Raia wa China ajifungua mapacha watatu wa kiume katika hospitali ya Regency

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
61,728
72,147
My Take: Nataka wanawake ambao wanazaa mapacha kama huyu Mchina 👇

=========

Mchina.PNG

Raia wa China, Liya Zhang (31), ambaye amejifungua watoto mapacha watatu wa kiume katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam ameshukuru kwa huduma nzuri alizopata.

Raia huyo alijifungua watoto hao siku ya Jumapili usiku hospitalini hapo na mpaka sasa anaendelea vizuri yeye na watoto wake hao watatu.

Akizungumza hospitalini hapo, Liya alisema awali wakati anahudhuria kliniki alidhani kuwa ana ujauzito wa mtoto mmoja lakini baada ya vipimo alishtuka kuambiwa kuwa ana watoto wa tatu.

“Nawashukuru sana madaktari bingwa wa watoto, Dk. Rahim na Dk. Supriya Khan kwa namna walivyonihudumia tangu awali mpaka najifungua, nimepata huduma nzuri sana hapa Regency na watoto wangu kama unavyowaona wako vizuri kabisa,” alisema Liya kwa lugha ya Kiswahili fasaha.

Liya alisema si mara yake ya kwanza kujifungua hospitalini hapo kwani mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kwanza wa kike hospitalini hapo na baadaye alikuja kujifungua mengine wawili wa kiume pia hospitaini hapo hapo na sasa amefurahi kupata watoto wa kiume watatu.

“Nilipata mtoto mmoja wa kike mwaka 2009 na baadaye nikapata mapacha wawili wa kiume na juzi Jumapili nimepata mapacha watatu kwa hiyo sasa nina jumla ya watoto sita na wote nimejifungua katika hospitali hii hii ya Regency na nadhani nitakuwa nimemaliza kwa kweli inatosha,” alisema Liya huku akicheka kwa nguvu.

Daktari bingwa wa watoto wa Regency, Dk. Rahim alisema wamekuwa wakimhudumia Liya tangu uzao wake wa kwanza ambapo alipata mtoto wakike hospitalini hapo na ujauzito wa pili ambapo alifanikiwa kupata watoto wa kiume mapacha.

“Na huu ni ujauzito wake wa mara ya tatu ambapo amefanikiwa kupata mapacha watatu wote wa kiume na uziri ni kwamba anaimani nasisi kwa muda mrefu kwani kila anapotaka kujifungua amekuwa akija hapa Regency na tunashukuru watoto wake wote wanaendelea vizuri sana,” alisema

“Tumekuwa tukihudumia wanawake wengi sana wanaojifungua lakini hii ni mara ya kwanza hapa Regency kuhudumia mwanamke kupata watoto watatu, hii ni habari njema kwetu sote,” alisema

Global Publishers
 
Hongera zake, Mungu amkuzie watoto wake.....naomba kuuliza je Regency wanapokea bima ya NHIF?
 
Hao ndy viongozi wenu wabaadae.
Wanazaliwa hapa
Watazuga kusoma hapa
Wataenda kwao kula kozi
Watarudi kujiunga na watawala
Watawatawala.
Wamejipenyeza sehemu nyingi mno.
Poor Tanzania.
Poor Afrika.
 
My Take: Nataka wanawake ambao wanazaa mapacha kama huyu Mchina 👇

=========

Raia wa China, Liya Zhang (31), ambaye amejifungua watoto mapacha watatu wa kiume katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam ameshukuru kwa huduma nzuri alizopata.

Raia huyo alijifungua watoto hao siku ya Jumapili usiku hospitalini hapo na mpaka sasa anaendelea vizuri yeye na watoto wake hao watatu.

Akizungumza hospitalini hapo, Liya alisema awali wakati anahudhuria kliniki alidhani kuwa ana ujauzito wa mtoto mmoja lakini baada ya vipimo alishtuka kuambiwa kuwa ana watoto wa tatu.

“Nawashukuru sana madaktari bingwa wa watoto, Dk. Rahim na Dk. Supriya Khan kwa namna walivyonihudumia tangu awali mpaka najifungua, nimepata huduma nzuri sana hapa Regency na watoto wangu kama unavyowaona wako vizuri kabisa,” alisema Liya kwa lugha ya Kiswahili fasaha.

Liya alisema si mara yake ya kwanza kujifungua hospitalini hapo kwani mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kwanza wa kike hospitalini hapo na baadaye alikuja kujifungua mengine wawili wa kiume pia hospitaini hapo hapo na sasa amefurahi kupata watoto wa kiume watatu.

“Nilipata mtoto mmoja wa kike mwaka 2009 na baadaye nikapata mapacha wawili wa kiume na juzi Jumapili nimepata mapacha watatu kwa hiyo sasa nina jumla ya watoto sita na wote nimejifungua katika hospitali hii hii ya Regency na nadhani nitakuwa nimemaliza kwa kweli inatosha,” alisema Liya huku akicheka kwa nguvu.

Daktari bingwa wa watoto wa Regency, Dk. Rahim alisema wamekuwa wakimhudumia Liya tangu uzao wake wa kwanza ambapo alipata mtoto wakike hospitalini hapo na ujauzito wa pili ambapo alifanikiwa kupata watoto wa kiume mapacha.

“Na huu ni ujauzito wake wa mara ya tatu ambapo amefanikiwa kupata mapacha watatu wote wa kiume na uziri ni kwamba anaimani nasisi kwa muda mrefu kwani kila anapotaka kujifungua amekuwa akija hapa Regency na tunashukuru watoto wake wote wanaendelea vizuri sana,” alisema

“Tumekuwa tukihudumia wanawake wengi sana wanaojifungua lakini hii ni mara ya kwanza hapa Regency kuhudumia mwanamke kupata watoto watatu, hii ni habari njema kwetu sote,” alisema

Global Publishers
Hongera mchina kwa kutuongezea Watanzania watatu.
 
Hawa kwao wamewekewa limit ya kuzaa Ila wakija huku wanajifanya mabingwa wa kufyatua watoto.
Wanazaa watoto watanzania hao ni wa kwetu

Wakienda likizo china hawaendi nao

Wanawake wengi china wanapenda kuzaa sana shida sheria zao hivyo wakija kwetu wanapanua mapaja yote wazalishwe
 
Sheria ya uzazi China imebadilishwa,kuhusu kuzaa watoto wachache haipo tena siku hizi.
Ni ruhusa kabisa kuzaa watoto zaidi ya wawili na tena wakifika wa 4 serkali inawapatia wazazi zawadi. Uwe unafatilia mara kwa mara taarfa.
 
My Take: Nataka wanawake ambao wanazaa mapacha kama huyu Mchina 👇

=========

Raia wa China, Liya Zhang (31), ambaye amejifungua watoto mapacha watatu wa kiume katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam ameshukuru kwa huduma nzuri alizopata.

Raia huyo alijifungua watoto hao siku ya Jumapili usiku hospitalini hapo na mpaka sasa anaendelea vizuri yeye na watoto wake hao watatu.

Akizungumza hospitalini hapo, Liya alisema awali wakati anahudhuria kliniki alidhani kuwa ana ujauzito wa mtoto mmoja lakini baada ya vipimo alishtuka kuambiwa kuwa ana watoto wa tatu.

“Nawashukuru sana madaktari bingwa wa watoto, Dk. Rahim na Dk. Supriya Khan kwa namna walivyonihudumia tangu awali mpaka najifungua, nimepata huduma nzuri sana hapa Regency na watoto wangu kama unavyowaona wako vizuri kabisa,” alisema Liya kwa lugha ya Kiswahili fasaha.

Liya alisema si mara yake ya kwanza kujifungua hospitalini hapo kwani mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kwanza wa kike hospitalini hapo na baadaye alikuja kujifungua mengine wawili wa kiume pia hospitaini hapo hapo na sasa amefurahi kupata watoto wa kiume watatu.

“Nilipata mtoto mmoja wa kike mwaka 2009 na baadaye nikapata mapacha wawili wa kiume na juzi Jumapili nimepata mapacha watatu kwa hiyo sasa nina jumla ya watoto sita na wote nimejifungua katika hospitali hii hii ya Regency na nadhani nitakuwa nimemaliza kwa kweli inatosha,” alisema Liya huku akicheka kwa nguvu.

Daktari bingwa wa watoto wa Regency, Dk. Rahim alisema wamekuwa wakimhudumia Liya tangu uzao wake wa kwanza ambapo alipata mtoto wakike hospitalini hapo na ujauzito wa pili ambapo alifanikiwa kupata watoto wa kiume mapacha.

“Na huu ni ujauzito wake wa mara ya tatu ambapo amefanikiwa kupata mapacha watatu wote wa kiume na uziri ni kwamba anaimani nasisi kwa muda mrefu kwani kila anapotaka kujifungua amekuwa akija hapa Regency na tunashukuru watoto wake wote wanaendelea vizuri sana,” alisema

“Tumekuwa tukihudumia wanawake wengi sana wanaojifungua lakini hii ni mara ya kwanza hapa Regency kuhudumia mwanamke kupata watoto watatu, hii ni habari njema kwetu sote,” alisema

Global Publishers
Mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kwanza, sasa Ă na miaka 31.
2009 hadi leo ni miaka 15, maana yake alijifungua mtoto wa kwanza akiwa na miaka 16! AlipĂ ta mimba akiwa na 15 yrs.
Hii ni kawaida kwa wachina? Maana hapa Tanzania umri huo umebaka?!
 
Aweke taarifa zake halisi public Kwa manufaa ya Nani?
 
Back
Top Bottom