The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 693
- 1,165
“Wale watu wanaokula mara nyingi, wanaokula mara kwa mara wanakuwa hawana muda wa kuunguza mafuta. Wanaofunga muda mrefu wanakuwa na muda mrefu pia wa kuunguza mafuta ya Mwili. Kuna magonjwa mengi yanayosababishwa na ulaji wetu wa mara kwa mara. Ukitaka kinga ya mwili iwe juu na kurefusha maisha, si kurefusha tu maisha bali maisha yenye quality (Ubora), kula mlo mmoja. Ni ngumu kuvumilia lakini mwili siku zote una tabia ya kuzoea. Si lazima ule mlo mmoja kila siku, unaweza kubadili ukala mara mbili au tatu kwa wiki, siku zingine ukala mara mbili”
Nukuu ya Pro. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Rais kuhusu Masuala ya Afya akizungumza kupitia Afya Podcast ya Muhimbili TV, Septemba 4, 2023
Nukuu ya Pro. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Rais kuhusu Masuala ya Afya akizungumza kupitia Afya Podcast ya Muhimbili TV, Septemba 4, 2023