kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,467
- 4,913
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Kama zilivo katiba za nchi nyingi duniani hasa zile zinazoendeshwa katika misingi ya kidemokrasia inatanabaisha wazi uwepo wa mihimili mitatu katika nchi, yaani Serikali, Bunge na mahakama, kati ya hiyo Mahakama ukiwa ndo muhimili uliopewa majukumu ya kutafasri sheria(ikiwemo katiba yenyewe maana nayo ni sheria).
Katika kutafasiri sheria mahakama imekuwa ikifanya mambo kadhaa wa kadhaa Kama vile kuzitamka baadhi ya sheria kuwa zipo kinyume na katiba au vipengele kadhaa vya katiba vinakiuka haki za binadamu na mikataba kadhaa wa kadhaa ya kimataifa N.K. na moja yaya mashuj katika harakati hizi za kupambana na sheria na vipengele vya katiba vilivyoonekana kuwa kandamizi basi ni the late Rev. Mtikila (R.I.P) kwa wale waliosoma sheria basi huyu ni moja ya watu lazima utakutana naye hasa kwenye somo la Katiba(Constitutional Law), hapo alipoenda Kambole mzee Mtikila yeye alishafika kitambo akipinga kipengele kinachozuia mgombea binafsi. Narudia tena R.I.P Reverend.
Naam, Reverend Mtikila!! Kwanini nimemkumbuka huyu jamaa? ni baada ya ya Leo kukutana na thread ikionesha kuwa my learned brother Jebra Kambole amefungua kesi kwenye Mahakama ya Haki za Binadamu ya Africa( African Court of Human Right) kupinga kipengele Cha katiba kinachokataza kupinga matokeo ya urais yakishakutangazwa. Mimi sitaki kuingia kwenye logic ya kwanini kipengele hicho kiwepo au kisiwepo kwenye katiba kwani hii ni more jurispudential au philosophical aspect hivyo kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake.
Kilichonisukuma kuja hapa jamvini ni namna ambavyo Leo tunawaharakati lukuki ambao kila siku Instagram, Twitter na Facebook account zao zimejaa malalamiko juu ya sheria wanazodai ni kandamizi zilizotungwa na Bunge au hata watu waliokamatwa kwa kwakuwa wamekiuka the so said tyranical laws na wengi wa Hawa ni wasomi wazuri na wengine ni wanasheria kabisa ambao wanajua haya mambo kuliko hata the late mzee Mtikila.
Ninachotaka kusema mzee Mtikila alitambua kuwa mahakama ndo chombo pekee kwa mujibu wa katiba chenye mamlaka ya kutafasiri sheria na alikitimia ipasavyo kuzichallenge sheria na vipengele vya katiba alivyoamini kuwa vilikuwa kandamizi na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa.
Kinachonishangaza wanaharakati wa Leo wamegeuza Instagram, Twitter na Facebook kuwa ndo mahakama zao, Zitto, Nape, Bashe, Maria Sarungi Julius Mtatiro na wengine wengi wanalamika huko, kibaya zaidi hata Rais wa Chama Cha Wanasheria(TLS) mwanamama Fatuma kalume naye analalamika huko. Hawa ni watu wanaofahamu wazi kuwa njia ya kisasa na ya busara ya kupambana na sheria za bunge zinazoonekana kandamizi ni kutumia Mahakama and nothing more, na hii ndo maana halisi ya ya mihimili ya dola ambayo inakamilisha kile kinachoitwa Check and Balance. ushahidi upo wa kutosha kuwa Jambo hili linawezekana, Reveland aliweza, Hawa kina Fatuma karume, Zitto, Maria Sarungi na wengine wanashindwa Nini hadi wanaishia kulia lia kwenye mitandao? Yes mtandaoni maana huko wanajijengea umaarufu na kwao umaarufu ni kitu Cha mhimu kuliko kile alichokifanya Mtikila ambacho mwisho wa siku kinawanufaisha watu wote.Badala ya kupambana na hizo sheria wanazoziona kandamizi watu wanapambana na matokeo, wanasubiri Abdul Nondo akamatwe wajaze mandishi kwenye account zao za mitandao, wanasubiri Mtatiro akamatwe wajaze mandishi kwenye account zao na sio kwenda kuomba mahakama kuzi declare sheria hizo kuwa kandamizi, yes! Mtandaoni! Hko wanajipatia umaarufu na kujijenga kisiasa.
Ndio maana nasema alichokifanya Jebra ni kutukumbusha namna pekee Bora ya kupambana na hicho tunachokiita unjust laws, na ujumbe huo uwafikie wote wanaoshinda mitandaoni kulalamika na kwa upana wake zimfikie mama/Bibi Fatuma Karume maaana amebeba dhamana kubwa katika hili badala ya kushinda mitandaoni akitoa mipasho atumie mda mwingine kuratibu mambo Kama haya anayoyafanya Jebla Kambole.
"The Court is there for some one who nocks the door" njia pekee ya kupinga sheria tunazodhami kuwa ni kandamizi ni kwa kwenda mahakamani na si mitandaoni!!
Asante Rev, asante brother Jebra kwa kutukumbusha.