Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,201
- 5,586
Mbunge wa zamani wa Mikumi na Msanii Staa Joseph Haule maarufu Prof. Jay @professorjaytz amesema sauti yake imebadilika kidogo kwakuwa Madaktari wa Muhimbili Hospital walimtoboa koo ili wavute uchafu kwenye mapafu yake ambao ulimfanya ashindwe kupumua.
Akiongea kwenye Power Breakfast ya @cloudsfmtz leo November 06,2023, Prof. Jay amesema “Ilifika wakati pumzi ikakata siwezi kupumua, na kama unavyosikia sauti yangu Madaktari ilibidi wanitoboe koo ili waweze kuvuta uchafu kupitia kwenye koo kwasababu mapafu yalikuwa yamejaa uchafu, hiyo yote ni mipango ya Mungu”
“Niliwekewa mpira unavuta kupitia mdomoni, wakati huo natumia mpira kula kwenye pua na mipira mingine ya dyalsis kwahiyo mwili mzima ulikuwa na wayawaya, Madaktari wakasema lazima tumtoboe koo Ndugu zangu wakagoma wakasema huyu Jamaa mtaji wake ni sauti kwenye siasa kwenye muziki lakini Madaktari wakasema tutampoteza huyu”
“Ndugu wakaona hali inazidi kuwa mbaya hata ile mashine ikawa inapoteza nguvu ya kunisaidia kwahiyo wakanitoboa koo, ndio maana nawapongeza Madaktari wa Muhimbili baada ya siku chache nikawa naanza kupumua poa“