Prof. Mkumbo asaini mkataba wa kupeleka maji wilaya za Tabora

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Wakati wengine wakiendelea kupiga kelele kuhusu uteuzi wa Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, yeye ameanza kutoa majibu ya vitendo kama alivyoahidi wakati akiapishwa na Rais Magufuli.

Prof. Mkumbo alisema, “Maisha yangu yote mpaka hapa nilipo nimetumia muda wangu mwingi kuhoji na kuuliza maswali hasa kwa serikali. Nimepata fursa sasa ya kushiriki kikamilifu, badala ya kuhoji nina kazi ya kujibu maswali ya serikali. Mheshimiwa Rais nakuahidi kuwa nitajibu hoja mbalimbali za serikali kwa nguvu zangu zote”.

Wananchi wa wilaya za Mkoa wa Tabora zinaelekea kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji katika maisha yao ambapo wananchi zaidi ya milioni 1.1 wa wilaya za Tabora watapata huduma ya maji kufikia 2019.

Huu ni mradi ambao utavuta maji kutoka ziwa Victoria.

Kazi ya msingi ya serikali ni kujibu hoja/changamoto kwa vitendo na siyo maneno pekee.

Hii ndiyo kazi tunayoitaka katika msingi wa dhana ya HapaKaziTu katika kuleta maendeleo ya haraka nchini.

 


Safi sana, ila nina swali unafahamu chanzo cha hayo Maji labda? Je ni yale ya kutoka Ziwa Nyanza?
 
swala kwa wale wataalam huu mradi wa maji From victoria na ule wa maji from malagalasi upi ungekuwa wa haraka kutekelezwa kwa ajili Ya wana Tabora ? kudos Kitila mkumbo
 
Watu hataingia pepon mpaka waamin.nahawataamin mpaka wapendane.nahawatapendana mpaka watoleane salam.aman ya mwenyezi mungu iwe pamoja nanyi.tupendaneni jaman upendo ndio msingi wakufungua njia chuki huzaa ubaya ubaya huzaa uchawi nauchawi huzaa mauaji namauaji huliangamiza taifa.angalien mataifa ya wenzetu nichuki2 kua huyu ninanii nasisi niwakina nanii huyu sii wamrengo wetu.bas wakachukiana wakauana taifa likapoteza dira
 
At least tumepata katibu mkuu ambae ni "professor & politician at per"
Hapa tujipange maana hata ziara mwalimu wangu huyu wa zamani naona ameanza V8 na masaki residence jamani sio kitoto!!!
 
Watanzania tuu waajabu sana mtu anachukiwa kwasababu2 anaitikad flan.tumeshindwa hata nawazungu niwabaguzi wa rangi lakin walimchagua obama kutokana2 nauwezo wake.
Mkuu;

Usihangaike na kikundi cha watu wenye chuki za kinafiki.

Inashangaza kuna wengine kila siku wanaomba ajira serikalini lakini walikuwa wanataka Prof. Kitila akatae uteuzi. Mtu anakuambia usifanye hiki lakini usipofanya anakifanya yeye.

Hawa ndio walewale waliwaambia CCM wasimsimamishe Edward Lowassa kuwa mgombea Urais wa Tanzania, lakini baadaye wao ndio wakamsimamisha kuwa mgombea Urais wa Tanzania baada ya CCM kukubaliana na hoja zao.

Unafiki ni hatari sana!
 
Mkuu tutazid kuwaelimisha siku zote.unajua hii jamii huku mtandaon walilelewa kitikad zaupande mmoja kwahiyo mtu anakua anajua ni hivi tu hakuna zaidi tunataka tuwaelimishe wajue kua vyama vipo lakin sisi ni team nchi kwanza lazima tuwe navyama kwaajili ya chaleng lakin muhim kuliko vyote ni nchi yetu.tutoke kwenye kudanganyana twende kwenye ukwel.mkuu upinzan tanzania hakuna nivema tukarud tuangalie tulipokosea niwapi tujirekebishe tujipange upya hapo nitakubali
 
Ndio shida ya mwanaume kupenda kusikiliza mipasho ya Mama Kopa! Sasa maji yanatoka wapi kupelekwa Tabora? Yanatoka Ethiopia?
Dogo usipende kurukia kukomenti. Imeandikwa kabisa maji yanatoka Ziwa Victoria halafu unauliza yatatoka wapi!!!!
 
Tulikuwa nae wizarani juzi ktk kikao chake cha kwanza kwa watumishi, namna alivowasilisha na kujibu maswali, hupati tabu kujua kuwa jamaa kichwani yupo vizuri!
 
swala kwa wale wataalam huu mradi wa maji From victoria na ule wa maji from malagalasi upi ungekuwa wa haraka kutekelezwa kwa ajili Ya wana Tabora ? kudos Kitila mkumbo
Mkuu Mdokozi;

Swali lako liliwahi kuulizwa bungeni na Mbunge Daniel N. Nsanzugwanko ambaye aliuza:-

Katika Mto Malagarasi iko miradi mikubwa mitatu ambayo ni mradi wa kutoa maji Mto Malagarasi kwenda katika vijiji 69 vilivyopo Wilaya ya Urambo, uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji wa miwa na mradi wa uzalishaji wa umeme wa megawati 44.5.

(a) Je, Mto Malagarasi una ujazo gani wakati wa masika na kiangazi?

(b) Je, maji ya mto huo yanatosheleza mahitaji ya miradi hiyo mitatu?

(c) Je, Serikali imefanya utafiti wa kiufundi kujua bajeti ya maji katika mto huo?


Majibu:-
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Nicodemus Nsanzugwanko, Mbunge wa Kasulu Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia Mto Malagarasi, ikiwemo mradi wa maji kwa ajili ya Miji ya Urambo na Kaliua, kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji umeme wa megawati 44.5. Wakati wa masika mto huu unakuwa na maji yanayotiririka kwa mita za ujazo 55 kwa sekunde; na wakati wa kiangazi unakuwa na mita za ujazo 40 kwa sekunde.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Kwanza imekamilisha mipango ya pamoja ya uendelezaji na usimamizi wa rasilimali za maji katika Bonde la Ziwa Tanganyika ambako Mto Malagarasi unapatikana. Hii ni sehemu ya utafiti wa kiufundi wa kujua wingi na ubora wa maji pamoja na mgawanyo sawia wa matumizi ya maji katika Bonde dogo la Mto Malagarasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utafiti huo, umeonesha ya kuwa Mto Malagarasi una maji ya kutosha kwa miradi mbalimbali itakayoibuliwa ikiwemo miradi mitatu iliyotajwa na bado yatabaki kuelekea yakitiririka kwenda Ziwa Tanganyika.
 
Kumekucha! waliopewa hati miliki ya hayo maji na malkia wajue tumeamua. Nitafurahi kusikia project imekamilika na maji yameanza kutiririkia Tabora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…