Rais Magufuli na Spika Ndugai watuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ndesamburo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”

Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.

Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

31 Mei, 2017
=============


 
Poleni kwa msiba wa mmoja wa wamiliki wa kikundi cha upatu na kupiga dili almaalufu Chadema .
 
Huyo mwandishi haeleweki mara kifo kimetokea leo sehemu ingine inasema jana.

RIP Mzee Ndesamburo
 
Ameni.huu ndio uzalendo tusiangalie tofauti za vyama,Spika uko vizuri Mungu wa mbinguni akulinda
 
Huu ni usaliti. Tulikubaliana hakuna kusapoti Wabunge wa Upinzani, kwa heri ama kwa shari...
 
Asante Mheshimiwa Spika huu ndo Utanzania tuliozoea siyo wa siasa za visasi hata kwenye matatizo.
 
Poleni kwa msiba wa mmoja wa wamiliki wa kikundi cha upatu na kupiga dili almaalufu Chadema .
Wewe akili zako unazijua mwenyewe, Rais wako/Mwenyekiti wako wa CCM anatoa wasifu mzuri kwa huyu mzee....


Jishangae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…