Profesa Nyagori ashauri Taasisi za Afya kumpa tuzo Rais Magufuli kwa mapambano ya Corona

Mvidunda

Senior Member
May 30, 2020
122
170
PROFESA NYAGORI ASHAURI TAASISI ZA AFYA KUMPA TUZO JPM MAPAMBANO YA CORONA

NA MWANDISHI WETU-MOROGORO

Daktari Mshauri Mwandamizi wa Magonjwa ya Ndani na Moyo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ambaye pia ni Mhadhiri wa vyuo vikuu mbali mbali vya tiba, Profesa Harun Nyagori, ameshauri taasisi za vyuo vikuu vya Afya nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), kumpatia tuzo maalumu ya heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kutambua mchango wake katika kupambana na janga la Corona.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro jana, Profesa Nyagori ambaye amewahi kutunukiwa tuzo mbalimbali za kimataifa zilizotambua mchango wake katika tafiti za maradhi ya moyo barani afrika, alisema kuwa kuna haja ya kutambua mchango mkubwa uliotukuka alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kwa mbinu za kipekee alizozitumia kupambana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virus vya Corona.

“ Nikiwa kama mtaalamu niliyebobea katika masuala ya tiba ya maradhi ya binadamu, ninampongeza sana Rais Dkt John Magufuli, kwa namna alivyoweza kutoa mchango wake mkubwa kwa Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla katika kupambana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Corona na ninatoa wito kwa taasisi za vyuo vikuu vya Afya hapa nchini na Shirika la Afya la Duniani (WHO) kumpatia tuzo maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kutambua mchango wake.”

Profesa Nyagori aliongeza kusema kuwa ugonjwa wa Corona ulipoingia kwa mara ya kwanza hapa nchini, wananchi wengi walijawa na hofu kubwa juu ya athari za ugonjwa huo na hivyo walihitaji sana kumpata mtu wa kuwatoa hofu hiyo.

“ Msongo wa mawazo (stress) unasababisha uwezo wa kinga mwilini kushindwa kupigana na maradhi na hivyo kinga za mwili kupungua ambapo kichocheo cha corticosteroid kinachozalishwa kwenye mwili kinaweza kuwa kisababishi kikubwa cha kupunguza kinga za mwili. Hofu huchukua nafasi kubwa sana katika kumfanya mtu kupata athari kubwa za ugonjwa fulani. Kisayansi hofu husababisha kinga za mwili wa biniadamu kushuka na hivyo kumfanya kuwa rahisi kuambukizwa na kushambuliwa na maradhi sambamba na kupata athari kubwa zaidi. Rais Dkt John Magufuli amefanya kazi kubwa kuwajengea ujasiri Watanzania kutokuwa na hofu kubwa juu ya ugonjwa huu wa Corona, huku wakichukua taadhari za kiafya ambazo wataalam wa Afya wanazitoa. Hatua hii imeepusha kwa kiwango kikubwa, athari ambazo zingetokana na ugonjwa huu.” Alisema Profesa Nyagori.

Profesa Nyagori aliongeza kusema kuwa majirani zetu na nchi nyingine nyingi ulimwenguni zimejikuta katika sintofahamu kubwa kutokana na janga la Corona kwa sababu hazikuwa na viongozi mathubuti, wenye msimamo, mbinu na ubunifu wa namna sahihi ya kupambana na janga hili kwa njia ya kisaikolojia kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa nao.

KUHUSU KARANTINI
Akizungumzia kuhusu mbinu ya kujifungia ndani (karantini) kama njia ya kuepuka na kuepusha kusambaa kwa maambuki ya virusi vya Covid-19, Profesa Nyagori alisema kuwa mbinu hiyo endapo kama ingetumika, ingelikuwa na madhara makubwa kuliko faida.

“ Hatua ya Rais Magufuli kutokubaliana na mbinu ya kujifungia ndani (Lockdown), imesaidia sana katika kuwafanya watanzania kuendelea kutafuta fedha ambazo zimewawesha kumudu kupata milo yenye lishe ambayo kimsingi imeimarisha kinga zao na kufanya isiwe rahisi kushambuliwa na maradhi Corona.

“Kujifungia ndani licha ya kisaikolojia kuongeza wasiwasi, lakini pia humfanya mtu kutopata fursa ya kutafuta pesa na hivyo kutomudu kupata mahitaji muhimu ikiwemo vyakula mchanganyiko ambavyo ni muhimu kwa lishe inayoimarisha kinga mfano vitamin na madini mbalimbali.” Alisema Profesa Harun Nyagori.
 
Hivi Magufuli aliwahi kupambana na Corona? Alichofanya na anachofanya Magufuli ni kuuficha ukweli juu ya janga hili kwa watu wasiokuwa na utimamu wa akili kama huyo profesa uchwara. Magufuli hajawahi kupambana na Corona. Ameacha wakufa waendelee kufa.

Naamini itakuja kumfikia na ataipata hiyo tuzo kwa wakati huo!
 
Professor amesahau kwamba kidaktar tunapambana kwenye Maabara sio ntantalila za mdomoni..yeye amejitoa ufahamu katka Hilo..ningekua professor ningetoa wazo la tuzo kama angekuepo aliegundua dawa ya Korona..na watu wakapona na sio tantalila za wanasiasa!!
 
Rubbish professor! Anatafuta kuchaguliwa/kuteuliwa. Eti professor, ndio maana Lisu anawadharau! Tuzo apewe kwa kufnya nini? Serendipity has saved the day , wa Brazil ali-apply serendipity unajua wanakufa wangapi a day?
Utakufa na stress wewe. Rais Magufuli humuwezi hata chembe wewe tunajua umedhibitiwa kwenye ufisadi wako sasa unahaha tu!
 
kamanda mzuri vitani hujukikana kwenye Vita chadema walk hi lock down wao bila kushirikisha wanachama wao wakatelekeza wanachama wao wajijue wenyewe kama watakufa kwa Corona shauri yao mwenyekiti mbowe na viongozi wenzie wabunge wakatelekeza Vita.

Raisi Magufuli akawa msitari wa mbele vitani akiongoza mapambano akasema ingieni kusali tufunge tuombe Mungu siku tatu na tujifukize. Mungu akasikia na kujifukiza kukatusaidia Vita ya Corona tumeshinda chini ya jemadari kiongozi anayejali watu wasife kwa corona .Apewe nishani na awamu ya pili
 
kamanda mzuri vitani hujukikana kwenye Vita chadema walk hi lock down wao bila kushirikisha wanachama wao wajatelekeza wanachama wao wajijue wenyewe kama watakufa kwa Corona shauri yao mwenyekiti mbowe na viongozi wenzie wabunge wakatelekeza Vita. Raisi Magufuli akawa msitari wa mbele vitani akiongoza mapambano akasema ingieni kusali tufunge tuombe Mungu siku tatu na tujifukize. Mungu akasikia na kujifukiza kukatusaidia Vita ya Corona tumeshinda chini ya jemadari kiongozi anayejali watu wasife kwa corona .Apewe nishani na awamu ya pili
Huyu Nyangori si ndiye aligundulika kuwa ni Dr feki kule Mbeya na Mororo? Maajabu ameibukia Tasisi ya JK.
 
kamanda mzuri vitani hujukikana kwenye Vita chadema walk hi lock down wao bila kushirikisha wanachama wao wakatelekeza wanachama wao wajijue wenyewe kama watakufa kwa Corona shauri yao mwenyekiti mbowe na viongozi wenzie wabunge wakatelekeza Vita. Raisi Magufuli akawa msitari wa mbele vitani akiongoza mapambano akasema ingieni kusali tufunge tuombe Mungu siku tatu na tujifukize. Mungu akasikia na kujifukiza kukatusaidia Vita ya Corona tumeshinda chini ya jemadari kiongozi anayejali watu wasife kwa corona .Apewe nishani na awamu ya pili
Alikimbia Dar akapita dodoma akaenda kujificha chato baadaye lubondo
 
Masikini Prof Nyagori , sijui kama ana elewe mwenendo wa corona duniani . Kwa ufupi Africa imepata unafuu sana kuhusu corona. Kwa hili Tumshukuru mungu . Hivi TANZANIA tungepata mlipuko kama wa Spain , Italy ,au Brazil pangekalika hapa .

Vifaa vya corona tu serikali ilikuwa inatembeza bakuli , Hospitalini oxygen pia hakuna .Nazungumza hivi sio kwa ushabiki wa kisiasa sababu mimi mwenyewe nilipata corona huku ughaibuni nikajionea hali halisi , TUMSHUKURU MUNGU KWA KULIEPUSHA BARA LA AFRICA KWA UGONJWA WA CORONA
 
Kusema ukweli Magufuli amefanya vizuri kwenye maamuzi yake kuhusu covid19. Nilimuunga mkono tangu mwanzo na bado namuunga mkono.
 
Wampe na mbowe kwa juhudi zake za kuwatia hofu na kuwatisha wananchi kuhusu Corona
 
Back
Top Bottom