala wake hatateua mbunge kuwa mkuu wa Mkoa au Wilaya. Amesema lengo ni kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji, kwamba "Haiwezekani katika watanzania mil. 50 tukose watu hadi turundie watu vyeo.

Tunataka tuchape kazi kwa ufanisi na ufanisi hauwezi kuja kwa kumrundikia mtu vyeo".

HAYO NDIO MANENO YA MAGUFULI RAIS WETU.
 
Ni kweli kabisa. Hii falsafa ihamishiwe mpaka kwenye chama. Haiwezekekani mtu anakuwa anakuwa mbunge halafu hapohapo yeye ni Mwenyekiti wa CCM )(W). Au mtu anakuwa Msemaji wa Chama halafu yeye ni Mbunge. Na hilo nalo tulione hadi kwenye ngazi ya Mwenyekiti wa CCM (Taifa), haiwezekani mtu awe yeye Rais halafu ahodhi uenyekiti wa Chama!
 
Bora wajue wafanye kazi walioipends ya kuwa wabunge, sasa watajali majimbo yao au watatemwa na wananchi.

Mfano mzuri wafate alichofanya Diwani yule wa Songea(jina nimesahau ni wa matala/ ka kama sijakosea) kuwatengenezea wananchi wake barabara ambayo hawakuwa nazo kwa miaka zaidi na zaidi ya 50 ndio now wanafurahia. Hongera kwake diwani
 
Sikufahamu kama kuna Mbunge alikuwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya..Naomba nipewe Mifano...
Engineer Stella Manyanya, yule alikua mkuu wa mkoa wa Mwanza kabla ya Ndikilo n. k
Najaribu kufikiria hivi; mfano rais aliyekua anawateua hao wabunge to RC/DC yupo anaangalia TV na kumsikia Magufuli anatamka hayo maneno hivi anajisikiaje? Piga picha yupo hapo kwa TV na mkewe wanatazama hilo tukio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…