Nianze na tafsiri ya wananchi, kwa ufupi hawa ni wakazi wazawa (native) wa nchi husika.
Katika nchi za demokrasia, Tanzania ikiwemo, utawala wa demokrasia ni utawala wa watu kwaajili ya watu wenyewe.
Rais anapewa mamlaka na nguvu na watu kuwaongoza watu waliompa nguvu iyo.
Rais John pombe ningine hajui hili au ni makusudi, Rais Magufuli ulibebwa na watu kuwa hapo ulipo na bado wao ndio upo juu chini miguu iliokusimamisha ni sisi wananchi wenzako
Baati mbaya umesau, unadhani upo mwenyewe katika nchi yenye kilomita za mraba 947,303 unashindana na waliokubeba, Rais unashindana na wananchi.
Rais John unakosea, ubabe si kuonekana wewe ni Imara, ubabe haukufanye uonekane mwanaume wa shoka kati ya wanaume na wanawake million 50 waishio Tanzania. Nakukumbusha tu leo Raisi wangu hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho .
Nikukumbushe watu kadhaa wababe duniani hujawai wala hutowafikia
Idi Amin. Shaka Zulu. Vlad the Impaler. Pol Pot. Adolf Hitler.
Lakini wote hawapo duniani, katika ulimwengu wa sayansi na tecnolojia na wasomi, ubabe si jambo sahihi. Wananchi wanapopaza sauti hawataki kitu flani sidhani kama ni busara kushindana nao
Raisi magufuli usishindane na wananchi