Raila Odinga amwangukia Lowassa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253

Mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya umoja wa vyama vya upinzani wa NASA, Raila Odinga ameweka wazi ombi lake kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa kuhusu mchakato wa uchaguzi huo.

Amesema kuwa Lowassa pamoja na Rais John Magufuli waliochuana kwenye uchaguzi mkuu uliopita ni marafiki zake, na kuwaomba wote wamuunge mkono kwenye uchaguzi huo.

Ombi la mwanasiasa huyo mkongwe wa Kenya na Waziri wa zamani wa nchi hiyo limekuja siku chache baada ya Lowassa kuweka wazi kuwa atamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta ili aendelee kuitawala nchi hiyo.


“Mimi na familia yangu tunamtumikia Mungu lakini vilevile kwa dhati kabisa sisi wana Monduli tunamuunga mkono Uhuru Kenyatta kwenye mbio za Urais nchini Kenya. Naomba nitamke wazi na dunia yote ijue kuwa sisi tunampenda Uhuru Kenyatta naye anatupenda, kwa hiyo tunamuunga mkono kwa kuwa tunaamini ana uwezo wa kuwaunganisha Wakenya na Watanzania,” alisema Lowassa alipotembelewa na wabunge wanawake kutoka Kenya, nyumbani kwake Monduli takribani mwezi mmoja uliopita.

Lowassa ana ushawishi kwa kiasi fulani kwenye uchaguzi huo kwa kuwa ni kiongozi mkuu wa Wamasai (Leigwanan) katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo pia kimeweka wazi kuwa kitamuunga mkono Kenyatta kwa kuwa kinaridhika na namna alivyofanya kazi hususan kuruhusu demokrasia nchini kwake.

Hata hivyo, msemaji wa vyama vya upinzani nchini Kenya, Philip Etale alisema kuwa Odinga ni rafiki wa Lowassa na Magufuli na kwamba asingependa urafiki huo upotee kwa sababu za kisiasa.

“Odinga aliweka bayana wakati wa kampenzi za uchaguzi wa Tanzania kuwa anawaunga mkono wote na kutaka mgombea bora ashinde. Kama ODM tunaamini katika demokrasia na tusingependa wakati wowote ule, tupoteze marafiki zetu kwa sababu ya siasa,” huo ulikuwa ni ujumbe wa Etale

Kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi ambao unatajwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kwani katika uchaguzi uliopita, Kenyatta na Odinga walizidiana kwa kiasi kidogo cha kura.


Chanzo: Mpekuzi
 
Lowassa ni chaguo la Mungu, kwenye sauti ya Lowassa ndipo Mungu hunena na watu wake, its matter of just time, mtakuja kuona, yote hutokea kwa makusudi ya Mungu
 
Ukawa please grow up hata Mkimsapoti yeyote unafikiri Rais Kenyatta akishinda 2020 Jubilee watatoa upuuzi wa Kuwa sapoti Nyinyi?
Mkuu tumeamua kuchagua demokrasia dhidi ya udikteta!!! Kwa kuwa ameamua kukumbatia udiketa basi tumeamua kwenda upande wa demokrasia
 
Odinga hawezi kupenya aise bora akatulie alee wajukuu wake......kenyatta kafanya mengi yanayoonekana kwa macho na yanayofaidisha wananchi direct.
 
Kwa vile Odinga aliamua kushirikiana na shetwaaani basi atoswe , eti niliwaunga mkono wote , How comes ?

Poor Odinga !
 
Wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Kenya zikipamba moto, mgombea urais kupitia Muungano wa Vyama vya Upinzani (Nasa), Raila Odinga amesema Rais John Magufuli na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ni marafiki zake na hataki kumpoteza yeyote kati yao.



Odinga pia amesema anataka wawili hao kumuunga mkono katika harakati zake za kuwania urais.

Kauli ya mwanasiasa huyo mkongwe imekuja baada ya Lowassa kueleza wazi kuwa anamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika kampeni zake za kubakia Ikulu ya Kenya.

Lowassa, ambaye mwaka 2015 aligombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa ameamua kumuunga mkono Kenyatta kwa sababu kwa kipindi alichokaa madarakani ameonyesha uwezo na amefanya kazi nzuri.

Baadaye Chadema ilitoa msimamo kuwa imeamua kumuunga mkono Kenyatta kwa kuwa Odinga anamuunga mkono Magufuli, ambaye ni rafiki yake.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema chama hicho kimefanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa mtu pekee anayepaswa kuungwa mkono ni Kenyata kwani ndiye chaguo sahihi kwa wapenda demokrasia.

Alisema kuwa tangu zamani rafiki yao alikuwa ni Odinga na walimuunga mkono kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2012 lakini wakashangaa ilipofika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, mwaka 2015 Odinga akamuunga mkono Magufuli, aliyegombea urais kwa tiketi ya CCM.

Alimwagia sifa Uhuru Kenyata kuwa katika kipindi cha uongozi wake nchi hiyo ilitoa nafasi pana kwa vyama vya upinzani na akakuza demokrasia wala hakuna mpinzani aliyewekwa lumande kama Tanzania.

Lakini msemaji wa umoja huo wa wapinzani wa Kenya alitofautiana na hoja hizo.

“Odinga ni rafiki wa wote, JPM na Waziri Mkuu Lowassa,” unasema ujumbe mfupi wa simu alioutuma mkurugenzi wa mawasiliano wa ODM, Philip Etale.

“(Odinga) Aliweka bayana wakati wa kampeni za uchaguzi kuwa anawaunga mkono wote na kutaka mgombea bora ashinde. Kama ODM tunaamini katika demokrasia na tusingependa, wakati wowote ule, tupoteze marafiki zetu kwa sababu ya siasa.

“Odinga anataka kuungwa mkono na kila mtu na ni matumaini yetu kuwa uamuzi huo hautokana na uchaguzi uliopita bali mambo mengine.”

Uchaguzi wa Rais nchini Kenya utafanyika Agosti 8 na Kenyatta, mtoto wa muasisi wa taifa hilo, Jomo Kenyatta, anawania kuongoza Kenya kwa kipindi cha pili mfululizo.


Chanzo: Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…