Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 14,240
- 22,488
Nimesikia CBE wamekuja na Template ya kuwa na Public Private Partnership kujenga Mabweni na Kujinasibu kwamba wamekuja na kitu bora na hadi kupeana zawadi ya kufanikisha hicho kitu..., Sasa najiuliza je jambo hili ni geni au lina tofauti zipi na kama tofauti zipo Je zitakuwa na tija...
Watu Binafsi wamekuwa Wakisadia na Kunufaika na Mabweni / Hosteli hili sio Jipya:
Ukienda chuo chochote au karibia na hapo watu wamekuwa wakijenga mahosteli yao binafsi sababu kuna soko la wanafunzi baadhi wasiopenda kukaa karibu / kwenye hostel za chuo au kama kuna uhaba na hazitoshi kwahio wanawekeza pesa zao kuanzia kununua ardhi mpaka kujenga.. (kwenye issue hii ardhi ndio gharama zaidi); Premium Areas.
Je Hosteli ni Huduma / Biashara
Kwa mwanafunzi au mwanachuo hana option lazima atafute sehemu ya kukaa.., hivyo ni jukumu la Chuo ambacho kinapata ruzuku za kodi za wananchi kuhakikisha kila mwanafunzi ana shelter ambayo ni affordable; sio mbaya watu binafsi wakiona fursa nao wakajenga hosteli hizo karibu na vyuo either zikiwa premium kwa bei ya juu au kwa bei rahisi zaidi kama wanaweza ili kuvutia wateja (if its possible). Kwahio tukisema na hizi ambazo ni huduma (affordable) nazo tuziweke ziwe for Profit ni kwamba lazima bei iwe juu (overheads plus profits) na kama kuna wanafunzi watashindwa kulipa premium prices ni kwamba serikali / kodi itabidi ifidie..
Je Tatizo ni Ujenzi au Usimamizi
Hapo inabidi tujiulize tatizo lipo wapi ? Je kujenga ni gharama au soko / faida ni ndogo ? Sababu kama hii ni huduma muhimu na hakuna option mwanafunzi lazima apate sehemu ya kukaa, na kama mwanafunzi huyo ni fukara hana pesa za kulipa premium basi utaona kwamba hii biashara hailipi..., Ila kama inalipa na wanafunzi ni wengi na faida ni kubwa ila issue ni usimamizi kwanini Chuo kisi outsource usimamizi kwa mtu na katika ile faida kumpa huyu msimamizi na wenyewe kubaki na faida ?, Sababu ukisema ni Ubia Partnership na mtu binafsi na faida isipokuja ni either utaongeza bei au kodi zetu zitafidia faida ya huyu mtu...
Cutting Corners (Maximizing Profits)
Kwenye huduma au service ambayo mtu hana choice kipaumbele kikiwa ni faida basi lazima kona zikatwe sehemu, kuna research ilifanyika Kenya baada ya jengo / bweni kuungua na watu kufa, iligundulika kwamba mahosteli / bweni mengi hayakidhi vigezo na yapo below standards (nadhani hata kuna waliosema hostel za JPM zilianza kupata ufa baada ya muda mchache) kwahio kama mtu amewekeza labda apate pesa yake baada ya miaka kumi sidhani kama atajenga jengo la kudumu miaka 30.
Je tuwekeze PPPs Wapi ?
Mfanyabiashara wala hatakiwi kukumbushwa au kuambiwa pale kuna fursa kama ataona fursa basi atawekeza na kama kuna sehemu serikali inafanya na yeye anaweza kufanya basi na afanye na kuongeza ushindani (mfano ma hosteli na yeye anaweza kuweka yake private kama alternative ili wasiotaka ya huku ambayo ni affordable waende kwake, au kama anaweza kufanya affordable zaidi basi all the best).., Ila kuna sehemu ambazo kuna watu private can do it better au wana kitu ambacho serikali hawana basi Ubia huo ndio unafaa.., mfano;

- Badala ya Kampuni za Simu kuwa na minara yao na miundombinu kila kona TTCL wanaweza wakawekeza infrastructure safi kabisa na kuwakodisha hawa watu... (Partnership TTCL Miundombinu na watu Binafsi Coverage / Marketing)
- Badala ya mwendokasi (serikali) kuhangaika na ununuzi wa magari na maintenance wanaweza kuingia ubia na kampuni kama TATA au kampuni yoyote ambayo itaguarantee ufanyaji kazi wa mabasi na service zake na mwisho wa siku kugawana faida
- Badala ya kuhangaika na ma IT wa hapa na pale wasio na uwezo serikali inaweza kuingia ubia na ma giant ambao wamebobea na kuhakikisha ufanyaji kazi ni wa uhakika na hauna shida.
- Tukumbuke kama ni outsourcing hili sio jipya limekuwa likifanyika tangu enzi na enzi kwahio kama ni outsourcing ya kitu fulani tender zitangazwe openly ili kila mmoja mwenye uwezo aweze kushiriki na kama ni HUDUMA basi kipaumbele kiwe affordable prices na sio how much a Private individual atatoa Gawio