Raia wa China wahukumiwa miaka 30 jela ama faini ya shilingi bilioni 108.7

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,806
34,193
Raia wa China wahukumiwa miaka 30 jela ama faini ya shilingi bilioni 108.7
china(1).jpg



Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imewahukumu raia wawili wa china kulipa faini ya shilingi bilioni 108.7 ama kwenda jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo 706.

Raia hao wawili wa china, XU FUJIE na HUANG GIN wanaotetewa na makili Edward Chuwa na Nehemia Nkoko walihukumiwa kifungo hicho na Mh.Hakimu Mfawidhi,Cyprian Mkeha akisoma huku hiyo Mh.Mkeha amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi wao na hivyo kuwakuta washatakiwa hao na makosa kadhaa.

Hakimu akaongeza kuwa kwa kuzingatia hali halisi ya kesi,ushahidi na hasara ambayo taifa imeipata kutokana na tembo 226 kupoteza maisha kwa kuuwa ni wazai kuwa raia haoa wa wachina wanatakiwa kupatiwa adhabu kama hiyo.

Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, hakimu Mkeha amesema ametoa adhabu hiyo pia kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa serikali,Faraja Nchimbi Paul Kadushi na Wankyo Simon na maombi ya utetezi kuwa wapunguziwe adhabu.

Awali kabala ya huku hiyo mawakili wa serikali,nchimbi aliiomba mahaka iwape adhabu kali washtakiwa hao kwa kuwa kati ya kipindi cha 2010 na desemba 2013 hapa chini jumla ya tembo 892 waliuawa .

Alidai kuwa washtakiwa hao waliingia nchini 2010 hadi novemba 2013 walipokamatwa kwa makosa hayo na kuwepo rumande matukio ya mauaji ya tembo yalipungua.

Nchimbi alibainisha kuwa washtakiwa hao waliiua robo ya tembo wanaouawa hapa nchini na kwamba kutokana na wingi wa nyara walizokutwa nazo inaonekana wazi ni miongoni mwa vinara wakubwa , wawezeshaji na wahusika wa shughuli za ujangili zinaeoendelea hapa nchini.

Novemba 2, 2013 katika mtaa wa kifaru mikocheni kinondoni washtakiwa hao wanadaiwa kukamatwa wakiwa na nyara hizo za serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 1,880 na thamani ya sh 5,435,865,000 wakivimiliki bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.
Chanzo.:: Raia Wa China Wahukumiwa Miaka 30 Jela Ama Faini Ya Shilingi Bilioni 1087
 
Back
Top Bottom