Tatizo kila mtu sa hivi yuko bize na madawati na kadili wanavotumia muda mwingi ku deal na madawati watajikuta upungufu unaendelea maana hadi yataanza kuharibika, leo hii unaweza kujitolea kujenga shule/kukarabati shule ya seikali kwa zaidi ya milioni 200 ukamuomba mkuu wa mkoa aje aifungue, halafu kukakawa na sehemu nyingine mkuu wa mkoa ameitwa kupokea madawati 20 siku hiyohiyo, unakuta mkuu wa mkoa anahairisha ufunguzi wa shule anaenda kupokea madawati ili aonekane kwenye tv kumfurahisha mkuu.
Viongozi wetu wanatakiwa kuwa wabunifu na kukubali kushirikiana na wananchi kutatua kero zao, kero sio madawati pekee