KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,993
- 36,500
Chama cha Figo nchini kimejiandaa kupeleka mapendekezo Serikalini kuanzisha uchukuaji wa Figo kwa marehemu, ili kuongeza idadi ya wapandikiziwaji kwani wengi wanashindwa kumudu kutokana na uchache wa watoaji figo hizo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi, kwenye maadhimisho ya siku uchangiaji viungo Duniani leo Hospitalini hapo.
Source: EATV
MY TAKE: Kwa namna yoyote hali hii ikipita inaweza kuleta mtafaruku kwenye kuvuna hizo FIGO kwa marehemu au watu kumaliziwa wakiwa wodini ili wawahishe FIGO kwa wahitaji.