Rais Kikwete amemteua Mtendaji Mpya wa Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
864
427
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua, Kissiok Ole Mbille Lukumay, kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.

Aidha, Rais Kikwete amemteua, Onesmo Hamis Makombe, kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu.

Taarifa iliyotolewa usiku wa jana, Alhamisi, Jijini Dar es Salaan na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa maofisa hao wawili ulianza Ijumaa ya Machi 27, mwaka huu.

Kabla ya uteuzi wake, Lukumay ambaye ana diploma in Materials Management na ni Certified Supplies Professional na pia ana MBA (Procurement and Logistics) alikuwa Ofisa Ugavi Mkuu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.

Naye Makombe kabla ya uteuzi wake alikuwa Kaimu Kamishna, Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu. Kielimu. Makombe ana shahada za B.Com, CPA na MBA (Finance and Human Resources Management).
 
Back
Top Bottom