Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,515
- 4,017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, jana tarehe 27 Oktoba 2024, amezindua soko jipya la Jumbi katika wilaya ya Magharibi B, mkoa wa Mjini Magharibi. Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Suzan Kunambi (MNEC).
Uzinduzi huu ni sehemu ya mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ukidhihirisha jitihada za serikali katika kuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi kwa kujenga miundombinu ya kisasa kama masoko ili kuinua ustawi wa wananchi.
Soma, Pia: Dkt. Mwinyi aondoa kodi ya sukari Zanzibar