GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,320
Nimeona Misungwi mkoani Mwanza na Geita Vijijini mkoani Geita!
Akiwa amebeba mizigo, anapigwa!
Akiwa analimishwa, anapigwa!
Akiwa anakokota mkokoteni, bado anapigwa!
Ni kama vile "lugha" pekee wanayoijua ni kipigo!
Utakuta wengine migongoni mwao kuna michubuko iliyotokana na ama kubebeshwa mizigo mizito au vipigo vya binadamu "wajinga"
Kwani haiwezekani kutumia njia nyingine kumfanya afanye kazi bila kujeruhiwa?
Kwani kipigo ndiyo njia pekee ya kumfanya punda kutimiza matakwa ya mmiliki wake?
Mbona kwa nchi zingine, hata tembo wanatumiwa kwa shughuli za kibinadamu katika mazingira rafiki tofauti na inavyotendeka kwa punda wa Tanzania?
Je! Punda amemkosa mtetezi? Simba, tembo, chui, fisi, mpaka na nyoka, wote hao wanalindwa na Serikali. Punda hana maslahi kwa Serikali?
Tanzania haina watetezi wa wanyama, au utetezi wao unaishia kwa nyangumi?
Kwa nini isijitokeze taasisi itakayotoa Elimu kwa wamiliki wa punda ili wajue jinsi ya kuwatumia kwa manufaa bila kuwasababishia mateso?