Raia wa China wahukumiwa miaka 30 jela ama faini ya shilingi bilioni 108.7

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imewahukumu raia wawili wa china kulipa faini ya shilingi bilioni 108.7 ama kwenda jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo 706.

Raia hao wawili wa china, XU FUJIE na HUANG GIN wanaotetewa na makili Edward Chuwa na Nehemia Nkoko walihukumiwa kifungo hicho na Mh.Hakimu Mfawidhi,Cyprian Mkeha akisoma huku hiyo Mh.Mkeha amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi wao na hivyo kuwakuta washatakiwa hao na makosa kadhaa.

Hakimu akaongeza kuwa kwa kuzingatia hali halisi ya kesi,ushahidi na hasara ambayo taifa imeipata kutokana na tembo 226 kupoteza maisha kwa kuuwa ni wazai kuwa raia haoa wa wachina wanatakiwa kupatiwa adhabu kama hiyo.

Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, hakimu Mkeha amesema ametoa adhabu hiyo pia kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa serikali,Faraja Nchimbi Paul Kadushi na Wankyo Simon na maombi ya utetezi kuwa wapunguziwe adhabu.

Awali kabala ya huku hiyo mawakili wa serikali,nchimbi aliiomba mahaka iwape adhabu kali washtakiwa hao kwa kuwa kati ya kipindi cha 2010 na desemba 2013 hapa chini jumla ya tembo 892 waliuawa .

Alidai kuwa washtakiwa hao waliingia nchini 2010 hadi novemba 2013 walipokamatwa kwa makosa hayo na kuwepo rumande matukio ya mauaji ya tembo yalipungua.

Nchimbi alibainisha kuwa washtakiwa hao waliiua robo ya tembo wanaouawa hapa nchini na kwamba kutokana na wingi wa nyara walizokutwa nazo inaonekana wazi ni miongoni mwa vinara wakubwa , wawezeshaji na wahusika wa shughuli za ujangili zinaeoendelea hapa nchini.

Novemba 2, 2013 katika mtaa wa kifaru mikocheni kinondoni washtakiwa hao wanadaiwa kukamatwa wakiwa na nyara hizo za serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 1,880 na thamani ya sh 5,435,865,000 wakivimiliki bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.

Chanzo: ITV
 
Huku wanaodili na ujangili wanapeta tu ,wanaishia kufunga wala gomba maisha ,muwashike na hao wanaowauzia hizo pembe
Hivi hao mawakili wanao watetea wahalifu wa namna hiyo kwa mfano wangeshinda hiyo kesi basi wana amani na furaha kabisa ?
 
Mimi nilidhani hii kesi ingekuwa kiini cha kufumua mtandao wote wa ujangiri nchini....Hao wachina wenyewe wanaletewa ili kuexport tu kwenda kwao china.Kwahiyo ni kama wateja wa kati wanaonunua hapa na kupeleka china kuuza kwa faida.Nani anawauzia?

Wanaowauzia wachina wao wamefadhili shughuli nzima ya kuwatafuta,kuwashambulia na kuwaua na kusafirisha meno na pembe mpaka kwa hao wachina.Ni akina nani?

Na hao wanaopewa dili la kutekeleza mision huko kwenye hifadhi ni akina nani?

Ni wafanyakazi gani wa hifadhi ambao wanafanikisha huu utekelezaji ufanikiwe kwa kiwango kikubwa kiasi hiki?
 
Huku wanaodili na ujangili wanapeta tu ,wanaishia kufunga wala gomba maisha ,muwashike na hao wanaowauzia hizo pembe
Hivi hao mawakili wanao watetea wahalifu wa namna hiyo kwa mfano wangeshinda hiyo kesi basi wana amani na furaha kabisa ?



Mkuu.unakosea no1 is guilty until proven so!!kuwatetea ni matakwa ya kisheria wawe na makosa au hawana!!sasa wakat wanakamatwa who knows kama kweli wanasingiziwa au.kweli kuna mashahidi??mkuu consult lawyer akupe msaada wa mawazo
 
Hivi.wale mukulu aliosema ana list yao bado?ampe ile list kwa ngosha.kama vipi
 
Mkuu.unakosea no1 is guilty until proven so!!kuwatetea ni matakwa ya kisheria wawe na makosa au hawana!!sasa wakat wanakamatwa who knows kama kweli wanasingiziwa au.kweli kuna mashahidi??mkuu consult lawyer akupe msaada wa mawazo
Aisee asante mkuu japo sihitaji ushauri wa hao Lawyers ,Magufuli alisema mtu umemkamata read handed ni uthibitisho gani unataka japo yeye ni raisi na ana washauri wa kisheria wa kutosha ,
Halafu swali langu ni kuwa ikitokea wameshinda kesi ya namna hiyo wanakua na furaha kabisa ??
 
Mi naona wangenyongwa tu maana huko wanaenda kula ugali wa bure
 
Aisee asante mkuu japo sihataji ushauri wa hao Lawyers ,Magufuli alisema mtu umemkamata read handed ni uthibitisho gani unataka japo yeye ni raisi na ana washauri wa kisheria wa kutosha ,


Wengi watasingiziwa watateswa na kuuawa Magufuli anakurupuka!! Nani.anafanya justifications kuwa flan kakamatwa red handed??mimi binafsi siungi mkono.u dictator wa Magufuli dawa kubwa ni kuziimarisha taasisi ziwe imara zifanye kazi dawa ni mahakama ifanye kazi.kwa misingi ya haki/sheria sio.matamko ya rais..
 
Mtandao bado haujafumuliwa. .......
Hawa wangetumika kuvuruga network ya wauaji wa Tembo. ..
 
Wengi watasingiziwa watateswa na kuuawa Magufuli anakurupuka!! Nani.anafanya justifications kuwa flan kakamatwa red handed??mimi binafsi siungi mkono.u dictator wa Magufuli dawa kubwa ni kuziimarisha taasisi ziwe imara zifanye kazi dawa ni mahakama ifanye kazi.kwa misingi ya haki/sheria sio.matamko ya rais..
Mbona swali langu la msingi hulijibu hao jamaa wangeshinda kesi ya tembo takribani 300 na ushee walio uwawa hao wachina wakaachiwa huru ,wangekuwa na furaha ? Wanakaa sehemu kabisa wanagonga glass, my learned counsel we did it ,ya Magufuli tuachane nayo
 
Back
Top Bottom