Pugu Road ilikataa jina la Nyerere Road na daraja la Kigamboni litakataa kuitwa daraja la Nyerere

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
20,857
51,486


Jana mheshimiwa Rais kapendekeza jina la daraja jipya la kigamboni liitwe daraja la Nyerere Ushauri wa mkubwa ni amri,daraja litaitwa Nyerere Sababu alizotoa ni za msingi sana lakini amini usiamini jina hili litaishia kwenye makablasha tu watu wataendelea kuliita daraja la Kigamboni,hata jiwe la ufunguzi liliandikwa daraja la kigamboni

Zamani Nyerere road ikiitwa Pugu Road kabla ya kubadilishwa jina lakini asilimia kubwa ya watu waliokuwa mjini enzi hizo bado wamezoea kutumia jina la Pugu Road labda wageni ambao hawajui kuwa ile ilikuwa ikiitwa Pugu Road

Natambua mchango mkubwa wa Marais wa Taifa katika nchi hii kuanzia Nyereri Mpaka JPM ila kila kitu kuita majina a viongozi wa kisiasa ni kutaka kudanganya umma kuwa wao ndio wa maana zaidi na kutotambua mashujaa wengine ambao hawakuwa wanasiasa ila wameiletea heshima nchi yetu,kuna watu kama akina Filbert Bayi,Ikangaa,Samatta,na yule mchawi aliyegundua mwenge sijui anaitwa Gonzo sijui nani hao wote ni mashujaa wa nchi yetu,Kuna mitaa maarufu na miundombinu maarufu ingepewa majina yao,sio kila kitu kizuri basi ni Mkapa Tower,Kikwete Hospital,Ali Hassan Mwinyi Road,Mkapa Bridge,Kikwete Bridge,JK Nyerere International Airport.kama Kuendekeza wanasiasa ndio maana barabara inayopita uani mwa ikulu inapewa jina la Barack Obama Drive wakati anayelala humo ni Rais wa Tanzania

kama sio lazima kutumia majina ya watu tutumie majina ya wanyama au vivutio vya utalii au majina ya sehemu husika nikiwa na maana daraja lingeendelea kuitwa kigamboni kama ilivyo mororgoro road,Pugu Road,Kilwa Road hiyo ni njia ya kutangaza utalii
 
Hilo ni daraja la Kigamboni.
Nyerere ni jina la heshima
 
umesomeka hata me nilijiuliza juzi kati kwan kuna ulazima wa kutumia jina moja kwa matukio kadhaaa kwan wengine hawapo? ifikie mahali tuwathamini na viongozi wengine mashuhuri
 
Hahahahahaaaaaa, mi umeniacha hoi kwenye hiyo sahihi yako tuuu
 
Kumbe mwenge uligunduliwa na mtu mwingine tofauti na nyerere, aisee go deeper kidogo kwenye hili
 

Hata jina la nchi liwe 'Kilimanjaro' badala ya Tanzania ili tuone kama majirani wataendelea kudai mlima Kili uko kwao. Huwezi kusikia mtu akisema mlima Kenya uko TZ au Uganda, kwa nini?
Tena ukitaka kufunga kazi TZ iitwe 'SERENGETI' kabisa!
 
Nchi hii ya maajabu. hivi kila kitu kitaitwa Nyerere, nahofia watu watageuza majina ya wake zao na kuwaita Nyerere kwa style hii. Vitu vyenye majina ya Nyerere vinatosha jamani Rais wetu! Kama kumuenzi Nyerere yamefanyika mengi yanatosha. Nyerere alikuwa mtu kama wewe na mimi na yule!
 
hapo kwenye kibao ingekuwa daraja hili la nyerere ingekuwa poa ila watu watazoea kuita daraja la kigambon maana na kibao kimeandkwa hvyo
 
Binafsi nawapenda mashujaa wetu,
Ila sioni ulazima wa kuname kila kitu kwa majina yao. Nikishangaa sana kuona eti ile hospitali ya udom inaitwa Benjamin mkapa hospital, kwanini isingeitwa tu hospitali ya Udom?
Kwani kuwaenzi ni lazima tuwape majina mpaka ya majengo? Huu kwangu ni upuuzi tu,
Hilo ni Daraja LA Kigamboni na litabaki kuwa LA kigamboni. Tunampenda baba wa taifa kwa mema mengi ila sio lazima kumuenzi kwa kutumia jina lake kwenye majengo na Barbara..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…