JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,688
- 6,484
Msimamo wa Timu Tatu za juu, Arsenal pointi 64, Liverpool (64) na Man City (63), hivyo atakayeshinda leo anaweza kuathiri kiasi fulani mbio za yule atakayepoteza.
Takwimu za jumla, Timu hizo zimekutana mara 210, Arsenal imeshinda mechi 99, City 65 na sare zikiwa ni 46 na mara ya mwisho kukutana (Oktoba 8, 2023) Arsenal ilishinda 1-0.
Rekodi ya ushindi mkubwa, Arsenal 5-0 Manchester City (Oktoba 27, 2000) na Manchester City 5-0 Arsenal (Agosti 28, 2021).
####
MAN CITY 0-0 ARSENAL, LIVERPOOL YASHIKA USUKANI
Mchezo wa Manchester City dhidi ya Arsenal umekamilika kwa suluhu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Etihad, matokeo ambayo yanaiwezesha Liverpool kuongoza msimamo wa Premier League
Arsenal imefikisha pointi 65 na hivyo kushuka hadi nafasi ya Pili ilifuatiwa na Man City yenye alama 64.
Liverpool ambayo imeshinda 1-0 dhidi ya Brighton inaongoza msimamo kwa kuwa na pointi 67.