Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,075
- 3,353
Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Shikamoo!!!
Mh. Rais naandika ujumbe huu kwa masikitiko makubwa sana kwa baadhi ya watendaji wako kukiuka maelekezo yako kwa makusudi kabisa.
Mh. Rais sasa hivi dunia iko katika vita mbaya sana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 ugonjwa ambao umeua zaidi ya watu zaidi ya 350,000 duniani kote.
Sisi hapa Tanzania idadi kamili ya waathirika, waliofariki haijulikani kwani vipimo vilileta matatizo mwanzoni kabisa mwa safari, hadi sasa kuna tume iliyoundwa kuchunguza hayo bado haijatoa taarifa yoyote. Hivyo basi kutokana na kusitishwa kwa muda utoaji wa taarifa kuhusu corora mambo mengi ya ajabu yameanza kujitokeza kutoka kwa watendaji wa chini.
1. Kuhusu watoaji taarifa za Corona mara kadhaa, Rais ulielekeza kuwa taarifa zote za mwenendo wa Corona zitatolewa na Waziri Mkuu, Waziri wa Afya au Msemaji wa Serikali ukasisitiza kwa kusema " ...Na si vinginevyo"
Mh. Ugonjwa huu bado upo na wewe umekuwa ukituasa sana
Mh Rais, nasikitika sana kusema kauli ya Mh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwamba Jumapili wananchi wa mkoa wa Dar wa salaam wajimwage kusherekea Corona kuisha ni kauli mbaya sana na hatari kwani Corona ipo na haijulikani itaisha lini. Kitendo cha kuwaambia wakazi wa Dar kufanya sherehe tutegemee maambukizo makubwa ambayo kuyadhibiti itakuwa ngumu sana kwani tayari wameaminishwa gonjwa hakuna.
2. Kauli kuhusu Corona kutolewa na Mkuu wetu wa mkoa ni kosa kisheria kwani tayari ulisha toa maelekezo nani atoe taarifa hizo rasmi.
3. Mh. Rais inasikitisha sana kumsikia Mkuu wa Mkoa akiwahamasisha wananchi waende hata beach washangilie, wapige kelele kwa hakuna gonjwa Dar
4. Ningependa kukuomba Mh. Rais uwakemee kama huyu RC Makonda kwani anapotosha watu. Kwa kauli ya jana watu wengi wameacha kuvaa barakoa nadhani jata kunawa maji wataacha.
5. Mh. Rais mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, hatuna uhakika kama tutakuwa hai kwani siasa imetawala sana katika maisha ya watu. Wizara ya afya ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa taarifa imezingirwa kisiasa.
Kauli yako moja tu itatumia, wakemee hawa wachache wanaotupotosha.
Asante Baba.