LGE2024 Pwani: CHADEMA waeleza changamoto za Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,172
5,532
1732726874065.jpeg

Baraza la Wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Kanda ya Pwani leo Novemba 27, 2024 limetembelea vituo vya kupigia kura katika mitaa mbalimbali ya Kinondoni likiwa limeambatana na kaimu Mwenyekiti wa Baraza hilo Taifa, Sharifa Suleiman.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Kanda ya Pwani, Rose Moshi wanawake hao wamebaini changamoto kubwa kuwa ni majina mengi ya wapiga kura kutokuwepo na yaliyopo kudaiwa kuwa hayasomeki vizuri.

Akizungumzia hatua hiyo Kaimu mwenyekiti wa BAWACHA Taifa, Sharifa Suleiman ameeleza kuwa hali hiyo imewakosesha haki wananchi kuchagua kiongozi wanayemtaka kutokana na sababu ambazo hazikuwa na ulazima.
 
Back
Top Bottom