Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,479
- 2,875
Barabara ya Moro-Dom au Dom-Moro kokote utakakoanzia ina umuhimu mkubwa kijamii, kibiashara na huenda hasara ya kuvunjika kwa daraja na kuchelesha kuikarabati ikipipwa kiuchumu na kibiashara in term of financial loss, ni kubwa sana.
Wakati ukarabati umeanza, ilimlazimu Waziri Mkuu kukatisha ziara yake Mkoani Tanga kufika darajani kujua kulikoni. Baadae tena Waziri Mkuu alitia timu ili kuona maendeleo ya ukarabati ukijumuisha na shughuli zingine.
Juzi usiku kuna taarifa ilitoka kutoka vyanzo visivyo rasmi ya daraja la muda kusombwa, wengine wakidai lilijaa maji na likawa halipitiki kwa muda na baadae likarejea kwenye kutoa huduma. Yote haya yanaendelea kuonesha umuhimu wa daraja la kuunganisha upande mmoja wa Dodoma na Morogoro ili kupitisha gari za abiria, gari za mizigo, baskeli, pikipiki hali kadhalika chochote kile kiwezacho kupita barabarani.
Kwenye mfumo wa kibiashara na uchumi kuna ujenzi wa madaraja ambayo hufanywa na familia, jamii au serikali ili kulipia gharama za huduma au bidhaa kwa lengo la kupata fidia/mrejesho kifedha huko mbele ya safari.
Mathalani,
Mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni moja ya financial leverage.
Kulipia gharama za watoto shule ya msingi mpaka kidato cha 4 ni financial leverage
Tafsiri rahisi sana ya Financial leverage ni "the use of borrowed money (debt) to finance the purchase of assets with the expectation that the income or capital gain from the new asset will exceed the cost of borrowing.
Je tukipima mrejesho kwa thamani ya fedha tunayowekeza kwa vijana wanaotoka la kwanza mpaka la 7 (hawa ni wengi) na wale wanaofika kidato cha 4; tunaweza kujua mrejesho ukoje na faida ipo?? (tunao wajibu kupima kwa namba na kwa mambo ambayo namba hazisomi).
Mrejesho huu hali kadhalika unahusika kwenye mikopo ya vijana wa vyuo vikuu. Kama hakuna mfumo rasimu wa kuwa-absorb wahitimu kwa lengo la kutumia akili zao na nishati yao; je kuna njia mbadala inafikiriwa ya namna ya kuzipata fedha hizi?
Kama hatujui, basi iko haja kutafuta kati yetu watu wenye fikra mbadala za nini kifanyike ili nishati ya vijana (muscular) na nishati ya akili iko haja ikajengewa mfumo rasmi ili itumike kwa lengo ya kuzalisha na kurejesha fedha zilizotumika kugharamia elimu. Hapa tunapata faida zaidi ya mara mbili...the expectation that the income or capital gain from the new asset will exceed the cost of borrowing...
Naomba nirejee mifano miwili ambayo nimewahi kutoa mara kwa mara hapa hapa jukwaani ambayo hata JPM amewahi kuisemea. Kwanini tulime korosho, pamba, kahawa, katani, kokoa, chai...halafu kazi ya kizichakata bidhaa ghafi viwandani badala ya kufanyia kazi humu ndani ifanyike katika mifumo rasmi kwa nguvu na akili za Watanzania, mara zote tunatoa ajira kwa Wachina, India, Vietnam, Indonesia. Nadhani hili sio sawa.
Tunahutaji kununua technology, know-how (expertise kutoka nje in form of training) ili kazi hizi tufanye wenyewe. Katika hili serikali inaweza kujenga financial leverage ambapo wanatafutwa watu wenye akili za kuja na investment project ambazo zikifanyika locally, ndani ya miaka 5-10 zinaweza kupunguza imports na kuongeza exports.
Wakati haya yakifanyika, kazi zinapatikana kwenye mifumo rasmi, mifuko ya jamii inakua kwa kupata wanachama wengi zaidi, tax base ya TRA inakuwa kwa viwanda kulipa kodi ya VAT kwenye manunuzi ya vifaa na huduma, viwanda kulipa corporate tax siku faida ikianza kuzalishwa, wafanyakazi kukawa PAYE likewise ongezeko la Indirect taxes ambazo TRA inapata kwa watu kutumia fedha kununua bidhaa na huduma mbalimbali.
Tukumbuke, mauzo ya umeme (TANESCO), mauzo ya Maji (DAWASCO, MWAUWASA popote pale mamlaka ilipo makusanyo ya mauzo ya maji yataongezeka, ikiwemo Tabora ambao kwa sasa wana uhakika wa maji ya ziwa Victoria)
Huduma zingine za kitaalamu na ubora zitaongeza makusanyo ya fedha kwa taasisi kama vile TBS, TMDA (kwa viwanda vya vifaa tiba na madawa ya binadamu), GS1, OSHA, NEMC the list goes on...
Wizara ya Uwekezaji OWM, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na biashara, wazara ya kazi, wizara ya Elimu iko haja kuwa na mkakati wa muda mfupi, muda wa kati unaotekelezeka ili mambo haya yatokee.
Vinginevyo kuna wakati tunakuwa na mfano wa wahandisi wa Tanroad 12 walisimamishwa, mpaka mambo yanaharibika na kuzidi kuharibika wao wako ofisini.
Katika hili, narejea, hatuhitaji kutegemea akili za walio serikalini pekee, kuna wengine washaridhika na paycheck za mwisho wa mwezi na wanasubiri retirement benefits, kuna haja ya kusaka watu wenye akili kama Farao alivyofanya wakati anatafuta suluhisho ya ndoto yake ya masuke 7 manono kuliwa na masuke 7 yaliyokonda.
Ndoto ya JPM kujenga uchumi wa kati kwa kutumia viwanda inawezekana, imebaki miaka 6 akabidhi kijiti kwa Rais ajae Nov 2025. Mpaka sasa kuna vichwa anavyo ambavyo usiku na mchana vinakesho ku-develop solutions?
Yusuf alimwambia Farao, miaka 7 hii ya chakula tele, ni wakati wa kuchukua 20% ya kila mavuno ya mwaka na kuhifadhi kwa ajili ya Misri na nchi za jirani. Miaka 10 ya JPM siku anatoka tukipima, hao "akina Yusuf" watakuwa wamefanya nini kwa ajili ya Tz na mataifa ya jirani.
Mimi ninaendika haya, walau namfahamu mtu mmoja ambae anaweza kutengeneza kazi walau 300-500. Na model yake ya investment na technology imekuwa proven kufanyika dunia nyingine. Najaribu kuwaza tu, ni namna gani walau akaaminiwa kwa kutengeneza ajira 100 kama pilot ili mafanikio ya 100 jobs yawape kumwamini kwa kazi zingine 200-400.
Hapa kuna watu kuingia kwenye mifuko ya pensheni, makazi bora, mfumo rasmi ya bima ya afya, mikopo ya wafanyakazi kwenye taasisi za fedha na faida zingine lukuki.
Kwa mtazamo wangu, kuchelewesha kutumia akili za vijana wa Tanzania kwa kujenga financial leverage, bila shaka ni sawa na uhujumu uchumi.
Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote