Rais Magufuli ateua Wakurugenzi Wakuu wa NSSF, TBC na Shirika hodhi la reli (RAHCO)

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
9,338
13,294
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.

TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).

Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Machi, 2016.
 
Dr JPM amemteua DR Ayub Riyoba Kuwa mkurugenzi wa TBC mbali na uteuzi hupo pia amemteua mkurugezi wa NSSF pia.Prof Godius Kahirara pia kamteua Dkt Mussa Iddi Ngwatu Kuwa mkurugezi RAHCO
 
CV ya mrithi wa Dau
 

Attachments

  • 1458383032124.jpg
    1458383032124.jpg
    86.9 KB · Views: 137
Back
Top Bottom