Nipe Andiko
Senior Member
- Jan 20, 2017
- 133
- 133
KESI YA JAMHURI NA MWALIMU RESPICIUS PATRICK MTAZANGIRA PAMOJA NA HERIETH D/O GERALD, KWA LUGHA YA KISWAHILI (TAFSRI ISIYO RASMI)
THE REPUBLIC
VERSUS
1. RESPICIUS S/O PATRICK@ MTAZANGIRA
2. HERIETH D/O GERALD
SWAHILI VERSION.
Hii ni kesi inayohusu kupigwa hadi kuuawa kwa aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta, Iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Sperius Eradius, na Mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo, kwa madai kuwa aliiba pochi.
Ambapo mtuhumiwa mmoja (Mwalimu Respecius) alikutwa na hatia ya mauaji na kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa mpaka kufa. Mtuhumiwa mwingine (Mwalimu Harieth) alikutwa bila hatia na kuachiwa huru.
KESI AMBAYO IMEVUTA HISIA ZA WATU WENGI SANA. NAMI KWA KUGUSWA NA KUONA UMUHIMU WA KESI HII, NIMEAMUA KUIFASRI YOTE KWA LUGHA YA KISWAHILI, ILI IWAFIKIE WATU WENGI, HASA WAALIMU AMBAO NDO WAHUSIKA WAKUU: (Hasa waalimu, Mwalimu yeyote husika tafadhali.). Tunafahamu wanafunzi wanavyoadhibiwa huko mashuleni kinyume cha utaratibu, Fuateni utaratibu kabla hayajawakuta
KESI HII IWE FUNZO (LESSON) KWA WAALIMU WOTE WENYE TABIA YA KUADHIBU WANAFUNZI VIKALI KINYUME CHA SHERIA
Kwa kusoma kesi hii, utajifunza vingi, mfano, Ushahidi unaotakiwa Mahakamani ili kushinda kesi, na jinsi ya kumbaini shahidi mwongo na mkweli.
Utafahamu, kama maelezo yanayotolewa kituo cha polisi yanaweza kutumika kama ushahidi Mahakamani na kuzingatiwa?
Na nini kitatokea endapo mashahidi kwenye kesi wanatoa ushahidi ambao unatofautiana kuhusu kitu kile kile kimoja (contradictions) kama ilivyokuwa kwenye hii kesi.
Pia, utajua NIA (INTENTION) inapimwaje au kutazamwa Mahakamani ili kujua kama mtuhumiwa alikusudia kuua ama la! Vitu gani vinaashiria mtu alikusudia kuua?
Vilevile, Utafahamu utaratibu sahihi na kununi za kutoa adhabu ya viboko shuleni. Wakati gani adhabu ya viboko hutolewa? Nani ana Mamlaka kutoa adhabu ya viboko? Nini kitatokea Mwalimu asipofuata utaratibu sahihi wa kutoa adhabu ya viboko? Na kama mwanafunzi akigoma hatua gani zitachukuliwa? Hayo na Mengine mengi, utayapata kwenye hii kesi.
(KWA KUWA NI KESI NDEFU, UNAWEZA KUIKOPI AU KUHIFADHI SEHEMU UNAYOWEZA KUIPITIA BAADAE UKASOMA TENA)
TAFADHALI USIBADILI MAUDHUI, (NARUDIA HII NI TAFSRI ISIYO RASMI, LAKINI MAANA (TONE) NI ILE ILE, KILICHOBADILIKA NI LUGHA TU).
KARIBU:
Kesi ilikuwa kati ya JAMHURI na washtakiwa wawili ambao ni
1. RESPICIUS S/0 PATRICK@ MTAZANGIRA na
2. HERIETH D/O GERALD
22/2 & 6/3/2019
Kesi hiyo ilisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Bukoba Registry, mbele ya Judge L.M. MLACHA, J.
FACTS:
Sperius Eradius, Mwanafunzi wa darasa tano, mtoto wa kuasiliwa (adopted) wa Mchungaji Justus Balilemwa. Alienda shuleni asubuhi na mapema kama kawaida. Akapangiwa kusafisha madarasa yeye na wenzake. Na wakafanya. Hakuna shaka kwamba, Alikuwa na afya njema, na hakuna aliyefkri atakufa baadae siku hiyo.
Kijana Sperius Eradius, Sasa amefariki, na hii kesi imeletwa kuchunguza sababu za kifo chake na kuwapa adhabu wale watakaobainika na mauaji hayo.
Taarifa ya kifo cha Sperius Eradius ilifika kituo cha polisi Bukoba siku hiyo hiyo majira ya saa saba mchana. Ambapo ilikuja baadae kuhusishwa na waalimu wawili Respicius Patrick@ Mtazangira na Harieth Gerald katika kesi iliyofunguliwa mahakamani, ilidaiwa kwamba Mwalimu Respicius Patrick @ Mtazangira na mwenzake Harieth Gerald wamemuua Mwanafunzi Sperius Eradius tarehe 27/08/2018 katika shule ya msingi Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoa wa Kagera.
Watuhumiwa walikana mashtaka
Kesi ilikuwa na mashahidi tisa (9) upande wa mashtaka/Jamhuri na Mashahid watatu upande wa Watuhumiwa.
Vielelezo vilivyotolewa kama ushahidi mahakamani:
{I} Taarifa (Report) mbili za madaktari kuhusu uchunguzi wa mwili wa marehemu ili kujua sababu za kifo chake. (Two postmortem reports) na
{II} Fimbo tatu kubwa au kuni.
(3 big sticks or fire woods.)
Kifo cha Sperius Eradius kimevuta hisia za watu wengi mno. Kwa sababu ni nadra kusikia waalimu wameshtakiwa kwa kosa la kuua mwanafunzi.
Polisi walikuwa na kazi ngumu sana. Ndugu hawakuiamini report ya kwanza ya Daktari. Hii ilipelekea kufanyika kwa uchunguzi mwingine wa mara ya pili.
Shule nzima iliweweseka. 27/08/3018 Ilikuwa ni kilio. Baadhi ya Wanafunzi na waalimu walimlilia Sperius Eradius.
TWENDE KWENYE KESI KUANZA KUSIKILIZWA RASMI:
Hakimu alianza na upande wa Mashtaka (Jamhuri).
Shahidi namba moja (PW1) Benigius Benezeti, ambaye ni bodaboda aliiambia Mahakama kuwa, alipigiwa simu na Mwalimu, Maadam Harieth Gerald, mteja wake wa siku zote, tarehe 27/8/2018, majira ya saa moja kamili asubuhi.
(Bodaboda) akaja akamchukua mpaka shule ya msingi Kibeta.
Ambapo Mwalimu (Harieth) alipokelewa na Wanafunzi. Mwalimu alikuwa na kikapu chenye chupa ya chai, kipande cha kitenge, mtandio na koti.
Vyote hivyo vilichukuliwa na Wanafunzi ambao walikuwa wamekuja kumpokea.
Punde tu, Mwalimu Harieth akagundua pochi yake haipo. Akamtuma bodaboda afuatilie njiani kuitafuta.
PW 1 (Bodaboda) akaenda ila hakuipata.
Baadae (bodaboda) akapewa taarifa na Mwalimu Harieth kwa njia ya simu kwamba, pochi imeonekana na Mwanafunzi wa darasa tano.
Bodaboda akamwachia hilo suala mteja wake akaendelea na shughuli zake.
PW4 (Shahidi namba nne upande wa Mashtaka/Jamhuri), Goodluck Gilbert
ambaye Alikuwa kaka mkuu
na PW6 (Shahidi namba sita upande wa Mashtaka/Jamhuri) Mericiana Yohana, ambae Alikuwa dada mkuu.
Wote, Wanafunzi wa shule ya msingi Kibeta
Ushahidi wao ambao pia uliungwa mkono na Shahidi namba 7 (PW 7) Enata Isidori (Mkuu wa shule) na Shahidi namba nane (PW8) Sundi Elisha (Mkuu wa shule msaidizi)
Waliunga mkono ushahidi uliotolewa na bodaboda au shahidi namba moja (PW1)
Kwamba, Mwalimu Harieth alikuja na pikipiki (bodaboda) asubuhi na akapokelewa na wanafunzi na darasa la pili ambao walibeba mizigo yake.
Baadae (Mwalimu Harieth) akaja asubuhi mstarini (SMART AREA), na akataka kujua kama kuna mwanafunzi yeyote amemwona mtu aliyechukua pochi yake?
Hakuna aliyejitokeza kusema amemwona mtu yeyote. Wanafunzi wakaenda darasani.
Mwalimu Harieth akapiga hatua kwenda darasa la nne, ambapo mwanafunzi mmoja kwa jina Elia alidai amemwona Sperius Eradius, Marehemu, akichukua pochi.
Sperius Alikuwa darasa la tano.
Mwalimu Harieth akaenda darasa la tano na kumchukua Sperius. Akataka kujua kama Sperius alikuwa mwizi au alikuwa na tabia ya kutoroka shuleni?
Darasa wakasema HAPANA
Mwalimu Harieth akaondoka na Sperius akampeleka mpaka ofsini (staff room) na kumwuliza kama amechukua pochi au la?
Sperius akasema HAPANA.
Mwalimu Harieth akamchapa Sperius fimbo tatu (3) kwenye mikono.
Kisha akaagiza kengele igongwe. Wanafunzi wakapanga mstari. Akawauliza kama kuna yeyote alimwona Sperius akichukua pochi?
Wanafunzi wawili wa darasa la nne (Flora na Imelda) wakasema, ni Sperius ndiye aliichukua. Wengine wakasema HAPANA.
Mwalimu Harieth akaagiza begi la Sperius na dada yake (Irene) yakaguliwe. Zoezi hilo likafanyika ila pochi haikuonekana.
Kisha Mwalimu Harieth akamkabidhi Sperius kwa Mwalimu Respicius, mkuu wa nidhamu (discipline master).
Shahidi namba nne upande wa Mashtaka/Jamhuri (PW4), Goodluck Gilbert (Kaka mkuu), aliiambia Mahakama kuwa;
Mwalimu Harieth alimsimulia kwa ufupi Mwalimu Respicius (mkuu wa nidhamu), akisema Wanafunzi wamemtaja Sperius kuwa amechukua pochi lakini Sperius anakana. Na kwamba amemchapa fimbo tatu lakini bado, Sperius anasema Hapana.
Mwalimu Respicius (Mkuu wa nidhamu) akamuuliza Sperius kama amechukua pochi au la! Sperius akakataa.
Mwalimu huyo wa nidhamu (Respicius) akamchukua mwanafunzi (Sperius) mpaka ofsini kisha akachukua fimbo.
Akamuuliza tena mara ya pili swali lile lile. Sperius akasema HAPANA.
Akamchapa Sperius mguuni, mgongoni na kichwani. Akampiga Sperius fimbo nyingi nyingi kabla ya kumwamuru apige magoti.
Kisha akauliza tena, "wewe umechukua pochi?" Sperius akasema HAPANA.
Mwalimu Respicius (mkuu wa nidhamu) akamwagiza PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu), achukue fimbo kutoka kwenye kuni (fire woods) ambazo zilikuwepo nje ya ofsi, huku akimuonesha kipande fulani cha kuni.
PW4 akaona kile kipande ni kikubwa mno. Akachukua fimbo ndogo na kumpelekea Mwalimu
Mwalimu Respicius akampiga nayo mgongoni huku akisema, hiyo haikuwa ile anayotaka
Akamwagiza awaite Wanafunzi wa darasa la nne ambao walikuwa na mapanga. Walipokuja akawaagiza kuleta vipande sita vya kuni (six (6) pieces of fire woods) na waviweke tayari kwa kazi (and prepare them for the job.)
Wakaleta vipande sita na kumkabidhi.
Akachagua vitatu kati yake, vile ambavyo vilikuwa vimenyooka vizuri. Kisha akabeba kimoja akamfuta Sperius na kumwagiza avue kaptura zake na viatu
Sperius akavua akabaki na “pensi” & “bukta”
Kisha Mwalimu Respicius akaanza kumpiga na fimbo. Akampiga kwenye viungo (joints) vya miguu na mgongoni.
Sperius akakubali kuwa yeye ndo ana pochi. Mwalimu Respicius akawatuma PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu) na wanafunzi wawili wa darasa la saba kwenda na Sperius kuleta pochi.
Wakaenda na Sperius lakini hawakuipata.
Sperius Akawaambia kwamba, alikuwa amekubali ili asiendelee kupigwa zaidi.
Wakamrudisha tena kwa Mwalimu Respicius, ambae alipatwa na hasira na kusema “ngoja niwaonyesheni kazi ya jiwe”.
Mwalimu Respicius, akasogea darasa la saba na kuchukua BIKARI. Kisha akarudi kwa Sperius na kusema, “Nitakuwekea alama ambayo utamuwekea hadi mjukuu”.
Akaingiza BIKARI kwenye kidole cha Sperius kwenye kucha na kuvuta kucha kuja juu. Akafanya hivyo, huku akisema, “Niambie waleti ilipo”
Sperius akasema NO.
Mwalimu Respicius akavuta juu kucha.
Sperius akasema “sina”. Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga kwa kutumia fimbo
Hali ya Sperius ikabadilika na kuwa mbaya. Kisha (Sperius) akasema “acha niwapeleke pochi ilipo”
Wanafunzi wakaambatana na Sperius kwenda kutafuta pochi. Wakiwa na Mwalimu wao. Wakafika ile sehemu ila hawakuipata.
Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga Sperius, ambapo alianguka wakiwa njiani wakati wanashika barabara kutoka vichakani.
Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga Sperius huku akisema “huu ni usanii, hivi sivyo wanavyozimiaga”
Wakasimama pale kwa muda. Sperius akapata nguvu. Akasema kwamba hawezi kutembea na akaomba kubebwa
Mwalimu Respicius akampiga tena akisema huo ulikuwa ni “usanii” kama mpango (plan) wa kutoroka. Akaagiza Wanafunzi wavue masweta yao Kisha wampepee apate hewa. Wanafunzi wakafanya hivyo.
Sperius akapata nguvu kiasi. Wakaelekea jengo la chekechea kutafuta pochi. Lakini hawakuweza kuipata. Mwalimu Respicius akampiga kichwani. Sperius akaanguka chini. Akapiga kifua kwenye jiwe. Akaishiwa nguvu.
Mwalimu Respicius akaita bodaboda. Wakapanda pikipiki na Sperius na kuondoka.
PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu) alielezea muda na kusema kipigo kilianza saa mbili kamili (8:00 AM) asubuhi na kuendelea mpaka saa tano kamili (11:00 AM) asubuhi.
Ushahidi wa (Shahidi namba sita upande wa Mashtaka/Jamhuri) PW6 Mericiana Yohana, ambae Alikuwa dada mkuu unafanana na huo wa PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu) in all material areas.
Shahidi namba 7 (PW 7) Enata Isidori (Mkuu wa shule) alitoa ushahidi kuwa, alikuja ofsini mapema siku hiyo.
Yeye na Mratibu Elimu wa kata (Ward Education Coordinator) walikuwa na mpango wa kwenda kutafuta Wanafunzi watoro wa darasa la saba.
Walipanga wawarudishe shule ili kujaza form za TSM9 ili waweze kufanya Mitihani yao ya mwisho
Hiyo ilikuwa pia ni wiki ya Mitihani na shule ilikuwa tayari kwa ajili ya Mitihani.
Akiwa ofsini, majira ya 7:15 AM, Mwalimu Harieth akaja na kusema kwamba pochi yake imepotea.
Wakawa na majadiliano kadhaa. (Mkuu wa shule) Akamshauri Mwalimu Harieth, afuatilie njiani hadi nyumbani kwake. Mwalimu Harieth akaomba ruhusa na kuondoka.
PW7 Enata Isidori (Mkuu wa shule) akampangia Mwalimu Alpinensia kuendelea na majukumu ya Mwalimu Harieth, ambayo ilikuwa ni kusimamia Mitihani ya darasa la pili.
PW7 (mkuu wa shule) akaondoka na kumwachia uongozi wa shule PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi
Shahidi namba nane upande wa Mashtaka/Jamhuri, PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi alitoa ushahidi kwamba, aliwasili shuleni siku hiyo na pikipiki na kuelekea moja kwa moja kwenye ofsi ya mkuu wa shule kusaini daftari la mahudhurio.
Akamkuta Mwalimu Harieth Ofsini. Wakasalimiana kila mmoja. Mwalimu Harieth akamwomba amzuie dereva pikipiki (bodaboda) asiondoke, akisema kwamba alikuwa amepoteza pochi yake. Na akataka kutoka nje.
Akamtaka bodaboda asubiri. Bodaboda akabaki na Mwalimu Harieth.
Kisha PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi aliachiwa uongozi wa shule na Mkuu wa shule kama ilivyoelezwa hapo awali.
PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi alitoa ushahidi wake kwamba Mwalimu Harieth alikuja baadae na kusema hajafanikiwa kuipata pochi njiani.
Aliwauliza Wanafunzi wa darasa la pili kama wameiona pochi, wakasema HAPANA. Akaondoka na baadae akaja na Sperius akasema baadhi ya wanafunzi wamemwona na pochi.
PW8, Mkuu wa shule msaidizi akamtahadharisha kuwa sio vizuri kuwaamini sana Wanafunzi. Akamshauri kutafuta uthibitisho zaidi.
Wakawaita wanafunzi. Mwalimu Harieth akaahidi kutoa Tsh 5, 000 kwa mwanafunzi ambae angeweza kumwonesha aliyechukua pochi.
Baadhi wakasema kwamba walimwona Sperius anaichukua, wengine wakasema HAPANA
PW8, (Mkuu wa shule msaidizi) Akamshauri Mwalimu Harieth kutafuta uthibitisho zaidi. Mwalimu Harieth hakuweza kupokea ushauri wake.
Mwalimu Harieth akamchapa Sperius fimbo tatu kwenye matako.
Sperius alishika fimbo wakati Mwalimu Harieth anaenda kupiga fimbo ya nne
Sperius akaenda kwa PW8 (Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi), akisema, “Naomba msaada”.
Mwalimu Harieth akamjibu PW8 akisema “Kwani wewe ndio umemtuma hiyo walet?”
Kisha Mwalimu Harieth akamchukua mwanafunzi huyo na kumpeleka kwa mwalimu wa nidhamu (discipline master).
Kwa kuwa ulikuwa muda wa Mitihani, PW8 akaelekea darasani kuendelea kusimamia Mitihani ya MEMKWA, akawaachia mgogoro huo Mwalimu Harieth na Mwalimu Respicius (Mwalimu wa nidhamu)
PW8 anashuhudia kuwa, alipata taarifa ya kupigwa kwa mwanafunzi kutoka kwa Mwalimu Claudia Modest.
PW8, alikuwa Kwenye darasa la MEMKWA wakati huo.
Wakaenda hima ofsini ambapo alimwona Mwalimu Respicius anampiga mwanafunzi kwa kipande cha ukuni. Akamsukuma Mwalimu Respicius pembeni, akachukua kipande cha ukuni na kukirusha mbali. Kisha akamtoa Sperius nje ya ofsi
Hali ya Sperius ilikuwa mbaya.
Mwalimu Respicius akamwambia kwamba, Sperius tayari amekiri kilichobaki ni kwenda na kuleta pochi.
PW8, Akamwamuru Mwalimu Harieth waende na (Mwalimu wa nidhamu) hadi eneo husika. Wakaondoka pamoja, ila Mwalimu Harieth akarudi muda si mrefu, huku akisema kwamba Mwalimu Respicius alikuwa amemruhusu arudi wakiwa njiani na kumwambia kuwa ataenda peke yake.
PW8 hakujua kilichoendelea kwa Sperius, alikuja kujua baadaye.
PW8 akamsimulia PW7, Enata Isidori (Mkuu wa shule) alipokuja baadaye siku Hiyo, kwamba Mwalimu Respicius amempiga Sperius sana na kuondoka naye kwenda kusikojulikana.
PW7 (mkuu wa shule) akampigia simu Mwalimu Respicius ambaye alirudi baadaye peke yake bila Sperius, na kuwaambia kwamba hakupata ushirikiano kutoka kwa wazazi wa Sperius na kwamba amemwacha Sperius nyumbani.
Muda si mrefu polisi wakafika pale shuleni na kuwaambia kuwa Sperius amefariki.
Siku ikageuka kuwa mbaya kwa waalimu na wanafunzi kwa vilio.
Mwalimu Respicius akatafutwa lakini hakuonekana. Alikuja kukamatwa baadae kutoka kichakani ambapo alikuwa amejificha, akatiwa pingu na kupelekwa kituo cha polisi.
PW7, PW8 na Mwalimu Harieth, nao pia walipelekwa kituo cha polisi kuhojiwa.
Na kuhusu kilichoendelea pale, baada ya kuondoka kwa Mwalimu Respicius na Mwanafunzi Sperius
Kuna ushahidi wa Shahidi namba mbili upande wa Mashtaka/Jamhuri, PW2 Happiness Tinkaligale ambaye ni mama (Mlezi) wa Sperius na Shahidi namba tatu upande wa Mashtaka, (PW3) Simon Samson.
PW2, mama (Mlezi) wa Sperius, aliiambia Mahakama kuwa, alipata taarifa kwamba Sperius alikuwa kando ya njia hajiwezi.
Akachukua pikipiki na kuelekea hilo eneo. Akamkuta Sperius eneo linaitwa Radio Vision. Huku kukiwa na watu kibao. Akamwona na Mwalimu Respicius amesimama ameshikilia fimbo.
Sperius alikuwa amelazwa chini hajiwezi na haongei. Mama (Mlezi) wa Sperius akataka kujua kipi kimetokea kwa mwanae.
Mwalimu Respicius akajibu kwa kifupi kwamba “Amekwapua”. Sperius hakuwa na kaptura wala viatu. Shati lake lilikuwa limevaliwa nusu upande.
Mama wa Sperius akaomba msaada watu waliokuwepo pale na kumpeleka Sperius Hospital ya mkoa apate msaada.
Mwalimu Respicius, akachukua pikipiki nyingine wakati huo na kukimbia. Sperius aliwekewa Oxygen, lakini muda si mrefu ikatangazwa amefariki.
Taarifa zilitumwa polisi na PW3, Simon Samson. PW3 pia ni miongoni mwa waliowachukua Sperius na mama yake na kuwapeleka hospitali. Ushahidi wake unafanana na huo wa PW2 (mama wa Sperius) katika kila kitu.
Alisimulia kuwa Sperius alikuwa amevimba miguu na kichwa. Pia aliona alama za kupigwa kwenye mbavu.
Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Dr. Kahima Jackson, Daktari wa magonjwa kutoka Hospital ya Rufaa Bugando
Huu ulikuwa ni uchunguzi wa mara ya pili ambao ulifuatia, baada ya uchunguzi wa awali uliofanywa na Dr. Otieno (DW3).
Dr. Kahima alitoa maelezo ya uchunguzi. Ambapo alifanya vipimo vya nje na ndani.
Vipimo vya nje vilionyesha baadhi ya majeraha yaliyotofautiana ukubwa, urefu na upana. Majeraha hayo yalikuwa kichwani, usoni, mashavuni, nyuma ya shingo, mabegani, mikononi, kifuani, mgongoni, tumboni, matakoni, na kwenye miguu yote miwili.
Alisema kwamba 95% ya majeraha yalikuwa ni alama (makovu) zilizosababishwa na kitu kisichokuwa na ncha kali (butu). Pia akaongeza kuwa, kulikuwa na aina mbalimbali za alama (makovu) kichwani na mikononi.
Na kwamba kulikuwa na alama kidoleni zilizowekwa na kitu chenye ncha kali (Kama kuchoma).
Alifungua kichwa, kifua na tumbo ila hakuweza kuona tatizo ambalo lilisababisha kifo. Alitaja sababu ya kifo kuwa Neurogenic shock iliyotokana na kitu kisichokuwa na ncha kali (blunt object).
Taarifa yake ya uchunguzi ilipokelewa Mahakamani kama kielelezo P1.
Shahidi namba tisa upande wa Mashtaka/Jamhuri PW9, Inspekta msaidizi Christopher Kapela ndiye alikuwa mpelelezi wa kesi. Alielezea namna alivyopata taarifa, na kwenda shule kukamata mtuhumiwa na akakusanya ushahidi.
Ambapo alichora ramani mbili za eneo la tukio, pale shuleni (Kielelezo P2) na eneo ambapo Sperius alikutwa na kuchukuliwa na mama yake. (Kielelezo P3). Vilevile aliwasilisha vipande vitatu (3) vya ukuni (Kielelezo P4) ambavyo inadaiwa vilitumika kutekeleza uhalifu.
KUSIKILIZWA KESI UPANDE WA MTUHUMIWA/MSHTAKIWA:
Mtuhumiwa alikuwa na haya ya kusema katika kujitetea.
Shahidi namba moja DW1, Respicius Patrick Mutazangira (51) (Mtuhumiwa mwenyewe) aliiambia Mahakama kwamba, alienda shuleni mapema siku hiyo na kuanza kufundisha wanafunzi wa darasa la saba.
Yeye ni Mwalimu wa hesabu na Sayansi. Alikuwa na kipindi maalum cha hesabu siku hiyo ambacho kilianza saa 7:00 AM. Alifundisha mpaka 8:40 AM, akaondoka na kwenda ofsini (staff room) kusahihisha makaratasi.
Punde, Mwalimu Harieth akamjia na kusema kwamba pochi yake imeibiwa na Mwanafunzi. Akamtaja huyo mwanafunzi kuwa ni Sperius, marehemu.
Akawaita wanafunzi wa darasa la sita na darasa la saba karibu na Ofsi. Akamtuma Amimu Haruna awaite wazazi wa Sperius. Pia akawaagiza wanafunzi kwenda na kumleta Sperius. Ila muda si mrefu, Mwalimu Harieth akaja na Sperius staff room na (Mwalimu Harieth) akamwomba (Mwalimu Respicius) amsadie.
Akataka kujua Sperius alikuwa wapi. Sperius akanyamaza. Akampiga fimbo tatu mikononi kwa kosa la kuondoka nje ya shule bila ruhusa.
Kisha akagundua kuwa Sperius alivaa kaptura nne (4). Hiyo ilikuwa tabia mbaya. Akamwamuru avue kaptura tatu (3). Akabaki na kaptura ya shule, bukta na nguo ya ndani (pants). Akampiga fimbo tatu miguuni kwa hilo kosa.
Mwalimu Sundi Elisha (PW8) Mkuu wa shule msaidizi, akafika wakati huo, akachukua fimbo na kuitupa mbali.
DW1, Respicius Patrick Mutazangira (mtuhumiwa). Aliilezea fimbo hiyo kuwa ni fimbo ya mwanzi na sio ukuni kama walivyosema PW4, PW6 and PW8.
DW1 (mtuhumiwa) akaendelea kusema kwamba, alimchukua mwanafunzi (Sperius) kwa nia ya kwenda kuwaona wazazi wake nyumbani. Na kwamba, hakuweza kutembea sana kwa sababu alikuwa na matatizo ya kiafya. Akachukua pikipiki
Wakaondoka na Sperius. Ila wakati wako njiani, kukazuka mabishano kati yake na dereva wa pikipiki, kuhusu kiasi cha nauli anachotakiwa kulipa.
Bodaboda alitaka 3,000/= akisema eneo wanakoenda ni mbali sana. Wakashindwa kuelewana. Akamlipa 1,000/= akashukia njiani. Akiwa pale, akatokea mwanamke fulani na kuuliza kipi kilikuwa kinaendelea. Akamwambia kuwa, anawatafuta wazazi wa Sperius.
Yule mwanamke akachukua simu yake na kumpigia mtu fulani. Akaja mwanamke mmoja na kupiga yowe akisema “unamuua mwanangu!”
Watu wengi wakaja. Yule mwanamke akamchukua mwanafunzi akaondoka. Na yeye (mtuhumiwa) akachukua pikipiki na kurudi shuleni.
Akapigiwa simu na Mkuu wa shule akiwa njiani. Akafika shuleni na kuwasimulia waalimu kilichotokea. Kisha akondoka shuleni kwenda kutafuta simu yake. Ambapo ilimchukua takribani masaa mawili (2) kwa sababu kulikuwa na mvua kubwa. Akiwa anarudi shuleni, aliwekwa chini ya ulinzi.
(Mtuhumiwa) Alikana kumpiga mwanafunzi, isipokuwa tu kwa zile fimbo sita za mwanzi.
DW2, Shahidi namba mbili (Mshitakiwa/mtuhumiwa mwingine), Harieth Gerald Sahini ( 47), Aliiambia Mahakama kwamba, aliwasili shuleni siku hiyo na kupokelewa na wanafunzi wa darasa la tano, la nne na la pili. Akafungua pochi yake na kumpa bodaboda Tsh 1,000/=
Alikuwa na kikapu, pochi, koti, kitenge na mtandio wa kichwani, ambavyo aliwapa wanafunzi. Akabaki mikono tupu. Akaelekea Ofsi ya Mkuu wa shule kusaini daftari la mahudhurio.
Kisha akaenda staff room kukagua mizigo yake. Kila kitu kilikuwepo isipokuwa pochi. Akarudi kwenye Ofsi ya Mkuu wa shule na kumwambia kwamba pochi yake imepotea.
Mkuu wa shule akamwelekeza afuatilie kwa wanafunzi waliompokea. Akaenda kwa wanafunzi wa darasa la pili. Wakamwambia aliyeichukua ni Sperius, mwanafunzi wa darasa la tano. Pia aliambiwa kwamba Flora, Imelda na Elia walikuwepo pia.
DW2 (mshitakiwa) Harieth Gerald, akaendelea kusema kwamba, alienda darasa la tano ila hakuweza kumpata Sperius.
Akaripoti suala hilo kwa Mwalimu wa nidhamu (Mwalimu Respicius) na akamwachia alishughulikie. Yeye akaenda darasa la pili kusimamia Mitihani.
(Mshitakiwa) Harieth Gerald alikana kuhusu kurudi nyumbani kutafuta pochi siku hiyo. Alikana kuongea na bodaboda (PW1) kwenye simu kuhusu pochi. Pia Alikana kumpiga mwanafunzi (Sperius).
Akitaja vilivyokuwemo kwenye pochi, Mshitakiwa (Harieth Gerald) alisema, Pochi ilikuwa na simu, vitambulisho (Kitambulisho cha kazi, cha Taifa na
cha kura) na Tshs. 75,000/=.
Na kwamba hakuweza kuipata pochi hadi sasa. Alikana kuhusika kwenye mauaji ya mwanafunzi (Sperius). Alikubali kuwa, yeye pamoja na waalimu Wengine walipelekwa kituo cha polisi baadaye siku hiyo, kama ilivyotangulia kuelezwa huko juu.
(Daktari) kama Shahidi namba tatu, upande wa utetezi/Defence (Washtakiwa), DW3 Dr. Felix Otieno aliiambia Mahakama kwamba,
Alifanya uchunguzi wa kwanza wa mwili wa marehemu (first Post-Mortem
examination) siku hiyo hiyo 27/08/2018. Akaona alama/makovu mbalimbali ya zamani usoni, mikononi, miguuni, mgongoni na tumboni. Akafunua tumbo ila hakuona chochote kisichokuwa cha kawaida.Taarifa yake ilipokelewa kama kielelezo D4.
DW3 Dr. Felix Otieno alielezea sababu ya kifo kuwa, majeraha ya kimwili (physical injury.)
Upande wa utetezi (washtakiwa) ulikuwa na vielelezo vingine vitatu, ambavyo ni maelezo yaliyotolewa polisi na Simon
Samson (PW3), Goodluck Gilbert (PW4) na Mericiana Yohana (PW6).
Vielelezo hivi vilitolewa na kupokelewa kwa ajili ya kulinganisha maelezo.
Washtakiwa walitaka kulinganisha kilichosemwa kituo cha polisi na kilichosemwa Mahakamani, hususani kwenye maelezo yanayohusu pochi.
Wawakilishi (Mawakili) wa pande zote mbili walipewa nafasi kuongea na Mahakama katika uwasilishaji wao wa mwisho.
Mr. Kabunga na Ms. Aneth Lwiza waliwakilisha upande wa utetezi (washtakiwa) huku Mr. Hashimu Ngole PSA (Wakili mkuu wa Serikali) akiwakilisha upande wa Mashtaka (Jamhuri)
Upande wa utetezi (Washtakiwa), walidai kwamba Washtaki (Jamhuri) wameshindwa kuthibitisha kesi pasipo na shaka na wakaiomba Mahakama iwaachie huru watuhumiwa.
Wakairejesha Mahakama kwenye kesi ya Nathaniel Alphonce Mapunda and another v. R [2006] TLR 395 wakisema ni heri kuwaachia huru watu 100 wenye hatia kuliko kumfunga kimakosa mtu mmoja asiye na hatia.
Wakasema, kesi ya Jamuhuri ina mkanganyiko (Utata) unaopelekea iwe dhaifu. Wakarejea kesi ya Christian Kale and Another v. R [1992] TLR 302 kuunga mkono hoja yao kwamba, Watuhumiwa mbele ya Mahakama wasifungwe kwa sababu tu ya udhaifu wao katika kujitetea ila kwa sababu ya ushahidi wenye nguvu wa upande wa Mashtaka (Jamhuri).
Waliwasilisha kuwa, Mkanganyiko (Utata) na kutofautiana kwa maelezo ya mashahidi upande wa Jamhuri, vimeharibu uaminifu wa mashahidi wa msingi wa Jamhuri, ambao ni PW4, PW6 na PW8.
Wakasema kwamba, kule kuwepo tu kwa watuhumiwa shuleni siku hiyo ya tukio, kusichukuliwe kuwa wao ndio waliomuua marehemu. Wakarejerea kesi ya Damian Petro v.R [1980] TLR 260 kuunga mkono hii hoja yao.
Pia upande wa utetezi waliirejesha mahakama kwenye kesi ya Salum Mhando v.R [1993] TLR 170, Crospery Ntalinda v R CAT Criminal Appeal No.312 of 2015, Goodluck Kyando v R [2006] TLR 363, Michael Aeshi v R [1992] TLR 92 and Kibwana Salehe v R [1968] TLR 391 kuonesha kwamba, kukiwa na mkanganyiko (Utata), ushahidi huo lazima ukataliwe. Wakaongeza kuwa, uaminifu wa mashahidi umeharibiwa.
Upande wa utetezi (washtakiwa), ukaonesha maeneo yafuatayo kama sehemu zenye (mkanganyiko) utata;
Moja, ushahidi kuhusu pochi.
pili, ushahidi kuhusu idadi ya kengele zilizolia siku hiyo.
Tatu, ushahidi kuhusu kutolewa kwa kucha na
Nne, ushahidi kuhusu sehemu ambayo Mwalimu Harieth alimpiga Sperius fimbo.
Pia waliongezea kwa kutaja maeneo mengine mawili;
Kwamba, upande wa Mashtaka umeshindwa kumuita Mwalimu Alipensia athibitishe kuwa yeye ndo alisimamia Mitihani siku hiyo, kitu ambacho kinawabeba. (A fact which give an advantage to them).
Wakaielekeza Mahakama kwenye kesi ya Aziza Abdalah v R [1991]TLR 71, wakidai kwamba kushindwa kumleta Shahidi muhimu, kunaipa Mahakama haki ya kuja na tafsri yoyote kuhusu jambo husika kwenye kesi. (Entitle the court to an
adverse inference to the prosecution on the point.)
Pia walidai kwamba, ushahidi wa uchoraji ni wa kukuzwa (kutiwa chumvi mno) hivyo unapaswa kupuuzwa. (Evidence on feinting is an exaggeration which should be neglected.)
Wakizungumzia (Sheria ya) Education No. 24 of 2002, upande wa utetezi, walidai kwamba, haiwafungi wateja wao, kwa sababu kulikuwa na ushahidi unaoonyesha kuwa, mshtakiwa (mtuhumiwa) namba mbili (Mwalimu Harieth) hakumpiga mwanafunzi, na zile fimbo sita alizochapa mtuhumiwa namba moja (Mwalimu Respicius) zilikuwa zimehalalishwa na baraza la shule (had justification from the school committee).
Wakielezea yaliyomo kwenye mkanganyiko (Utata), upande wa utetezi (washtakiwa), walisema, ushahidi wa PW4 na PW6 ambao unaonesha kwamba Mwalimu Harieth hakuja na pochi shuleni hauendani na maelezo yao waliyotoa polisi (Vielelezo D2 na D3) hivyo kuufanya ushahidi huo uwe wa uongo.
Wakasema, hao mashahidi wamekana kile walichosema kituo cha polisi, hii inawafanya kuwa waongo na wasioaminika.
Kuhusu kengele, utetezi upande wa washtakiwa waliwasilisha kuwa, PW8 hakusikia kengele nyingi Kama ilivyodaiwa na PW4 and PW6 hii inawafanya kuwa waongo na wasioaminika.
Wakaendelea kusema kwamba, PW4 ni mwongo kwa sababu ushahidi wake unahitilafiana na ule wa Daktari kwenye kipengele cha kutolewa kucha.
Upande wa utetezi ukaialika mahakama kutazama kwamba ushahidi wa PW4 na PW6 Unahitilafiana na ule wa PW8 kuhusu eneo ambapo fimbo za Mwalimu Harieth zilichapwa.
Wakasema, wakati PW8 alisema kwamba fimbo zilichapwa matakoni, PW4 na PW6 wakasema kwamba, Mwalimu Harieth alimchapa Sperius mikononi. Hii inawafanya PW4 and PW6 kuwa waongo na wasioaminika
Upande wa Mashtaka (Jamhuri) ukiwakilishwa na Mr. Hashimu Ngole, PSA (Wakili mkuu wa Serikali), wakasema kwamba neno (kirai) BEYOND REASONABLE DOUBT (Iliyothibitishwa pasipo na shaka yoyote) sharti itafsiriwe vizuri ipasavyo (properly).
Akailekeza Mahakama kwenye kesi ya Magendo Paul and Another v R [1993] TLR 125, ambayo (kesi hii) ilifuata maamuzi ya House of Lords (Mahakama ya juu kuliko zote Uingereza) katika kesi ya Millar v Minister of Pensions ambapo (Judge) Lord Denning alinukuliwa akisema
Sheria itashindwa kuilinda jamii, kama Mahakama itaruhusu tofauti ndogo ndogo zichukue nafasi ya haki.
Akasema kwamba, kutofautiana huwa kupo mara zote kwenye kesi, cha muhimu ni kuchunguza, Je! hizo tofauti zinafika kwenye kiini au mzizi wa kesi au la!
Mr. Hashimu Ngole akawasilisha kwamba, mzizi mkuu kwenye kesi iliyopo Mahakamani ni kupigwa na kifo kilichotokana na kupigwa huko. Hivyo vipengele vingine ni vitu vidogo vidogo tu. Alisema.
Upande wa Mashtaka (Jamhuri) uliwasilisha kuwa, mashahidi wake walikuwa wazi kabisa na thabiti (very specific and firm) kuhusu namna marehemu alivyopigwa na kufariki.
Akiongelea maelezo yaliyotolewa polisi, PSA (Wakili mkuu wa Serikali), alisema kwamba maelezo yanayotolewa polisi na mtuhumiwa sio ushahidi (police statements are not evidence), hivyo yasiingizwe kwenye kesi kuichanganya Mahakama. Na Pia hayo (maelezo) sio sehemu ya ushahidi wao.
Isitoshe, maelezo hayo hayaoneshi kama yalisomwa kwa mashahidi (baada ya kuandikwa).
Akaendelea kuwasilisha kwamba, mashahidi wake wamekana kuhusu kutoa maelezo kama hayo kituo cha polisi Wala
Hawakutoa maelezo mbele ya PW9.
The Principal State Attorney (Wakili mkuu wa Serikali), akasema kwamba, haoni uzito wa huo utata (mkanganyiko) kati ya PW5 and PW4 kuhusu kucha kwa sababu suala sio kwamba kucha haikutoka, ila suala au hoja ni kwamba Bikari ilitumika kumwadhibu mwanafunzi.
Aliuchukulia huo mkanganyiko (utata) kama kitu kidogo na akaiomba Mahakama iupuuze.
Akanukuu kesi ya Marando Slaa Hofu and 3 others v R CAT Criminal Appeal No.246 of 2011, Chrisant John v R CAT Criminal Appeal No. 313 of 2015, Elia Nshambwa Shapwata and another v R CAT Criminal
Appeal No. 92 2007, Edson Simon Mwombeki v R CAT Criminal Appeal No. 94 of 2016, Lusungu Duwe v R CAT Criminal Appeal No.76 of 2014 na R v
Golda (1960) I WLR 1169 Kuunga mkono hoja kwamba, mkanganyiko (utata) mdogo unatakiwa kupuuzwa
Mr. Ngole akairejesha Mahakama kwenye kesi ya R v Golkadas Karia (1951) EACA 211 kuhusu doctrine of common intention (nia moja ya kutimiza kusudio lisilo halali).
Huku akirejea kesi hiyo, akasema kwamba, (common intention) sio lazima kwenye kila kesi, kwamba lazima watu wawili wakutane na kukubaliana kufanya uhalifu. Maafikiano ya kufanya uhalifu yanaweza kuonekana kutokana na vitendo.
Na kwa mtazamo wake, vitendo vya mtuhumiwa namba moja na mtuhumiwa namba mbili, kwenye hii kesi, inaonesha kuwa, walikuwa na dhamira au nia moja (common plan) ya kumuua Sperius.
Anasema kwamba, mtuhumiwa (mshitakiwa) namba mbili (Mwalimu Harieth) aliyakataa maneno ya wanafunzi kwamba Sperius hakuwa na tabia ya wizi.
Mwalimu Harieth aliwapuuza wanafunzi na kuendelea kumpiga Sperius na mwisho kabisa akamkabidhi Sperius kwa Mwalimu Respecius, ambaye alimpiga mpaka akafa.
Kwake yeye, (Wakili mkuu wa Serikali, Mr. Ngole), hii inaashiria kwamba, wahalifu hao wawili walikuwa na nia moja ya kumwua mwanafunzi.
Mr. Ngole akaendelea zaidi na kuiambia Mahakama kwamba, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba Watuhumiwa wameongea uongo ili kujitetea.
Akasema kwamba, kwa kuwa Watuhumiwa hawana jukumu la kuthibitisha unyofu wao (kutokuwa na hatia kwao), ila kama wakisema uongo, msimamo wa kisheria ni kuwa, uongo wao unaithibitisha kesi ya Jamhuri.
Akitoa mfano, alisema kwamba, mtuhumiwa namba mbili (Mwalimu Harieth) alidanganya pale aliposema kwamba hajampiga marehemu (Sperius) wala kutoka nje ya shule.
Akaielekeza Mahakama kwenye kesi ya Pascal mwita and another v R [1993]TLR 295 na Musa Timotheo and another v R [1993] TLR 125 kisha akaialika Mahakama itamke kwamba huo uongo wa Watuhumiwa unaithibitisha kesi ya Jamhuri.
Na kuhusu Nia ya uwovu (malice aforethought), Mr. Ngole aliirejesha Mahakama kwenye kifungu 200 cha sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code), kesi ya Chrisant John na kesi ya Enock Kipela v R CAT Criminal Appeal No. 150 of 1994.
Upande wa Mashtaka ukawasilisha kwamba, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba Mwalimu Respicius alimpiga mwanafunzi (Sperius) mno, na akaongezea kwamba, namna kupigwa huko kulivyofanywa kuliashiria kwamba alidhamiria kumwua Sperius.
Akaielekeza Mahakama kwenye Education Circular (sheria) ambayo inataja fimbo nne tu, kisha akaendelea kusema kwamba, marehemu alipigwa fimbo nyingi bila ushahidi wa kuiba pochi.
Akaikataa hoja ya upande wa utetezi kwamba Mwalimu Respicius alikuwa na mamlaka kutoka baraza la shule kuchapa zaidi ya fimbo nne, akidai kwamba, baraza halikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.
Akaiomba Mahakama ikubali kuwa, Jamhuri imethibitisha kesi yake pasipo na shaka, (beyond reasonable doubts) dhidi ya Watuhumiwa wote hivyo Mahakama iwatie hatiani kama walivyoshtakiwa.
Waheshimiwa wazee wa baraza (assessors/Wasaidizi wa Jaji) wawili walishawishiwa na ushahidi kama ulivyoainishwa hapo juu pamoja na sheria husika, kwa umakini kabla hawajaulizwa kutoa maoni yao.
assessors wawili wakawatia hatiani kwa mauaji, Watuhumiwa wote wawili.
(JUDGE ANAENDELEA KUONGEA)
Wakaniambia kwamba, kulikuwa na ushahidi mzuri unaoonyesha kwamba Sperius alikufa kutokana na kupigwa na Mwalimu Respicius.
Wakaendelea kusema kwamba, Mwalimu Harieth naye aliweka mkono wake, kwa sababu yeye ndiye aliyemkabidhi Sperius kwa Mwalimu Respicius.
Pia (Mwalimu Harieth) aliukataa ushauri wa Mkuu wa shule msaidizi, kuhusu kufanya utafiti zaidi ili apate uhakika, na badala yake akampeleka Sperius kwa Mwalimu Respicius ambaye alimpiga Sperius mpaka akafa.
(Assessors) wakaongeza kuwa, Mwalimu Harieth hakuweza hata kujitokeza kuzuia kilichokuwa kinaendelea, anaonekana kuunga mkono kile kilichokuwa kinaendelea.
Assessor mmoja aliungana na wenzake katika maamuzi yao kuhusu Mwalimu
Respicius, ila akakataa kuunga mkono uamuzi wa kumtia hatiani Mwalimu
Harieth.
Alitoa wazo (hoja) kwamba, ushahidi wa kumpiga Sperius ambao unamhusisha Mwalimu Harieth unahitilafiana. Ambapo PW4 na PW6, walisema kwamba alimpiga Sperius mikononi. PW8 ambaye pia alikuwepo, akasema kwamba, alimchapa matakoni.
Amewapa fursa ya kumtilia shaka Mwalimu Harieth na kumkuta asiye na hatia.
(UCHAMBUZI/MTAZAMO WA JUDGE MWENYEWE RASMI):
Nilipata fursa ya kupitia ushahidi na maoni kwa makini.
Baada ya kupitia ushahidi na maoni ya pande zote kwa makini, Nimebaini kuwa, Fact 12 hazijakanwa
Moja, Watuhumiwa hawajakana kumjua marehemu. Wote walisema walikuwa wanamjua marehemu Sperius Eradius vizuri kabisa, mwanafunzi wa darasa la tano.
Pili, Watuhumiwa hawakukana kwamba, Sperius Eradius alikuwepo shuleni asubuhi katika afya njema
Tatu, Watuhumiwa hawakani kwamba, Sperius alituhumiwa kuiba pochi na
Nne, Watuhumiwa hawakani kwamba, Sperius Eradius kwa sasa amefariki.
Tano, Watuhumiwa hawakani kwamba, mwili wa Sperius Eradius ulikutwa na majeraha mbalimbali kuzunguka mwili mzima.
Sita, Mwalimu Harieth anakubali kwamba, alipokelewa na Wanafunzi ambao walichukua kikapu chake na vitu vingine alivyokuwa navyo
Saba, Mwalimu Harieth anakubali kwamba, alienda kwenye Ofsi ya Mkuu wa shule ambapo aliwakuta PW7 and PW8.
Nane, Mwalimu Harieth anakubali kwamba, aliwaambia PW7 and PW8 kuwa pochi yake ilikuwa haionekani.
Tisa, Mwalimu Harieth anakiri kwamba, alimshirikisha Mwalimu Respicius kulishughulikia tatizo kwa uwezo wake kama Mwalimu wa nidhamu.
Kumi, Mwalimu Respicius anakubali kwamba alimpokea mwanafunzi kutoka kwa Mwalimu Harieth na kumpiga fimbo sita
Kumi na moja, Mwalimu Respicius anakubali kwamba, alionwa na PW8, Mkuu wa shule msaidizi, akimpiga mwanafunzi.
Kumi na mbili, Mwalimu Respicius anakubali kwamba, alionwa na Mwanafunzi na PW2 and PW3 kando ya njia ambae (Sperius) hao (PW2 na PW3) walimchukua.
Maswali makubwa muhimu ya kutafutia ufumbuzi sasa ni haya,
Nani alisababisha majeraha mbalimbali kwa mwanafunzi (Sperius)?
Na alikuwa na dhamira (nia) gani?
Haya maswali yatajibiwa kwa ushahidi.
Ushahidi wa PW4, PW6 and PW8 unaonesha kuwa mwanafunzi (Sperius) alipigwa fimbo tatu kutoka kwa Mwalimu Harieth (akitumia fimbo za kawaida za shule) kabla hajakabidhiwa kwa Mwalimu Respicius ambaye alimpiga mno kuanzia 8:00 AM mpaka 11:00 PM.
Zaidi, Ushahidi unaonyesha kwamba, (Mwalimu Respicius) alitumia Fimbo za kawaida za shule, lakini baadaye akabadili na kutumia kipande cha ukuni. Na kwamba alimvua kaptura zake na viatu kabla ya kumpiga.
Inaonekana zaidi kwamba, alimpigia staff room na maeneo mbalimbali nje ya Ofsi.
Alimpiga (Sperius) mikononi, miguuni, mgongoni, shingoni na kichwani.
Pia alitumia Bikari kuchoma kwenye kidole cha Sperius.
Huu ushahidi unaendana na taarifa ya uchunguzi ya Dr. Kahima, PW5 na unaungwa mkono pia na ushahidi wa Dr. Otieno, DW3. Bado unazidi kuungwa mkono na Ushahidi wa PW2 na PW3 ambao wamlichukua mwanafunzi (Sperius) kando ya njia na kumpeleka hospitali
Kwa upande mwingine, Mwalimu Harieth alikana kumpiga Sperius.
Mwalimu Respecius alikubali kumpiga Sperius ila akasema kwamba, ilikuwa kidogo, viboko vitatu vya kawaida tu.
Sasa nani mkweli?
Nilichukua muda kupitia ushahidi kwenye kipengele cha kupigwa, na azimio (nia) ya kupiga, kwa umakini.
Nikiwa nafanya hivyo, Nikarejea kauli ya Kibiblia ya Pontio Pilato, wakati aliposema, Ukweli ni Kitu gani? (Meaning, what do we mean by the truth?)
Hakuwa anajua maana ya Ukweli na hilo lilikuwa ni tatizo katika kuamua kesi iliyokuwa mbele yake.
Mimi sina tatizo kama Hilo hapa kwangu.
Tatizo langu ni hili; Ni kwa nini watu hawataki kusema ukweli Mahakamani Hata kwa vitu vilivyo wazi kabisa?
(My problem is this; why is it that people do not want to say the truth in court
even on obvious things?)
Kila anayekuja Mahakamani anasema, “Sio kweli Mheshimiwa”, (meaning it is not true your honour). Kwa nini?
Nikavuta pumzi na kuwaza sana kuhusu hilo.
Kisha nikagundua ugumu wa kuwa Jaji na Hakimu. Ni kazi inayotaka akili itulie.
na kujitolea kwa ajili ya haki na msaada kutoka kwa Mungu.
(It is a job which needs peace of mind, commitment towards justice and assistance from God.)
Inawataka (Majaji) kuwa makini sana kwenye kutathmini (kuchambua) ushahidi, vinginevyo watashindwa na hatari ya kupotezwa (kudanganywa)
Kwa hiyo nitajaribu kuwa makini sana katika kuuchambua ushahidi wa kila Shahidi ambaye amefika hapa Mahakamani.
Nitaanza kuongelea uaminifu wa mashahidi.
‘Bahati nzuri hiki sio kipengele kisichokuwa na mifano (authorities)’ [mfano kesi za nyuma]. Emphasis added.
Tuna mifano mingi. (We have many authorities.) Baadhi imeshanukuliwa kwangu na Mawakili.
Kwenye kesi ya Edson Simon Mwombeki (supra), mahakama ya rufaa ilifuata uamuzi wake wa awali wa kwenye kesi ya Goodluck Kyando V.R, [2006] TLR 363.
Na ilikuwa na haya ya kusema; Kila Shahidi ana haki ya kukubalika na lazima aaminiwe na Ushahidi wake ukubaliwe, labda kama kuna mantiki na sababu njema ya kutomwamini Shahidi (Imetafsiriwa.)
(“Every witness is entitled to credence and must be believed and his testimony accepted unless there are good and cogent reasons for not believing a witness”)
Mahakama (ya rufaa) ikaendelea kusema yafuatayo katika ukurasa wa 16. Ikasema kwamba;-
Sababu nzuri za kutomwamini Shahidi ni pamoja na ukweli kwamba, Shahidi ametoa ushahidi usio yakinifu (improbable) au usio na mashiko (implausible) au ushahidi umehitilafiana kwenye sehemu muhimu (materially contradicted) na Shahidi au mashahidi wengine. Soma kesi ya Mathias Bunda/a V. R, Criminal Appeal No. 62 of 2004).
Kwa maneno mengine, lazima kuwepo na sababu nzuri (njema) kabla ya kuukataa ushahidi wa Shahidi.
Sababu hizo nzuri zinazoweza kupelekea Mahakama iukatae ushuhuda wa Shahidi ni zifuatazo;
Pale ambapo Shahidi anaongea jambo au kitu ambacho hakina maana (unreasonable), kitu ambacho hakiwezekani kabisa (not probable) katika mazingira ya kesi husika.
(Anaongea) kitu ambacho kinadhoofisha (defeat) au hakina mantiki (logic). Au kitu ambacho kinapingana au kuhitilafiana na ushahidi uliotolewa na Mashahidi wengine.
Mwingine anaweza kuuliza swali, vipi kuhusu kuhitilafiana (utata) kwenye ushahidi?
Je! Inawezekana kusema kwamba, pale ambapo kuna utata na/au kuhitilafiana (kutofautiana) katika ushahidi, ushahidi wa Shahidi lazima utiliwe shaka na kukataliwa?
Ikizungumza kuhusu utata na kuhitilafiana (kwa ushahidi), mahakama ya rufaa ilikuwa na haya ya kusema kwenye kesi ya Chricant John (supra) ukurasa wa 19-20
Kwamba, ‘Utata (kutofautiana) kwa shahidi mmoja yeyote au miongoni mwa mashahidi hakuwezi kukwepeka au kuzuilika kwenye kesi yeyote ile. Japo, katika kuzingatia aina, idadi na madhara ya utata (kutofautiana), lazima kila mara, ikumbukwe kwamba, mashahidi hawawezi kila muda kukumbuka kwa kina maelezo ya kila kitu kilichotokea.
(It must always be remembered that witnesses do not always make a blow by blow mental recording of an incidence.)
Kwa hiyo kutofautiana kusichambuliwe bila kuwekwa kwenye muktadha wake sahihi, kama jitihada za kutafuta uzito wake. Ili kujua, kama (kutofautiana) kunaenda mpaka kwenye mzizi wa kesi au la, ama badala yake unaharibu uaminifu wa wahusika kwenye kesi.
Mahakama ilifuata maamuzi yake ya awali kwenye kesi ya Elia Nshamba Shapwata and Another (supra), ambapo ilisema kwamba;
Katika kuchambua utofauti (discrepancies), contradictions (utata) na maneno yaliyoachwa (omissions), haipendezi kwa Mahakama kuchukua sentensi kadhaa na kuzitumia peke yake huku wamezitenganisha mbali na maelezo mengine yaliyobaki
Mahakama sharti iamue, Je! huo utofauti na utata ni kidogo sana (minor) au unaingia kabisa kwenye kiini au mzizi wa kesi?
Mahakama ya rufaa iliweka bayana kwamba kutofautiana (kuhitilafiana) kidogo tu (minor contradictions) ambako hakufiki kwenye kiini au mzizi wa kesi kunaweza kupuuzwa.
Lakini pale mbapo utata au kutofautiana kunafika mpaka kwenye mzizi au kiini cha kesi, kutapelekea kukosa imani na Shahidi na ushahidi wake.
Uchunguzi kuhusu kutofautiana (Utata wa ushahidi) lazima viende sanjari (pamoja) na uchunguzi wa mwenendo wa Shahidi.
Viwili hivyo, vina uhusiano wa karibu.
Mtindo wa kuchunguza mwenendo wa mashahidi unaweza kutofautiana kutoka Jaji au Hakimu mmoja na mwingine.
Lakini kwa mtazamo wangu (Judge), uchunguzi huu unaweza kufanyika kama ifuatavyo;
Uchunguzi kwa njia ya kupima namna ambavyo Shahidi anaonekana (mwonekano wa Shahidi) kizimbani.
Namna anavyoongea na kujibu maswali aliyoulizwa na Wakili wake wakati wa examination in chief na namna anavyojibu maswali wakati wa cross examination.
Kama Shahidi hawezi kuongea sawasawa, anashindwa kusimama imara kwenye sehemu muhimu (key areas), ana uso wa kutetemeka, anashika kichwa kama vile anataka kukumbuka hadithi aliyoambiwa na mtu fulani.
Hicho kinaweza kuwa kiashiria kwamba, mwenendo wa Shahidi huyo unajenga maswali.
Lakini kama Shahidi anasimulia maelezo thabiti kabisa na anazidi kutetea msimamo wake kwa nguvu zote, wakati wa cross
examination, hatetemeki (isipokuwa kwa ile kawaida ya kuogopa Mahakama kwa baadhi ya watu), pia yuko tayari kuomba radhi pale ambapo hakumbuki vizuri kitu fulani.
Huyo ndiye Shahidi ambaye mwenendo wake hautakiwi kutiliwa mashaka. Katika kesi nyingi, huyu ndiye Shahidi wa ukweli.
Nilipata muda kuwachambua mashahidi wote kwa makini. Sikuweza kutilia mashaka mwenendo wa PW2, PW3, PW4, PW5, PW6 and PW8.
Wote walionekana imara na thabiti. Ushahidi wao ulikuwa na mpangilio wa mantiki na unashabihiana wote katika vipengele vyote muhimu.
Sikuweza kugundua hisia zozote za uongo katika ushuhuda wao kwenye kipengele muhimu cha kupigwa.
Nawaona kama watu waliokuwa hawasemi kitu, isipokuwa ukweli tu.
Kwa upande mwingine, mwenendo wa DW1 (Mwalimu Respecius) na DW2 (Mwalimu Harieth) ulionekana kuwa hafifu kilipofika kipengele cha kupigwa kwa mwanafunzi. Walionekana kama kuna kitu wanaficha.
Hawakuwa wazi. Wote walikuwa wanatetemeka wakati walipokana kumpiga mwanafunzi (Sperius)
Ushahidi wao haukuwa na mantiki katika hatua fulani.
Haukuwa unaaminika, mathalani, kuamini maneno ya DW1 (Mwalimu Respecius) kwamba, alimpiga marehemu fimbo ndogo sita tu, wakati Shahidi wake DW3 (Daktari) ambaye aliufanyia uchunguzi (vipimo) mwili wa marehemu masaa 2.30 baadae, alisema kwamba kulikuwa na majeraha mbalimbali.
DW1 (Mwalimu Respecius) hakusema nani alieongezea kipigo. Ikiwa mwanafunzi (Sperius) alipigwa kidogo tu shuleni kama (Mwalimu Respecius) anavyotaka tuamini, nani tena alikuja hapo katikati na kuongeza majeraha mbalimbali ambayo yalionekana na Shahidi wake Dr. Otieno?
Je, Inawezekana kusema kwamba, mama yake (Sperius) PW2 na PW3 ndio waliompiga wakiwa njiani kwenda hospitali?
Na ikiwa Sperius alikabidhiwa kwa mama yake akiwa katika hali nzuri kama DW1 (Mwalimu Respecius) anavyotaka tuamini, ni kwa nini mama yake alipiga yowe ambalo lilivuta watu wengi?
Na kama alipigwa kidogo, kwa nini alikufa punde tu baada ya kufika hospitali?
Maswali haya hayana majibu! Yanaenda kuharibu mwenendo wa DW1 (Mwalimu Respecius). Yameuhafifisha ushahidi wake. Hii pia inamaanisha kwamba, aliongea uongo wakati amekula kiapo.
Uongo wake unaithibitisha kesi ya Jamhuri. (Tazama kesi ya Felix Lucas Kisinyala v. R CAT Criminal Appeal No. 129 of 2002 na Salum Yusufu Liundi v. R CAT Criminal Appeal No.26 of 1984).
Kwa hiyo, ni hitimisho langu kuwa, Mwalimu Respicius ndiye aliyempiga mwanafunzi (Sperius) na kwamba alimpiga kwa namna ilivyoelezewa na PW4, PW6 and PW8.
Ni hitimisho langu pia kwamba, majeraha yaliyoonwa na PW3, PW5 na DW3 yalisababishwa na DW1 (Mwalimu Respicius).
Mwenendo wa DW2 (Mwalimu Harieth) haukuwa pia mzuri. Naye alisema uongo, usiohitajika wakati mwingine. (She also spoke lies, sometimes very uncecessary).
Alidanganya Pale aliposema kwamba hakuondoka shuleni siku hiyo asubuhi, na kwamba alipitiliza kwenda darasa la pili kusimamia Mitihani.”
Uso wake haukuweza kuakisi (kuendana na) maneno yake kizimbani wakati akiwa anayaongea hayo.
Sauti yake ilipungua (fifia), kumaanisha kwamba, alikuwa anapingana na dhamira yake.
Ukweli ambao uko wazi, ni kwamba aliondoka kwa muda mfupi hiyo asubuhi.
Vilevile alifanya jitihada kadhaa kutafuta pochi na wanafunzi kama ilivyoainishwa na PW4 and PW6.
Uongo wake kwenye kipengele hiki, unaithibitisha kesi ya upande wa Mashtaka (Jamhuri), kwamba, alienda na wanafunzi kwa muda fulani kutafuta pochi huku akiwaacha wanafunzi wa darasa la pili na Mwalimu Alipensia.
Vipi kuhusu upigaji kwa upande wa Mwalimu Harieth?
Nina ushahidi wa PW4 na PW6 ambao walisema kwamba, Mwalimu Harieth alimpiga mwanafunzi (Sperius) fimbo tatu mikononi, ndani ya ofsi, akitumia fimbo za kawaida
Pia nina ushahidi kutoka kwa PW8 ambaye alisema kwamba, (Mwalimu Harieth) alichapa fimbo tatu matakoni.
Swali sasa ni Je! Huu mkanganyiko (utofauti) ni mdogo au mkubwa (muhimu)?
Nimeufkria sana kwa makini. Nadhani huu ni utofauti wa msingi (muhimu) kwa sababu unafika mpaka kwenye kiini/mzizi wa kesi.
Upigaji, sio kama utofauti wa kwenye pochi, huu (utofauti kwenye upigaji) unaenda mpaka kwenye mzizi wa kesi.
Upo uwezekano mkubwa sana kwamba mashahidi waliokuwepo nje hawakuweza kuona vizuri, kutokana na umbali (hadi ndani ya ofsi) lakini nadhani huu utofauti (utata) usichukuliwe kiwepesi.
Inaonekana kwamba, hakuna ushahidi mzuri (wa kutosha) kutoka upande wa Mashtaka (Jamhuri) kuthibitisha pasipo na shaka kwamba Mwalimu Harieth alimchapa marehemu viboko vitatu
Nakubaliana na upande wa utetezi na mmoja kati ya wazee wa baraza (assessors) kwamba, ushahidi kwenye kipengele hiki, hauaminiki
Nitaendelea kuchambua utata/tofauti zingine.
Utata kwenye pochi na kengele haufiki kwenye mzizi wa kesi. Huu nauchukulia kama mdogo sana hivyo naupuuza.
Utata kuhusu kuondolewa kucha, unagusa kipengele cha kupiga, lakini unaonekana kusababishwa na umbali na mshtuko.
PW4 alikuwa anamwangalia Mwalimu (Respicius) kutokea nje ya ofsi, na alikuwa katika hali ya mshtuko baada ya kuona kilichokuwa kinaendelea na baada ya yeye mwenyewe kupigwa (wakati ameambiwa alete ukuni fulani yeye akaleta fimbo nyingine). Emphasis added.
Anaweza kuwa aliona damu baadhi zinatoka kidoleni kutokana na kutumika kwa Bikari kisha akafkri kwamba kucha ilikuwa inatolewa
Hicho ni kitendo cha kawaida ambacho kinaweza kutokea kwa Shahidi yeyote hususani pale ambapo yuko kwenye mshituko kama ilivyokuwa kwenye hii kesi.
Nauchukulia utofauti huo kama mdogo sana, kwa sababu hiyo naupuuza.
Utata kutokana na maelezo yaliyotolewa kituo cha polisi, nao hauwezi kutiliwa maanani kwa sababu tatu;
Moja, ulikuwa unahusu pochi na sio kupiga.
Mbili, maelezo hayo hayaoneshi kama yalisomwa kwa mashahidi baada ya kuyachukua. Na
Tatu, kama ilivyowasilishwa kiusahihi kabisa na Wakili mkuu wa Serikali, maelezo yanayotolewa polisi sio ushahidi.
Hayawezi kuushinda ushahidi uliotolewa kwa kiapo.
Kazi yake ni kuondoa imani na Shahidi, ambapo kwa mtazamo wangu yameshindwa kufanya hivyo, kutokana na uthabiti na mpangilio wa maelezo uliotolewa na PW4 and PW6.
Hilo limetajwa na limeisha.
Ngoja sasa nielekee kweye kuchambua Kanuni ya adhabu ya viboko (Corporal Punishment Regulations made under Section 60 (o) of the Education Act, Cap. 353 R.E. 2002.
Nitaziandika kwa kirefu kurahisisha usomaji. (Kanuni hizo) zinasomeka kama ifuatavyo; (Anaongea Muheshimiwa Jaji)
“THE EDUCATION (CORPORAL PUNISHMENT) REGULATIONS, GN.
294 OF 2002.”
1. Kanuni hizi zitaitwa the Education (Corporal Punishment) Regulations.
(These regulations may be cited as the Education (Corporal Punishment) Regulations.)
2. Katika kanuni hizi, labda kama mazingira yanaruhusu vinginevyo, “Adhabu ya viboko” inamaanisha adhabu kwa kumchapa mwanafunzi kwenye mikono yake au kwenye matako huku akiwa amevaa nguo zake za siku zote, kwa kutumia fimbo nyepesi na inayonyumbulika, lakini (adhabu ya viboko) haijumuishi kumchapa mtoto na kifaa chochote au kuchapa sehemu nyingine yoyote ya mwili.
“(Corporal punishment” means punishment by striking a pupil on his hand or on his normally clothed buttocks with a light, flexible stick but excludes striking a child with any other instrument or on any other part of the body).
“Mkuu wa shule” inamaanisha Mwalimu yeyote aliyeteuliwa na mamlaka husika kuwa msimamizi wa shule ya msingi au sekondari na inajumuisha mtu yeyote ambaye anamwachia majukumu yake
“(head of school”* means any teacher appointed by the relevant authority to be in-charge of primary or secondary schools and includes any person to whom he delegates his duties.)
“Mwanafunzi” inamaanisha mtoto yeyote aliyeandikishwa katika shule yeyote ya msingi au sekondari lakini haijumuishi mtoto aliyeandikishwa chekechea au chuo cha ualimu
(“Pupil” means any child enrolled in any primary or secondary school but does not include a child enrolled in a pre-primary school or teachers' college)
“Mamlaka ya shule” inamaanisha waalimu wote ila haijumuishi wahusika (wanachama) wengine kwenye ofsi.
“(school authority” means all teachers and does not include other members of staff.)”
3-(1). Adhabu ya viboko inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama kwa makosa makubwa yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia shule heshima.
(Corporal punishment may be administered for serious breaches of school discipline or for grave offences committed whether inside or outside the school which are deemed by the
school authority to have brought or are capable of bringing the school into disrepute.)
(2) Adhabu ya viboko iwe na uwiano, sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.
(Corporal punishment shall be reasonable having regard to the gravity of offence, age, sex and health of the pupils and
shall not exceed four strokes on any occasion.)
4. (1) Mkuu wa shule kwa busara zake, anaweza kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake katika maandishi kwa Mwalimu yeyote aliyechaguliwa kwa umakini mkubwa kutoka ofsini kwake. Na huyo Mwalimu aliyechaguliwa atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika
(The head of the school in his discretion may administer corporal punishment or may delegate his authority in writing to a carefully selected member of his teaching staff provided that the authorized member of staff may act only with the approval of the head of the school on each occasion with corporal punishment is administered.)
(2) Mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike, ambapo ikitokea hivyo, Mkuu wa shule anaweza mwenyewe kutoa adhabu au kumruhusu kwa njia ya maandishi Mwalimu wa kiume kutoa adhabu ya viboko.
(A female pupil may only receive corporal punishment from a female teacher except where there is no female teacher at the school in which case the head of school may himself administer corporal punishment or authorize in writing a male teacher to administer corporal punishment.)
5. -(1) kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu.
(On every occasion when corporal punishment is administered it shall be recorded in writing in a book kept for this purpose and such record shall state in each instance the name of the pupil, the offence or breach of discipline, the number of strokes and the name of the teacher who administered the punishment.)
(2) Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na mkuu wa shule.
(Every entry in the book shall be made and signed by the head of the school.)
6. Kukataa kukubali adhabu ya viboko kwa Mwanafunzi au mzazi kwa niaba yake,
kunaweza kupelekea kusimamishwa masomo kwa mwanafunzi, kwa mujibu wa kanuni za kusimamisha na kufukuza wanafunzi shuleni za mwaka, 2002.
(A refusal to accept corporal punishment either by a pupil or by a parent on the pupil's behalf may lead to the exclusion of the pupil in accordance to the Expulsion and Exclusion of Pupils from Schools
Regulations, 2002.)
7. Hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kupitia sheria ya Tume ya utumishi wa waalimu ya mwaka 1989, dhidi ya Mkuu wa shule au mamlaka ya shule, kama utaratibu wa kutoa Adhabu ya viboko umekiukwa
(A disciplinary action shall be instituted under the Teachers Service Commission Act, 1989 as against a head of school or school authority if the administration of corporal punishment is violated)
8. (Revokes the Education (Corporal Punishment Regulations.)
Kanuni zinaonyesha mambo muhimu yafuatayo;
Moja, Adhabu ya viboko inatolewa kutokana na utovu wa nidhamu shuleni uliokithiri ama kwa makosa makubwa (grave offences)
Pili, Inatolewa na Mkuu wa shule au
Mwalimu yeyote aliyechaguliwa kwa umakini mkubwa kutoka ofsini, ambaye ameruhusiwa na Mkuu wa shule kwa njia ya maandishi.
Tatu, (Adhabu ya viboko) Inatolewa kwa kumchapa mwanafunzi kwenye mikono yake au kwenye matako huku akiwa amevaa nguo zake za siku zote, kwa kutumia fimbo nyepesi na inayonyumbulika, lakini haijumuishi kumchapa mtoto na kifaa chochote au kuchapa sehemu nyingine yoyote ya mwili.
Nne, lazima iwe na uwiano, sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya wanafunzi na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.
Tano, sharti iingizwe kwenye kumbukumbu kwa njia ya maandishi, katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, na kumbukumbu hiyo sharti itaje kwa kila tukio, jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu.
Sita, Mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike, ambapo ikitokea hivyo, Mkuu wa shule anaweza mwenyewe kutoa adhabu au kumruhusu kwa njia ya maandishi Mwalimu wa kiume kutoa adhabu ya viboko.
Saba, Mwanafunzi ambaye anagoma kupewa Adhabu ya viboko anaweza kufukuzwa shuleni
Na nane, Mwalimu ambaye atashindwa kuenenda sawasawa na hizi kanuni, anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Turudi kwenye kesi yetu sasa, Hakuna shaka kwamba, wizi lilikuwa ni kosa kubwa. Ila ushahidi unaonyesha kwamba, hapakuwa na uthibitisho kwamba Sperius ndie alihusika kuiba (pochi).
Wanafunzi watatu tu walisema kwamba, Sperius ndiye alikuwa amechukua pochi. Wengi walisema sio yeye, na wakaongezea kwamba (Sperius) hakuwa na tabia kama hiyo.
PW8 alimtahadharisha Mwalimu
Harieth kuhusu hicho kitu. Hakuamini kwamba Sperius ndiye alikuwa ameichukua.
Pamoja na hayo yote, Sperius alipigwa kama kibaka (street hard core criminal). Alipigwa mno! Maskini. (He was beaten heavily! Poor boy!)
Mwalimu Respicius hakuwa na ruhusa kutoa Adhabu ya viboko. Hakupata ridhaa ya PW7 au PW8 (Mkuu wa shule na mkuu msaidizi)
Aliendelea kumpiga mwanafunzi (Sperius) pamoja na kuingilia kati kwa bosi wake, PW8. Akionesha tabia yake halisi.
Mwalimu Respicius hakutumia fimbo za kawaida za siku zote, kuchapa viboko vinne kwenye matako kama ilivyoelekezwa na sheria.
Alitumia kipande cha ukuni kumpiga mwanafunzi (Sperius) huku akirudia rudia.
Bado hakukumbuka pia kunakili kumbukumbu ya Adhabu kwenye kitabu maalum.
Hii inaashiria kwamba, kilichofanywa na Mwalimu Respecius sio tu jinai, bali pia ni uvunjifu wa Kanuni za Elimu (Education Regulations).
Mwisho nitaenda kuchambua nia ovu (Malice) na nia moja ya kutenda kusudio lisilo halali (common intention).
Nitaanza na nia ovu (malice), Dhamira (nia) ya kuua.
Kesi kuu ya kutuongoza hapa ni maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Enock kipela v. Republic, (supra).
Mahakama ya rufaa ilisema kwamba;
Mara nyingi mshambuliaji hawezi kutangaza nia yake ya kuua au kusababisha majeraha ya mwili. Kutambua kama alikuwa amedhamiria au la, lazima uangalie mazingira kadhaa, yakiwemo yafuatayo;
Usually an attacker will not declare his intention to cause death or grievous bodily harm. Whether or not he had that intention must be ascertained from various factors, including the following:
1: Aina na ukubwa wa silaha, kama ipo, iliyotumika katika shambulizi. (The type and size of the weapon, if any, used in the attack)
(2) Kiwango cha nguvu iliyotumiwa kwenye shambulizi. (The amount of force applied in the assault;
(3) Sehemu za mwili ambapo pigo au shambulizi lilielekezwa au kupigwa (The part or parts of the body the blow were directed at or inflicted on)
(4) Idadi ya mapigo (shambulizi), japo pigo au shambulizi moja, itategemea na kilichotokea kwenye kesi husika, linaweza kutosha kabisa (kuonesha dhamira).
(The number of blows though one blow may, depending on the facts of a particular
case, be sufficient for this purpose)
(5) Aina ya madhara yaliyopelekewa (kusababishwa).
(The kind of injuries inflicted).
(6) Kauli au Maneno ya mshambuliaji, kama yapo, ambayo aliyatoa kabla, wakati na baada ya mauaji. (The attackers utterances, if any, made before, during or after the killing) na
(7) Mwenendo wa mshambuliaji kabla na baada ya mauaji (The conduct of the attacker before or after the killing).
Tazama pia kesi ya Saidi Ali Matola @ Chumila v. Republic, CAT Criminal Appeal
No.129 of 2005.
Ushahidi unaonyesha kwamba Mwalimu Respicius alitumia fimbo za kawaida, lakini akabadilisha baadae na kuanza kutumia kuni
Mazingira hayaoneshi kwamba (Mwalimu Respicius) alitumia nguvu kubwa, ila inaonesha kwamba alimpiga mwanafunzi (Sperius) mara nyingi (kwa kurudia rudia) huku akitamka maneno makali.
Alitumia fimbo na kuni (kupiga) mwili mzima - Miguuni, mikononi, mbavuni, mgongoni, mabegani, usoni, shingoni na kichwani.
Marehemu alipata alama (makovu) mwili mzima pamoja na majeraha makali
Ushahidi unaonyesha kwamba Mwalimu Respicius alitamka maneno yafuatayo wakati wa shambulizi; “Ngoja niwaonyeshe kazi ya jiwe” (literally meaning let me fix him properly.)
Kisha akaongezea kwamba, “nitakuwekea alama ambayo utamuonyesha hadi mjukuu”
Na wakati mwanafunzi alipoanguka chini, Mwalimu wa nidhamu (Mwalimu Respecius) alinukuliwa akisema; “Huu ni
usanii, hivi sivyo wanavyozimiaga”
Alisimama kwa muda kisha akaendelea na zoezi.
Tabia au mwenendo wa Mwalimu Respicius was that of a very rough and harsh teacher. (Mwalimu jeuri na katili sana).
Alitoa Adhabu kwa masaa matatu kwa mwanafunzi ambaye alikuwa nusu uchi na ambaye alikuwa akirudia rudia kusema kwamba hajachukua pochi.
Aliukataa ushauri wa Mkuu wa shule msaidizi ambaye alisitisha kupigwa.
Alimrudisha Mwalimu Harieth, wakati alipoomba waende wote na akaendelea na zoezi peke yake
Kisha akarudi shule na kuwaongopea waalimu kwamba amemkabidhi mwanafunzi (Sperius) kwa wazazi wake, akiwa salama kabisa
Alificha Ukweli kwamba, mwanafunzi (Sperius) alikuwa kwenye hali mbaya.
Na mwisho, wakati askari wamekuja shuleni, alikimbia na kwenda kujificha kwenye kichaka cha karibu.
Yote haya kwa mtazamo wangu, yanaonesha kwamba Mwalimu Respicius alidhamiria ama kumjeruhi au kumwondoa kabisa mwanafunzi (Sperius)
Alijua alichokuwa anakifanya na aliamua kukifanya mpaka mwisho.
Alikuwa na nia ovu yote inayohitajika kuwepo kwenye kesi ya mauaji. (He had the necessary malice needed in a murder case.)
Hoja yake ya kujitetea kwamba, alikuwa tu anamwadhibu mwanafunzi kawaida, Haikubaliki.
Vipi kuhusu Mwalimu Harieth?
Ushahidi unaonyesha kwamba Mwalimu Harieth alipoteza pochi yake.
Kisha akamshuku (kumuhisi) Sperius Eradius kuwa ndiye mwizi, ambaye alimkabidhi kwa Mwalimu wa nidhamu, kwa hatua zaidi.
Ushahidi unaonyesha pia kwamba, alienda huko na huku kutafuta pochi akisindikizwa na wanafunzi
Mbali na kwenda na kumkabidhi mwanafunzi (Sperius) kwa Mwalimu wa nidhamu (Mwalimu Respecius), hakuna ushahidi mwingine unaomuunganisha na upigaji ambao ulifuatia.
Apart from moving around and handling over the boy to the discipline master
there is no other evidence connecting her with the beatings which followed.
Kuna kiashiria cha kujizuia kama ilivyoainishwa na wazee wa baraza (assessors).
Kwamba hakuchukua hatua yotote kuzuia kupigwa (kwa Sperius). Hicho kiashiria kipo.
Lakini, hata hivyo, sidhani kwamba, kinatosha kuwa nia moja ya kutimiza kusudi lisilo halali (common intention) kama inavyomaanisha kwenye kifungu cha 23 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kwenye mazingira ya hii kesi.
Sioni uhusiano wowote kati yake.
Kwa hiyo ni hitimisho langu kuwa, hapakuwa na ushahidi mzuri kuhusu upigaji kwa upande wake au nia moja ya kutenda kusudio lisilo halali yenye uzito kumwuunganisha na kilichofanywa na DW1 (Mwalimu Respecius)
Na kama ilikuwepo nia yoyote, ilikuwa inalenga au inaishia kurudisha pochi yake na si kumwondoa kabisa mwanafunzi (Sperius)
Baada ya kusema na kumaliza hilo, Nahitimisha na kuamua kwamba, upande wa Mashtaka (Jamhuri) umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya mtuhumiwa namba mbili (Mwalimu Harieth)* kikamilifu kabisa pasipo na shaka, ambaye namkuta bila hatia na kumwachia huru.
Kesi dhidi ya mtuhumiwa namba moja Respicius Patrick @ Mutazangira ilithibitishwa kikamilifu pasipo shaka yoyote. Namkuta mtuhumiwa namba moja Respicius Patrick @ Mutazangira, kuwa na hatia ya mauaji kinyume cha kifungu namba 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 Iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, hivyo namtia hatiani kama ipasavyo.
L. M Mlacha.
Judge
6/3/2019
HUKUMU:
Kuna adhabu moja tu ya kosa la mauaji ambayo ni kunyongwa mpaka kufa.
(There is only one sentence for murder which is death by hanging).
Nakuhukumu wewe mtajwa RESPICUS PATRICK @ MUTAZANGIRA kunyongwa mpaka kufa.
I sentence you the said RESPICUS PATRICK @ MUTAZANGIRA to death by hanging.
Mahakama (Court):
L.M. Mlacha.
Judge
6/3/2019.
Haki ya kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa imefafanuliwa
(Right of Appeal to the Court of Appeal Explained).
L. M Mlacha
Judge
6/3/2019
MWISHO (WA KUTAFSRI).
Imetafsiriwa na Zakaria (0754575246)