Rais Magufuli hivi wewe ni jemedali wa aina gani? Ndugu zetu wanavyo pukutika Dar huwaoni?

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
2,467
1,697
Awali ya yote napenda kutoa pole zangu kubwa na rambi rambi kwa ndugu na familia wote nchini waliopata kuondokewa na wapendwa wao na mungu wa mbinguni aziweke roho za wapendwa hao peponi na miili yao mahali patakatifu duniani. Amen!

Zaidi ya hayo napenda pia kutoa shukran zangu nyingi na za dhati kwa waganga na wakunga wote nchini kwa kazi wanazo zifanya na kwa kujitoa kwao muhanga kuwasaidia ndugu zetu katika kukabiliana na janga hili la Covid-19 peke yao wakati serikali yetu na mtu anayesifika kama jemedali wetu kujichimbia kwenye pango lake huko Chato.

Hongereni sana askari wetu na wapiganaji wetu hodari wa hii vita dhidi ya Coronavirus. Mungu awabariki na kuwapa nguvu ya kuendelea kuokoa maisha ya ndugu zetu. Nyie ndiyo mashujaa wetu!

Rais Magufuli kama wewe ni jemedali wa kweli wa watanzania, kwanini sasa hatukuoni ukiwa mstari wa mbele katika kushirikiana na wananchi wako katika mapambano dhidi ya ya hili janga la Coronavirusi ambalo wewe mwenyewe umeliacha liendelee kusambaa mpaka hapa lilipo?

Kama jemedali wetu kweli, ina maana wewe vifo vyote hivyo vinavyotokea nchini huvioni wala kuvisikia? Au ndiyo tuseme kuwa wewe ahusikii na hivyo vifo? Kuna kitu gani kina kuzuia kuchukua sasa hatua ya ku "lock down" Dar es salaam na miji mingine mikubwa ambayo imeathirika kwa hali ya kuogopesha?

Wanadiaspora wengi kama akina Mange Kimambi na wengineo walipokuwa wakitoa ushauri wao juu ya kufunga mipaka na kuwazuia wachina wasiingie nchini kwa wingi, hawakuwa wajinga kama ulivyokuwa unafikiri kufanya hivyo, walijua fika nini kitatokea kama ndugu zao Tanzania hawata chukua tahadhari mapema za kuzuia kusambaa kwa huu ugojwa. Sioni sababu ya kuwalaumu wao wakati ukweli wa mambo unaanza kuonekana nwenye jamii yetu Tanzania.

Rais Magufuli watanzania wengi bado wana kumbukumbu nzuri za actions zako ulizo zifanya mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuru yaMuungano wa Tanzania. Tuna kumbuka kama Jemedari wetu mashuhuri, shupavu na mwenye msimamo, ulikwenda Muhimbili hospitala na kuwatendea mambo mazuri wagonjwa walio lazwa kwenye hospitali yetu maarufu hiyo kwa kutoa amri ya kubadilisha hali ya hospitali hiyo ili wagonjwa waweze kupata matibabu katika hali iliyo kuwa nzuri. Swali langu kwako; je, ujasiri ule ulio uonyesha Muhimbili uko wapi leo katika mampambano ya kukabiliana na hili janga la Coronavirus?

Karibu siku sita sasa toka utoe kauli yako hii kwenye press conference yako Chato hatuja sikia kauli nyingine yeyote ile kutoka kwa viongozi wahusika kutoka kwenye kiongozi anahusika na janga hili. Viongozi ulio wapa mamlaka kama Waziri Mkuu, waziri wa Afya na makatibu wao hatuwaoni wala kusikia chochote kutoka kwao pamoja na turbulence kubwa ambayo imejitokeza ya watu kusambaza clips na audios za tofauti na za kutisha mitandaoni.

Kitendo hiki cha ukimya wenu na matukio ya vifo vingi vinavyo tokea na mazishi ya hata usiku nchini, kinawatia wasi wasi mkubwa sana watanzania wengi ambao wana shindwa kuelewa kwa nini jemedari wao ambaye amewapa matumaini makubwa ya maisha yao, anatoweka kwenye ukumbi wa mapambanonhaya na kuwaacha peke yao bila mwongozo.

Rais Magufuli naomba uweke kwenye kumbukumbu yako kuwa hili janga ni wewe mwenyewe ndiye uliye sababisha likawa hivi na sio mtu mwingine. Na wewe ndiye utakaye laumiwa mwishoni na sio Waziri mkuu wala waziri wa Afya. Wao wametekeleza tu maagizo uliyo kuwa umeyatoa kwao.

Nimeshangaa sana na kusitushwa kuona njia ambazo wewe umezichukua katika kukabiliana na usambazaji wa huu ugonjwa.

Mwanasayansi mkubwa na mashuhuri ambaye inasadikika kuwa ana PHD ya Chemistry na ambaye amefanya mambo mengi katika maisha yake, anashindwa katika ku coordinate njia na measures ambazo zingesaidia kuzuia kusambaa kwa huu ugonjwa nchini. Sasa Rais Magufuli kama wewe, mtu ambaye watanzania wanakutegemea na kukupa imani kubwa kama mkombozi wao katika matatizo yao nchini unashindwa hata kuwapa maneno mazuri ya upendo ili kuwaondoa wasiwasi wao, unategemwa nani mwingine watanzania watakuwa ma imani naye?

Watanzania wengi wanashangazwa na msimamo wako na uamuzi uliouchukua wa kujitoa mwenyewe kutoka kwenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa mipango na maazimio yatakayo saidia kupunguza kuenea kwa Covid-19, kwani kwenye mambo mengine mengi huko nyuma ulikuwa mstari wa mbele wewe mwenyewe kwenda Sites za miradi mbali mbali kama ya majengo na barabara na shughuli nyingine za maendeleo kama bandari, Bank kuu, Airports na kadhalika, lakini kwenye swala hili la Coronavirus ambalo binadam ulimwengu mzima tunakabiliana nalo, wewe unashindwa kwenda kufanya ukaguzi wa mitambo iliyowekwa ili kuona na kujiridhisha mwenyewe kama inafanya kazi kwa umahiri unaotakiwa, badala yake unaingiza mitini na kujitokeza pale unaona sasa watanzania wanahitaji kuomba.

Nashangaa pia unawaamasisha watanzania kwenda kukesha kwenye mahekalu kwa siku tatu mfululizo kumwomba mungu ambaye asili yake ni mungu tuliye aminishwa na watu ambao wewe unawaita mabeberu. Hao watu walio tuletea hiyo dini na huyo mungu wao ambaye wewe na baadhi ya watanzania wengi hivi sasa ndiye nguzo na tumaini lako kubwa kwenye hili janga, wao wenyewe limeqakuba ile vibaya. Kuna mahekalu na misikiti mikubwa kama Rom na Meka? Kama Pop na Mashehe maarufu ulimwenguni wameslim amri na kulazimika kufuata maagizo ya wataalam wa kisaynsi, wewe utakuwa nani Rais Magufuli katika ulimwengu wetu huu mpaka Mungu wa mabeberu akusikilize wewe kuliko hao mabeberu ambao yamemfanya watu wengi duniani tumwamini?

Mimi kwenye maisha yangu sijawahi ona na kushuhudia vifo vingi vya binadam wenzangu kama nilivyo shuhudia kwa wazungu huku Ulaya. Wazungu pamoja na kujiamini kwao, mbele ya huu ugonjwa ilibidi kuufyata. Kiburi chao chote kiliwaisha.

Mimi nilitegemea kwenye hili janga wewe Rais kuwa bega kwa bega na makam wa Rais, waziri mkuu, waziri wa Afya na wataalam wa magonjwa ya virus na watendaji wengine katika kuhakikisha kuwa maamuzi na utaratibu wote mlio uweka wa njia za kupambana na huu ugonjwa mnayafuatilia kwa karibu. Kwa mfano; madai ya kwenye audios mitandaoni juu ya kutoroka kwa watu walio sadikika kuwa wamewekwa karantin kwenye hospitali ya Amana Ilala, sijaona hata mtu mmoja mmoja alikwenda kwenye sehemu ya tukio zaidi ya audios za online Radios za watangazaji na mkuu wa wilaya ya Ilala. Sasa hii tutaihitaje Rais wetu?

Rais Magufuli nina uhakika kuwa wewe na watendaji wa serikali yako mlikuwa na mda mrefu sana wa kujiandaa na huu ugonjwa, kwani kama Rais na amiri jeshi mkuu utakuwa umezungukwa na wataalam mbalimbali ambao wamebobea katika maswala haya ya pendamic. Nashindwa kuelewa pamoja na kuwa na mda wa kujiandaa mmeshindwa kwa kiasi fulani kuzuia kusambaa kwa haraka kwa hivi virusi.

Ushauri wangu kwako Rais Magufuli nakuomba usikilize ushauri wa wataalam wako na watanzania wengi wa nje ku Lock Down Dar es salaam na kama itashindikana kabisa kabisa basi zuia njia zote zinazo kwenda mikoani kwa kuweka maabara ya kufanya Tests kwa watu wote wanao ingia au kutoka.

Ushauri wangu mwingine ni kuangalia jinsi gani masoko yetu yatatoa huduma sehemu ambazo zilo wazi ili watu wasikusanyike pamoja. Bars na makanisa yafungwe. Watu wanaweza nunua Alkohol na kunywa sehemu za wazi nje au kunywa nyumbani na kutumia Screens zao kuabudu. Mungu sio lazima aabudiwe makanisani, anaweza akaabudiwa popote pale.

Zaidi ya hayo ni ombi tu, ombi la kutaka urudi Magogoni ukapaange mambo yako kwa uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ticha(teacher) huku nilipo (kijijini ndani).amerudisha namba akiwa nyumbani kwake. Ilianza kama mafua,tumbo kuuma,then kifua kubana(alikuwa na pumu+presha). Mwili umekataliwa hosp,taarifa imetolewa...... fasta.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom