Rahisi sana nchi hii kuwa tajiri, viongozi hawataki ama hawafahamu?

gstar

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
775
1,332
Mara nyingi ili nchi iwe Tajiri inategemea na uthabiti na umahiti wa serikali iliyopo madarakani, rushwa ni adui wa haki na maendeleo. Tatizo lililopo kwa nchi nyingi zinazo endelea ni ubinafsi kwa viongozi wake na hii nitabia ya viongozi wengi wa ki Afrika, inaweza kuwa ndio tabia halisi ya sisi wa Afrika!

Idadi ya watu ni sifa kubwa ya kuitajirisha nchi, nchi yetu inakadiriwa kuwa na watu wapatao milioni 60 na ushee, hivyo serikali inaweza kuzalisha ajira rasmi ama zisizo rasmi, kutoa vipaumbele na vivutio vya kikodi kwa wawekezaji wa ndani kutumia ipasavyo soko la ndani kwa bidhaa zinazo zalishwa ndani na kupunguza ama kuzuia kuagiza bidhaa kutoka nje. (Zile tunazoweza kuzalisha mf. Nguo)

Bidhaa za ndani zinahitaji masoko hivyo tukizuia kuagiza bidhaa za nje tutaongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani ambazo zitaleta tija kwa Taifa. Viwanda vielekezwe kuajiri raia wa kitanzania, kupunguza kuajiri raia wengi wa kigeni na kutoa mafunzo kwa wazawa ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kujiamini.

Viwanda tunaweza anza navyo ni kama vya nguo na usindikaji wa vyakula, pamoja na viwanda vya madawa na vifaa vya kielektroniki kama simu. Vyombo vya usafiri mfano pikipiki na magari twaweza kuanza na viwanda vya ku-asemble components na kuboresha uzalishwaji wa baadhi ya components ndani ya nchi yetu.

Udhibiti wa rasilimali za madini na maliasili mfano mbuga na udhibiti wa njia za usafiri wa majini na nchi kavu. Utoaji wa mikopo kwa vikundi vya watu na makampuni ya ndani, kubinafsisha mashirika kwa makampuni ya wasomi wa ndani, kuwajengea uwezo wa kusimamia makampuni na kulipa kodi ya serikali.

Tutapata wapi rasilimali watu na fedha?

Kwakuwa tuna vijana wa kutosha, wengi hukosa ajira kutokana na ukosefu wa ujuzi stahiki, takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya wahitimu wa kidato cha nne hupata daraja la div 4 mpaka 0 hao huonekana kwamba si lolote si chochote. Uanzishwaji wa elimu ya ufundi uwe lazima kwa mashule yote ya sekondari, elimu inayofaa kuzingatiwa ni ile ihusuyo mitambo ya viwandani, ujenzi ufundi wa elektroniki, useremala n.k. mara wanapomaliza kidato cha nne moja kwa moja wanaingia kwenye uzalishaji. Kupitia makampuni na viwanda vidogo na vikubwa vilivyoanzishwa kila Kijiji na serikali na kusimamia na wasomi wa nyanja husika.

Udhibiti wa kodi na vipaumbele vyenye tija pamoja na kubana matumizi ya serikali inaweza kuchangia kuongeza pato la ndani la nchi, kuimarisha utalii na kuimarisha sekta ya kilimo, kilimo cha kisasa mashamba makubwa yanayotuimia teknolojia ya kisasa, kuuza mazao nje ya nchi ili kuongeza fedha za kigeni. Uchimbaji wa madini ya vito na madini mengine uzingatie maslahi ya kitaifa. Ukopaji wa fedha za kuanzisha na kusimamia miradi udhibitiwe na fedha zielekezwe sehemu husika.

Kuzingatiwa maadili ya nchi kwa kutoa elimu dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa Pombe kupitia kiasi kupunguza uuzwaji holela wa vileo na kudhibiti uzembe na uzururaji. Nahitaji kupewa nafasi hata nisaidie kwenye hili kama kuna nafasi ya kurekeleza haya naamini inawezekana kuyasimamia, tukiwa na nia ya kweli na team ya watu sahihi.
 
Back
Top Bottom