Postal/zip code ya Tanzania ni ipi?

Nadhani utakuwa unajaza fomu fulani, hard or soft copy. Na km ni soft copy, labda online form, unaweza ukakuta fomu hiyo inakataa kuwa submitted kwasababu hujajaza sehemu ya Postal Code. Km unaishi Dar, jaza hivi: DSM, TZ. Tanzania hatuna mfumo wa Zip Code, kwahiyo usijaze chochote.
 
Tanzania hakuna zip code.Zip code zinakuwa namba tano ambazo kila state ina namba yake inayoanzia..nahufahamu kwa marekani tu .

Wewe ukiona form haikubali ku submit blank sehemu ya zip code just weka post code ,for out side state.
 
Haya sirmudy zip code ya tz ni hii hapa, 35091. Hii kirefu chake ni (Zone Improvement Program) inarihisha katika kutambua maeneo hususani kwa watu wa posta. hata kama mfumo hou hautumiki hapa tz lakini namba yetu ndio hiyo kaka
 
mkuu ZIP Codes inahusiana na mfumo wa posta wa huko marekani...

hapa kwetu hatuna hicho kitu...

hiyo +255 siyo ZIP Code bali ni International telephone code...ukitaka kunipigia simu yangu say....0713..000000...nawe ukiwa nje ya TZ unachofanya ni piga +255 0713 000000 hapo umenipata...mfano hiyo code Kenya ni +254 na USA ni +1

kwa habari zaidi kuhusu ZIP Codes tafadhali soma hapa: ZIP code - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Bado haijawa rolled out Tanzania nzima ila kuna pilot project ya postal code ilikuwa inajaribiwa Arusha ..... allAfrica.com: Tanzania: Arusha Switches to Zip Codes

Kwa ufupi kwa sasa bado hatuna postal codes kwa Tanzania.

Kwa nchi kama Tanzania hata kama wata-introduce hii system labda wajaribu kufungua matawi ya Posta sehemu mbali mbali ili watu wawe wanaenda wenyewe kuchukua barua zao huko.

Wakiingia na gear ya kutaka kuwa wana-deliver wao kwenye kila anwani sidhani kama wataweza, gharama ni kubwa sana kulinganisha na volume ya mail waliyonayo wao.

Wenzao huko wanaoendesha huo mfumo kwa siku wana-process mamilioni ya barua na vifurushi~pamoja na hayo bado gharama za uendeshaji zinawamaliza!.
 
Naombeni msaada wadau, anaejua POSTAL/ZIP CODE YA TANZANIA naomba anitajie

Hatuna huo mfumo kwa hapa bongo kuna wakati walisema mipango iko mbioni ili tuendane na wakati lakini naona miaka inaenda,watu wako busy kupata mipango ya uchaguzi 2015 na vi EPA vyao,

kuwa na postal/ZIP code kungetusaidia sana kwani ingekuwa ni rahisi kujua mtu anaishi wapi n.k,kwa bongo ni shida kweli hata hatuna mitaa,nyumba hazina mpangilio utakuta sebule inatazama na choo cha mtu,bado tuna safari ndefu kwenye mambo ya makazi
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Tanzania haina mfuma wa postal/zip code. +255 is area code ya simu kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom