Reverend Kishoka, umepotea sana jamvini, lakini kama kawaida kuibuka tu umeibuka na kigongo kikali kama kawaida yako!
Nikirudi katika mada, ni dhahiri kwa kadri siku zinavyosogea Ule mtaji wa Kisiasa ambao Raisi Magufuli aliingia nao, unakatika kwa kasi ya kutisha, nitaelezea machache kwa nini hali imekuwa hivi na suluhisho.
1. Hali na Hofu ya Mwelekeo Usiotabirika wa Kiserikali.
Hapo mwanzo JPM alivyoingia madarakani, ile hali ya tumbuatumbua ilishangiliwa sana kutokana na ukweli kwamba Watanzania walikuwa wanakerwa mno na kiwango cha ufisadi katika nchi hii, lakini kadri staili ya utumbuaji ilivyoendelea na ilivyofanywa, ikajenga hofu kubwa katika kada ya utumishi, hofu hii ina faida zake ikiwemo nidhamu " japo hata ya woga ikiwemo", lakini hasara mojawapo ni watu kuogopa kufanya maamuzi wakimsubiri mkubwa juu yao aamue, mkubwa naye anangoja mkubwa wake juu aamue, kiufupi ule urasimu/bureaucracy ukawa in play, na hii inaweza kushusha ufanisi wa mambo, katika baadhi ya mambo
Lakini pia tukiangalia baadhi ya kauli zinatuma mixed signal na zinashindwa kuclear doubt moja kwa moja, kwa mfano JPM alisema wanasimamisha ajira mpya na mishahara mipya kwa miezi miwili tu, lakini Usimamishwaji huu umeenda hadi mwaka mzima!!. Ishu ya Ajira na malimbikizo ya wafanyakazi yamekula sehemu kubwa ya mtaji wa kisiasa wa JPM
2. Ishu ya Demokrasia
Bila shaka juhudi kubwa sana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi zimefanywa nchini ili kuwafanya wananchi wawe ni washiriki katika kujadili na kuamua mustakbali wa Taifa lao, ushiriki huu ni kwa namna nyingi, kuwa wanachama wa vyama, mijadala, maandamano mikutano n.k, Kitendo cha kulimit mikutano ya kisiasa si kitendo cha kisheria na wala hakikuzi Demokrasia, ni dhahiri ibara ya 11 ya sheria za vyama vya siasa iko wazi kabisa juu ya haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano nchi nzima, na siyo kwenye maeneo waliyoshinda majimbo tu!, Hatua kama hizi zinatia wananchi wasiwasi kwamba, kwa nini unazuia mikutano, Je huna majibu ya kutosha ya hoja za wapinzani wako ndiyo maana unazuia wasizungumze?, lakini pia hii inatia wasiwasi juu ya utawala wa sheria, kwa sababu kama sheria zinasema ABC, lakini wewe unataka ifanyike XYZ hapo kidogo unakuwa haueleweki.
3. Ishu ya Uchumi na bidhaa muhimu.
Ukiangalia kwa sasa hali ya bidhaa muhimu kama sembe, vimekuwa juu sana, Imefikia kilo ya Sembe ni ghali kuliko lita ya petroli, unakuta Sehemu nyingine Sembe ni shilingi 2200 kwa kilo wakati lita ya Petroli ni chini ya hapo, Katika vitu ambavyo JPM inabidi aviangalie sana kama anataka kurudi 2020 basi ni uchumi hususan upatikanaji wa bidhaa muhimu, hivi vinawagusa wananchi moja kwa moja na hali yake ikiwa ngumu, naye atapata wakati mgumu sana mwaka 2020.
Katika kipengele hiki cha uchumi, Ndani ya mwaka 1 wa utawala wake hususan ile bajeti ya mwaka jana kodi imeukuwa si rafiki kwa mtu wa kipato cha chini , chukulia mfano VAT katika miamala ya fedha, vijisenti vya watu vimekwanguliwa kwelikweli kutokana na miamala hii kiasi kwamba sasa watu wanahisi kwamba ni bora warudi kama zamani kupeana cash kwa cash ktk manunuzi badala ya kurushiana, Sasa kitu chochote linachokwamisha pesa kutembea kiurahisi baina ya watu kinadhoofisha uchumi, Kodi za VAT kwenye miamala ya fedha inayolipwa na Mlaji haina budi kuangaliwa!
4. Ishu ya Bashite
Katika vitu vitakavyomcost kisiasa JPM ni ishu ya Bashite, Bashite keshakataliwa na umma, hukumu yake imeshakatwa na watu, kuendelea kumkumbatia ni basi tu lakini hana tena Legitimacy, Kuwepo kwa Bashite katika ile nafasi kunaundermine hatua nzuri na mambo ya msingi sana anayofanya JPM, kwa mfano chukulia mfano suala hili la uhakiki wa vyeti feki, hili ni zoezi zuri mno na ni miongoni mwa Legacy bora kabisa za JPM, lakini hata hivyo linaonekana kutokuonekana hivyo kwa sababu msimamizi mkuu wa watumishi katika jiji fulani naye anashutumiwa kuwa na vyeti feki na yeye wala hajaguswa!
Hitimisho:
1. JPM ajenge mazingira ambapo sera, mipango na maamuzi ya serikali yawe wazi na yanayotabirika
2. JPM aipanue, ailinde, aitetee na aikuze Demokrasia, kwa sababu kwa kufanya hivi hana cha kupoteza zaidi ya kuwathibitishia wananchi kuwa anayo majibu ya lutosha ya mambo yao hata kama wapinzani wanasema hili na lile
3. Uchumi na upatikanaji wa bidhaa muhimu ni muhimu sana, Dembe, Sukari, Mchele, Maharage, Mafuta ya kula, ya taa, gesi ya kupikia, chumvi hivi vitu supply yake haitakiwi kuyumba hata kidogo.
4. JPM inabidi sasa aone na akubali kuwa Bashite anaparalyse State Machinery na anaathiri kwa kiwango kikubwa taswira ya taasisi ya Urais mbele ya umma. Bashite amefanya taasisi ionekane ina double standard ktk suala la vyeti kitu ambacho si kizuri, Ni wakati sasa wa kumuweka Bashite pembeni ili mambo yarudi katika msitari!