PSPF-Nini Kinachoendelea?

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,726
3,762
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji - PIC imesema mfuko wa pensheni wa PSPF upo hatarini kufa muda wowote kuanzia sasa kutokana na deni kubwa ambalo mfuko huo unadaiwa ambapo mpaka sasa deni limefikia fedha za Tanzania shilingi Bilioni 987.7





Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji chini ya Mwenyekiti wake Richard Ndassa ikipitia ripoti ya mfuko wa pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam leo.
Kiasi hicho cha fedha ni kutokana na madeni ambayo mfuko huo unaidai serikali pamoja na uwekezaji ambao umefanywa na mfuko huo katika maeneo mbali mbali nchini ikiwemo ujenzi wa majengo na kama Chuo kikuu cha Dodoma na ukumbi wa bunge.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, mbunge wa Sumve Bw. Richard Ndassa, ametoa angalizo hilo jijini Dar es Salaam leo na kwamba kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 453 ni madai ya wastaafu wanaofikia 53,734 wengi wao wakiwa ni walimu wanaoidai serikali mafao yao, ambapo katika kufanya hivyo hujikuta wakizurura na makaratasi katika ofisi za umma pasipo msaada wowote.

Imedaiwa kuwa kwa kipindi cha miezi sita serikali haijapeleka michango ya makato ya watumishi wake kwa mfuko huo kiasi cha kufikia kushindwa kulipa hundi za malipo kwa miezi kadhaa, huku mfuko huo ukiingia mkataba wenye utata na mfanyabiashara mmoja maarufu nchini ambapo inaelezwa kuwa shirika hilo linamdai mfanyabiashara huyo takribani shilingi bilioni sita.

Katika maelezo yao, wajumbe wa kamati wameitaka serikali kutoa majibu ya jinsi inavyoweza kutatua tatizo la madeni yanayoikabili PSPF, ili iweze kulipa madeni ya malimbikizo ya pensheni kwa wastaafu ambao kwa sasa wanaishi maisha magumu.

Aidha, wabunge hao wameitaka serikali kuacha tabia ya kuchukua pesa kutoka katika mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na mashirika mengine ya umma bila kulipa, kwani ipo siku serikali yenyewe ndiyo itakayoiua mifuko na mashirika hayo na kuleta madhara makubwa kwenye uchumi.

Nafikiri wakati umefika sasa W kwa anachama wa Pension Institutions kushituka na kutengeneza chama cha kutetea maslahi yao wanayochangia. Vinginevyo tatizo hili haliwezi kwisha kwa sababu fedha hizi zinatumika vibaya na tuliowapa dhamana.


Source; BY Langolajiji blog. Kamati ya PIC yasema mfuko wa PSPF hatarini kufa | langolajiji
 

wameshakula shakula yao
 
Mkwere aliahidi mbeya katika sikukuu ya mei mosi kuilipa PSPF lakini wapi. Mashirika ya umma yanauliwa na serikali yenyewe. Utashangaa mkurugenzi PSPF anafutwa kazi kwa kusema ukweli
 
Mkwere aliahidi mbeya katika sikukuu ya mei mosi kuilipa PSPF lakini wapi. Mashirika ya umma yanauliwa na serikali yenyewe. Utashangaa mkurugenzi PSPF anafutwa kazi kwa kusema ukweli
Sababu Ni kuwa they just invested poorly In liabilities instead of in assets.
 
Hii sasa ni hatari kubwa sana kwa wanachama wachangiaji, ndio maana wastaaafu wanasumbuliwa sana,
Mfuko huu umeprove failure ni wazi kabisa wanachama hawanufaiki vilivyo, hakuna mikopo ya fedha kwa wanachama. Sas mwishowe wanachama watapoteza haki zao kama mwendo ndio huo
 
Hii Ni pension crisis, haina tofauti na lile tatizo la financial crisis lililowakuta wamarekani miaka ile. Bailout hapo is inevitable
 
Kampeni na hela za kuhonga wapiga kura za chama cha mafisadi ndio hua zinatafuna fedha za mifuko ya hifaz...
 
Hapa ndo kazi ipo, sehemu kubwa ya investment za mifuko ni majengo na kwenye bonds za serikal ambayo cjui liquidity yake ikoje, na serikali kwa namna nyingine ndo mpangaji mkubwa wa hayo majengo halaf halipi kwa wakat. Sasaiv mh.Magu ndo atajua maana halisi ya urais, mifuko ikiyumba mabenki ndo yatafuatia kukwama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…