MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
" Marehemu alipofikia muda wake wa Kustaafu nilimuomba aendelee kwani sikuona wa Kumrithi. Na mpaka hivi leo ametutoka duniani ama hakika atanipa Kazi ya ziada kumpata Mbadala wake ", alisema Rais Dkt. Magufuli.
Tusidanganyane hapa duniani hakuna Mtu ambaye hawezi kuwa bora kwa Mwenzie hata kama ikitokea amefariki au amestaafu au amefukuzwa Kazi.
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli sasa kwa Kauli yako kama hii ikitokea utakayemteua akiwa bora kuliko Marehemu utatuambia nini tena? Je, utaenda Kufukua Kaburi la Marehemu na kumchapa Vibao kwa kumwambia kuwa kumbe alikuwa hana lolote na alikuwa anakuchelewesha tu?
Mbona hata Wewe ( Mheshimiwa Rais. Dkt. Magufuli ) muda wako wa Kustaafu ukifika au ukiwahi Kuungana na Israeli kwenda Mbinguni ( namaanisha Kufa ) bado nina uhakika Tanzania tutapata Rais mzuri tu kuliko Wewe na huenda pia akatufanya hata tukusahau tu upesi?
Umeshauriwa sana uwe unazipima Kauli zako uwapo katika Hadhira lakini kwa bahati mbaya mno umekuwa Sikio la Kufa ( siyo Msikivu ) na hushahuriki pia Kiasi kwamba unatupa Maswali mengi zaidi juu yako.
Najua utaninunia ila badilika sasa JPM.