Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kupitia Ukurasa wake wa twitter amethibitisha kuwa vuguvugu la maandamano ya siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano lingali bado lipo kwenye ratiba ya Muungano wa Azimio.
Maneno yake yanakuja dakika chache tu baada ya Mahakama kudinda kuweka zuio la maandamano, ikisema ni haki ya msingi ya kila mwananchi.
Awali Odinga alikutana na Wabunge wa Muungano wa Azimio kwenye ofisi za wakfu wa Jaramogo Oginga Odinga kujadili maandamano ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.
Kwa upande mwengine Waziri wa usalama wa ndani Professor Kithure Kindiki ametoa onyo kali kwa Viongozi wa Upinzani akiwataka kuacha kuichokoza Serikali.