Pwani: Baada ya mvua kuharibu Barabara ya Chalinze – Segera, TANROADS waendelea na ujenzi hadi usiku

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,464
Mvua zinazoendelea kunyesha Nchini zimesababisha uharibifu katika Barabara ya Chalinze – Segera hasa eneo la Kimange Mkoani Pwani.

Awali baada ya kudaiwa njia hiyo imefungwa kutokana na mvua iliyonyesha Aprili 15, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alisema “Barabara ilifungwa wakati mvua inanyesha ila baada ya hali kutulia, gari zinapita upande mmoja huku TANROADS wakiwa eneo la tukio ili kurudisha njia zote zipitike kama kawaida.”

Akizungumza usiku wa Aprili 15, 2023 akiwa eneo la tukio Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila amesema “Tumefunga njia moja maboresho yanaendelea, tunaweka zege na mawe ili kutengeneza barabara kutoharibika tena, eneo litakuwa salama kufikia Aprili 16, 2023.

“Hata kazi itakapokamilika bado watumiaji wataendelea kutumia njia moja ili kutoa nafasi kwa zege kukauka.”
 
TANROADS HAKUNA KULALA

HATUA ZA HARAKA KURUDISHA MATUMIZI YA BARABARA YA CHALINZE - SEGERA ZINAENDELEA
 

Attachments

  • VID-20230416-WA0022(1).mp4
    15.3 MB
Safi sana mama piga kazi kanyaga twende. Hii ndio Tanzania yako inapendeza
 
Back
Top Bottom