Pori kuwa shamba mkoani Morogoro

Pori kuwa shamba mkoani Morogoro

Maninho21

Member
Joined
Apr 22, 2022
Posts
58
Reaction score
93
Ndugu zangu habari zenu.. nahitaji maoni na ushauri katika hili. Nahitaji kununua pori walau ekari 50 niligeuze shamba mkoani morogoro; ni wilaya gani mkoani morogoro ina ardhi nzuri hasa kwa kilimo cha mpunga. Gharama zake huwa ni bei gani ekari ya pori. Na kwa namna ya pekee kwa wale wataalamu wa ardhi ni mambo na hatua gani nizingatie kwenye kufanya manunuzi ili niepuke migogoro baadae.
Natanguliza shukurani za dhati.
 
Mapori yapo Mkuu, huko, huko moro. Sijajua umejipangaje kwa ekari.
 
Ningependa kujua wilaya gani inafaa kwa kilimo cha mpunga. Kuhusu kujipanga, naamini pori haiwezi kuwa gharama hasa kwa morogoro (nisahihishe) kwaajili nilikuwa nafikiri labda kiasi cha juu sana ni laki mbili kwa ekari
 
Mashamba yapo, maeneo ya Kilosa kuna mahali wanalima sana mpunga panaitwa Kilangali huko hata ukitaka heka 100 ni wewe tu na ni ya umwagiliaji, ila mauziano lazima wakuuzie serikali ya kijiji na sio mtu binafsi
Mashamba ni gharama sana kwa uwezo wangu wa kuanza kilimo. Nawaza kupata pori la ekari kadhaa nilisafishe nianze kilimo
 
Ndugu zangu habari zenu.. nahitaji maoni na ushauri katika hili. Nahitaji kununua pori walau ekari 50 niligeuze shamba mkoani morogoro; ni wilaya gani mkoani morogoro ina ardhi nzuri hasa kwa kilimo cha mpunga. Gharama zake huwa ni bei gani ekari ya pori. Na kwa namna ya pekee kwa wale wataalamu wa ardhi ni mambo na hatua gani nizingatie kwenye kufanya manunuzi ili niepuke migogoro baadae.
Natanguliza shukurani za dhati.
Nenda Malinyi huko Mlogolo.
 
Ningependa kujua wilaya gani inafaa kwa kilimo cha mpunga. Kuhusu kujipanga, naamini pori haiwezi kuwa gharama hasa kwa morogoro (nisahihishe) kwaajili nilikuwa nafikiri labda kiasi cha juu sana ni laki mbili kwa ekari
Mashamba yapo, Vianzi na Menge. Wilaya ya Mvomero, kutokea morogoro mjini unaweza tumia nauli kama 6000 hv kwa pikipiki, ukitokea Lukobe, lakini being sio hiyo mkuu, huku bei imechangamka kidogo kwa ekari ni 400000. Huku yanafaa zaidi kwa kilimo cha tikiti, alizeti, mahindi na mkonge. Pia unaweza kata viwanja kwa maana kuna makazi pia. Nb mimi sio dalali nakupa code tu.
 
Nimepokea mzee
 
Uzi mzuri sana huu, wenye taarifa kamili watupe tafadhali.
 
Back
Top Bottom