LGE2024 Pwani: Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ataka CCM wasiwachukie Wapinzani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,160
5,505
1732687102962.png

MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutowachukia wagombea wa vyama vingine waliojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani wameshiriki kukamilisha Demokrasia.

Makamu huyo wa Rais ameyasema hayo alipokuwa akifunga kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani katika Viwanja vya Mailimoja Kibaha ambapo amesema kitendo cha kuwepo kwa vyama vingine kugombea kwenye uchaguzi huo kinaleta ushindani.

Amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla kwenda kuwachagua wagombea wa CCM ili waendeleze kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.

“Hawa wa vyama vingine wamekuja tuwashinde sisi hatuna huruma kwenye uchaguzi, wala hatuna urafiki likija swala la uchaguzi tupambanie kwanza kushinda halafu baadae ndio tutashiriki kwenye kula pamoja, hata wapinzani niwaombe wasipoteze kura zao kwa mtu ambaye wanajua hatashinda wapeni kura wagombea wa CCM waendelee kuongoza na kuleta maendeleo,” amesema.

PIA SOMA
- LGE2024 - Makalla: Wagombea wa CHADEMA sifa yao kuu ni ukamanda Wagombea wa CCM sifa yao ni Utu na unyenyekevu na wanapatikana kidemokrasia wachagueni hao tu
 
Back
Top Bottom