Rais Magufuli akatembelea kijiji cha Hiware Bazar kilichoko India

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,002
Kijiji cha Hiware Bazar ni kijiji kilichoko wilaya ya Ahmednagar Jimbo la Maharashtra, India. Kijiji hicho kilikuwa na ukame wa kupindukia ambacho watu wengi waliamua kukihama na kukitelekeza.

Kwenye hicho kijiji anapatikana mwenyekiti bora wa kijiji anayesifiwa sana duniani aitwaye Popatrao Bajugi Pawar.Huyu ni msomi mwenye digrii mbili ambaye alipomaliza digrii zake akiwa msomi pekee kijijini aliamua kurudi kukibadilisha kijiji chake mara baada ya kumaliza masomo.

Aliporudi kijijini 1990 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Hiware Bazar kwa kura zote.

Mwenyekiti huyo aliposhika madaraka ya uenyekiti wa kijiji aliamua kuitumia elimu yake kukibadilisha hicho kijiji kwa kuanzisha mradi wa kudaka maji na kuyahifadhi kutoka milimani mvua zinaponyesha na kuyatumia kwa kilimo.Kijiji hicho kimebadilika na kuwa kijiji bora chenye ardhi nzuri na kilimo kizuri na kinapigiwa sifa si India tu bali na watu mbali mbali duniani kama kijiji bora kilichofanya mapinduzi makubwa toka kijiji cha kilofa hadi kuwa kijiji cha watu walioendelea kwa kipindi kifupi.

Mheshimiwa Raisi kwa kuwa anapenda maendeleo ya haraka kama anavyosema kuwa tumechelwewa kuendelea nashauri atembelee India lakini safari yake ilenge kutembelea hicho kijiji.Mfumo unaotumika kwenye hicho kijiji waweza tumika na vijiji vingi hapa nchini na kuleta maendeleo ya haraka sana vijijini.

Angalia video ya hicho kijiji

 
Wasomi wetu hawataki kusikia mambo ya vijijini.Wanataka wakae mjini waendeshe magari.Wahitimu wa SUA ndo hasa wanatakiwa vijijini lakini hakuna mkakati wa kuwafanya wavutiwe kwenda huko.
 
This is the lifestyle i always dream and fight for. Tatizo wanasiasa wetu ni watu wa hbovyo sana, wanawaza kula bata tuu, hakuna anayejiumiza na umaskini wa watu wake, tumebarikiwa rasilimali za kila aina but poor Tanzania.
 
.Wahitimu wa SUA ndo hasa wanatakiwa vijijini lakini hakuna mkakati wa kuwafanya wavutiwe kwenda huko.

Huyo mwenyekiyti wa kijiji wa India hana digrii ya kilimo ana digrii ya Masters of commerce Kasomea biashara.Na kijijini hakupelekwa na serikali alijipeleka mwenyewe na uzalendo wake na kijiji hakikuwa na mazingira ya kuvutia yalikuwa mabaya si kwa msomi tu bali na kwa wale ambao hawajasoma lakini aliamua kuyabadilisha.

Huu wimbo wa kusema serikali itengeneze mazingira haustahili kuimbwa!!! Kazi ya msomi ni kubadilisha mazingira yakiwa mabaya yawe mazuri.Huko kwenye mazingira mabaya ndiko wasomi wapya wanatakiwa waende sio waende kuzuri ambako wasomi wa zamani walishakubadilisha.

Wasomi wetu wengi wapya wanataka kuishi kwenye mazingira ambayo wenzao waliowatangulia waliyafanyia kazi kuyaboresha.Ndio maana watu wanadharau wasomi sababu wanaona wasomi wanaongezeka lakini maeneo yaliyo nyuma miaka nenda rudi yanabaki vile vile pamoja na kuwa maeneo hayo yametoa wasomi kibao lakini hawarudi na digrii zao kwenda kuyaboresha kama huyo wa India.
 
This is the lifestyle i always dream and fight for. Tatizo wanasiasa wetu ni watu wa hbovyo sana, wanawaza kula bata tuu

Huyo mwenyekiti wa kijiji hakuwa mwanasiasa na wala hakutegemea wanasiasa alipofanya maamuzi yake na hakuwa na mtu wa kupigana naye au kushindana naye kisiasa au kisomi.Yeye binafsi alichukua maamuzi ya kuwa AGENT OF CHANGE kijijini kwake.

Kusukumia kila lawama kwa wanasiasa nadhani wasomi wanakuwa hawatendi haki.Wasomi wafike mahali waonyeshe usomi wao umesaidiaje kubadilisha maisha walau hata kwa kiwango cha kijijini kwao walikozaliwa.Wasomi wengi hawana kitu cha kuonyesha kama huyo mwenyekiti wa kijiji wa India.

Niseme wazi wasomi wengi wa Tanzania hawana tofauti na wanasiasa kwa sababu wote maneno mengi hawana kitu cha kuonyesha kuwa angalia mimi msomi nimekibadilisha kijiji kile kuondokana na umaskini.
 
Kamwambie yule mume wenu aliyewaweka pale masaki akatembelee huko india Rais hana nafasi yupo busy kuzuia michezo ya pool table
 
Achats TE="Precise Pangolin, post: 15596073, member: 72456"]Kamwambie yule mume wenu aliyewaweka pale masaki akatembelee huko india Rais hana nafasi yupo busy kuzuia michezo ya pool table[/QUOTE]
Acha kujipendekeza utaolewa wewe
 
ni kweli iran inatumia maji iliyovcuna kwenye mvua kwa kilimo cha umwagiliaji sisi mpaka sasa kwa kiasi kikubwa kilimo chetu kinategemea mvua hata ile miradi kama ya dakawa tuliyoanzishiwa mara walipotukabidhi tukashindwa kuiendesha wasomi wetu waache kulalamika watumie elimu yao kuonyesha nini walichokisoma sio kudai hakuna ajira
 
Kasema hawezi kumpa chakula mtoto wa jirani (upinzani)he kama wanahitaji hayo maendeleo ni jimbo la upinzani kwa kauli yake hatatoa hiyo fursa.my take
 
Walichofanikiwa Zaidi ni kubadilisha mindset na attitude, sasa wenzenu wanang'ang'ania waruhusiwe kuwa madada poa na kucheza pool saa tatu. Huku asiende JPM twendeni sisi ili tulete tofauti, Enzi hizo scholarship za kwenda India nafasi tano mnaenda watu wawili wengine wanakula kona wanataka Japan, Australia, Ulaya na Marekani.

Kusubiri serikali itatufanyia haipo na hiyo crip imetaja serikali mwishoni mwanzo ni wananchi wenyewe ndio wamechukua hatua na muda umekuwa rasilimali muhimu manake 20 yrs wamatumbi kusubiri maendeleo wanaona shida wao wanataka ahadi hata ikichukua miaka 100 hawana nouma.
 
Enzi hizo scholarship za kwenda India nafasi tano mnaenda watu wawili wengine wanakula kona wanataka Japan, Australia, Ulaya na Marekani.

Mkuu hilo ni tatizo. Watu kutaka kwenda safari wanazorudi na albamu zilizojaa picha za mabibi na mabwana wa kizungu badala ya kurudi na vitu vinavyoweza saidia nchi.Safari za kwenda kwenye maeneo kama ya India kama hicho kijiji mtu unarudi na vitu kichwani unavyoweza fanyia kazi na kubadilisha jamii.

Ni vizuri kwa yeyote aliyepania kuleta mabadiliko vijijini kutembelea kule si Raisi pekee.Ningekuwa na uwezo ningewapeleka wasomi kibao kule halafu wakirudi nawaambia nendeni vijijini mkayafanyie kazi mliyoyaona india kwenye hicho kijiji, nisiwaone mjini tena mnacheza pool asubuhi kwa kusingizia hamna kazi.
 
sasa kama wewe umeweza kutueleza yaliyofanyika mpaka hicho kijiji kikafanikiwa kuna haja gani ya Makufuli kwenda huko? kwa jinsi Makufuli alivyo maelezo yako yanatosha kishajifunza tayari
 
sasa kama wewe umeweza kutueleza yaliyofanyika mpaka hicho kijiji kikafanikiwa kuna haja gani ya Makufuli kwenda huko? kwa jinsi Makufuli alivyo maelezo yako yanatosha kishajifunza tayari

Hivi wewe katika sehemu zote ulizosoma uliwahi kwenda FIELD? Unaelewa maana ya kwenda field pamoja na notisi kibao ulizoandika na kusoma darasani?

Kama wewe umeelewa ngoja nikuulize bwawa moja la kudaka maji huwa linakuwa na upana na urefu na kina cha mita ngapi?
 
wakati wanajitolea kubadilisha hivyo vijiji watakuwa wanakula nini? yaani uache watu wanakula maisha kirahisirahisi mjini uende kijijini mikono mitupu kubadilisha maisha?!!! no, thank you.
 
wakati wanajitolea kubadilisha hivyo vijiji watakuwa wanakula nini? yaani uache watu wanakula maisha kirahisirahisi mjini uende kijijini mikono mitupu kubadilisha maisha?!!! no, thank you.

Ukiwa na mawazo kama haya utakuja kufa lofa.Waliofanikiwa walikabiliana na changamoto ziwe mjini au kijijini
 

Ukame wa Tanzania ni wa kujitakia.sababu kila sehemu hunyesha mvua.Tatizo tunayaacha hayo maji ya mvua yasafiri kuzurura tu bila kuyadaka kuyavuna na kuyahifadhi.Tungelima kipindi cha mvua tukapata mazao na tukawa na msimu mwingine wa kilimo cha umwagiliaji unaotumia maji tuliyovuna.Ni kosa kubwa kuacha kipindi cha mvua hadi kipite bila kuvuna maji.Unatakiwa uhamasishaji kuwa kila kijiji kiwe na eneo la kukusanya maji na kuyavuna kipindi cha mvua.Hiyo itawezesha vijiji vyetu kuwa na misimu miwili ya kilimo ambapo kutakuwa kilimo cha kutegemea mvua,zikikatika wanaingia kilimo cha umwagiliaji.
 
hizo fursa walikua wanazipata watu wa wizarani miaka ya nyuma walifanikiwa kuzurura karibu kila mahali umeona kuna mabadiliko yeyote zaidi ya kupata posho za safari sisi kama vijana tunapenda kufanya vitu vizuri ila kuna baadhi ya nyenzo lazima uwe nazo siyo tu kukurupuka kwenda kuanzisha harakati.
 
Kama GHADAFI NA LIBYA WALAHI. ..
 

hahahahahahha...maendeleo gani anayapenda?

Hhahahahahahahaha...ya kununua bombadier ?

Ya kula hela za rambirambi na kujenga airport kubwa Chato?

Muogopeni Mungu jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…